kikao cha kumjadili mrisho gambo cha kwama

Antar bin Shaddad

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
202
101
kikao cha sekretariet ya ccm mkoa Arusha kilichokutana leo kumjadili mjumbe wa baraza la vijana Taifa,mrisho gambo kimeshindwa kufanyika baada ya mashahidi au wanachama waliokuwa wanamtuhumu gambo kuwa alikihujumu chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana kushindwa kutokea.

kwa mujibu taarifa za ndani ya ccm kulikuwa na mashahidi 22 ambao waliandikiwa barua za kuja kujieleza na kuthibitisha tuhuma zao mbele ya mbele sekretarieti ya mkoa inayoongozwa na katibu wa CCM mkoa mary chatanda lakini hadi saa 10 jioni hakukuwa na shahidi aliyejitokeza kati ya hao 22 kuthibitisha madai yao ya kuhujumu CCM na hivyo sekretariet kumruhusu gambo akaendelee na shughuli zake.

gambo alituhumiwa kuwa alimhujumu mgombea wa ccm batilda burian wakati wa uchaguzi mkuu kwa kukataa kumpigia kura na badala yake alimpigia godbless lema wa cdm na tuhuma hizo zilitolewa na kundi la vijana baada ya gambo kutoa kauli kali mjini dodoma wakati wa kikao cha baraza kuu la uv-ccm kilichofanyika mwezi machi ambapo alitoa maoni kuwa chama hicho kinachukiwa na wananchi kutokana na kuwakumbatia mafisadi wa richmond EL na RA.

baada ya kauli yake hiyo mwenyekiti wa uv-ccm mkoa wa arusha james millya ambaye anafahamika kama mfuasi wa EL aliitisha kikao cha baraza la mkoa wilayani longido na kumvua gambo nyadhifa zake ndani ya uv-ccm hatua hata hivyo imeshindwa kutambuliwa na ngazi nyingine za chama hicho .

habari zaidi zinaeleza kuwa wakati chatanda akiwa ameitisha kikao cha sekretariet millya naye alikuwa anaendesha kikao cha kamati ya utekelezaji ya jumuiya yake katika ofisi za vijana ili wajumbe ambao walikuwa wameitwa kwenda kutoa ushahidi wasiende kwenye kikao cha sekretariet.

zaidi kuhusu kinachoendelea ndani ya chama cha magamba tutawajuza
 
Hao walevi tu wanaangaika! Huyu mary chatanda c ndiyo alipiga kura ya kumpitisha meya wa arusha wakati yeye ni diwani vitu maalum wa mkoa wa tanga! Haelewi anachokifanya ni nini, na bwana gambo wahawezi kumng'oa tena coz el ashapunguzwa makali yake
 
Back
Top Bottom