Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,278
- 8,493
RAIS Jakaya Kikwete amekubali kustaafu kwa lazima kwa Mwansheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, ifikapo Novemba 6, mwaka huu.
Bw. Mwanyika anastaafu kwa lazima katika kipindi ambacho Mkutano wa 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakuwa ukiendelea, ukitarajia kuhitimisha sakata la mkataba tata wa Richmond, ambao ulisainiwa wakati akiwa Mshauri Mkuu wa Serikali wa mambo yote ya kisheria.
Habari za kustaafu kwa lazima Bw. Mwanyika ambaye amekanusha mara kadhaa kuhusika kwake na Richmond, zimethibitishwa Dar es Salaam jana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Majibu ya maandishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa gazeti hili, iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano (OR-MUU) Bi. Zamarad Kawawa, ilieleza; "Bw. Mwanyika amekubaliwa kustaafu atakapofikisha umri wa kustaafu kwa lazima wa miaka 60 ifikapo tarehe 6 Novemba, 2009."
Hatua ya Bw. Mwanyika kukubaliwa kutaafu kwa lazima inaibua maswali mengi, hasa kwa kuzingatia kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 59, haina kipengele kinachoeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atastaafu baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
Kifungu kidogo cha (5) kinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atashika madaraka yake mpaka (a) uteuzi wake utakapofutwa na Rais au (b) mara tu kabla ya Rais mteule kushika madaraka ya Rais.
Kwa maana hiyo ya katiba Bw. Mwanyika angeweka kuacha kushika wadhifa huo ama kwa kuachishwa na Rais au kusubiri mwakani baada ya Uchaguzi Mkuu, kabla ya Rais mteule kushika wadhifa wa rais.
Kutokana na wadhifa wake huo, baada ya mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC kusainiwa, na baadaye bunge kuuda Kamati Teule ya kuchunguza utata uliogubika mkataba huo chini ya Dkt. Harrison Mwakyembe (Kyela), ilibainika kuwa utiaji saini mkataba huo ulisheheni makosa mengi.
Wakati akiwasilisha taarifa ya kamati iliyochungusa utiaji saini mkataba huo bungeni, Dkt. Mwakyembe alisema;
"Mkataba umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha serikali."
Dkt. Mwakyemba alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali, Bw. Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, hivyo, "Wawajibishwe na mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu," alisema Dkt. Mwakyembe wakati akiwasilisha mapendekezo ya Kamati yake kwa bunge kuhusu hatua alizopaswa kuchukuliwa Mwanyika.
Baada ya Kamati hiyo kutoa mapendekezo hayo, Serikali kupitia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ilitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya kamati, akisema kikatiba, Mamlaka ya Nidhamu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Kwa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, IKULU," alisema Bw. Pinda.
Hata hivyo, katika Mkutano wa 16 wa Bunge uliomalizika mjini Dodoma, Serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Adam Malima, ilitangaza utekelezaji wa awamu ya pili mapendekezo ya Kamati ya Dkt. Mwakyembe, ambapo alisema Bw. Mwanyika hakuwa na kosa analoonekana kutenda kutokana na wadhifa wake huo.
Bw. Malima alisema iwapo mtumishi yeyote wa umma atatajwa na watuhumiwa walioko mahakamani kuwa alihusika katika makosa ya jinai, Serikali haitasita kumfikisha mahakamani
Hata hivyo utekelezaji wa mapendekezo hayo pamoja na yaliyohusu maofisa wengine ulikataliwa na Bunge na kuiagiza Serikali kuwasilisha upya utekelezaji mwingine wa maazimio yake katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanzia Oktoba 27, mwaka huu siku tisa kabla ya Bw. Mwanyika kustaafu.
Source: Majira 06 October 2009
Mwandishi: Reuben Kagaruki