Kijana wa kikristo anatakiwa kukaa kwao hadi atakapooa hata kama ni miaka 50. Umasikini wa wazazi ndio unapelekea watu wakimbie kutafuta maisha

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,589
15,384
Kwa Mujibu wa maandiko mtu huoa kutokea kwao sio magetoni au alipopanga au kujenga.

Mzazi wa Kikristo anatakiwa kuwa na utajiri sio tu kuhudumia familia bali urithi kwa wajukuu wa watoto wake.
Mithali 13:22
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; <br>Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

Zab 112:3 SUV. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele


Isaka alioa akiwa na miaka 40. Alitokea kwao. Na huyu alikuwa anaongea na Mungu kabisa. Mwenyezi Mungu angeweza kumfukuza akatafute maisha. Ila hakukuwa na haja kwa sababu mzazi wake na baba yetu wa imani alikuwa anajua andiko la
Mwanzo 2:24
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.


Ni hayo tu.

Usimfukize mtoto wa kiume nyumbani hadi aoe.

Akioa haoaswi kuendelea kukaa hapo nyumbani ni dhambi. Mpe mali aanzishe taasisi yake na mkewe.
 
Back
Top Bottom