Kigoma: Nusu ya wanafunzi hawajafanya mtihani wa Darasa la Saba, utoro watajwa

Mungu atunusuru,wengi wao wamekimbilia mikoani kuwa wadada wakazi na machinga...
Wamejazana mitaani wakiuza chai na mitumba..wengine wanadeki na kuosha vyombo mijini tu..
Yaani kigoma,ukerewe,kagera,na visiwa vyote vya kanda ya ziwa ...ilo ni tatizo
 
Elimu yenyewe hata kama wewe ni msomi huoni hamasa ya kumshawishi na mwingine asome. Ni mwendo wa kusoma historia ya vitu badala kujifunza kuvifanya vitu vitokee. Kwa historia hizi zinazoendelea kufundishwa nawashngaa hata wanaosema elimu ni Ufunguo wa Maisha. Elimu ya bongo inachosha
 
Kama wamesoma na hawajafanya mtihani unahitimishaje kuwa watabakia wajinga?

Nyie ndiyo mnaoamini kufanya mtihani na kufaulu ndio kuondoa ujinga.

Unataarifa kuwa kunahatua mitihani inatarajiwa kufutwa kabisa?
 
Elimu ya msingi ni lazima kwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule. Sasa nafikiri kuna haja ya kuwawajibisha wazazi wa watoto ambao watatega kufanya mtihani au kuonesha utoro wa namna yoyote ile.
Kama wazazi watawajibishwa inabidi na serikali pia iwajibishwe kwa kushindwa kutengeneza fursa za kutosha za ajira kwa vijana waliosoma,,, sheria iwe ni msumeno isimbane mtu mmoja
 
Hali hii inasikitisha sana, yaani nilidhani Wazazi walishabadilika kumbe Bado watu wanaona Elimu Haina maana hadi leo hii, duu.

My Take: Kwa Hali hii, sidhani kama kuna siku wajinga watakuja kuisha hapa Tanzania.

========

KIGOMA; WAKATI wanafunzi wa darasa la saba wakimaliza mtihani wa elimu ya msingi nchini kote leo, imeelezwa kuwa mkoani Kigoma nusu ya wanafunzi hawakuweza kufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali ikiwamo utoro.

Ofisa Elimu wa Mkoa Kigoma, Paulina Ndigeza akizungumza mjini hapa jana alisema kuwa wanafunzi 53,000 walifanya mitihani yao kati ya wanafunzi 102,948 waliotarajiwa.

Ndigeza alisema pamoja na changamoto hiyo ya idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kufanya mtihani, alibainisha kuwa mwamko mdogo wa wazazi kuwasimamia watoto wao imekuwa changamoto kubwa na kwamba mkoa umeshaanza kutekeleza mikakati ya kupambana na changamoto hiyo.

HabariLeo
Matokeo ya kudharau sekta binafsi na wadau wa maendeleo kwenye kutafuta solution ya matatizo ndio matokeo yake haya..

Nakiri kwamba niliwapelekea tamisemi mfumo wa kudhibiti mahudhurio ya watoto wa shule tena bure kwa kuwashirikisha wazazi wao kila siku ila walichonijibu ni kuwa wanao teyari sasa hii idadi kubwa hivi imeshindwa kufanya mtihani kisa utoro kwann huo mfumo wao usingesaidia kuzua haya..

Hii nchi watendaji wa serikali mna mapuuza sana
 
Hakina maana ni useless takataka kabisa wala sina muda nacho
Unaona takakata si kwa sababu ni karatasi unayomiliki ila kwa sababu ya kile kilichobaki kichwani baada ya kukitafuta kwa zaidi ya robo ya maisha yako!

Kifupi ndicho kinakuweka mjini
 
Kama wazazi watawajibishwa inabidi na serikali pia iwajibishwe kwa kushindwa kutengeneza fursa za kutosha za ajira kwa vijana waliosoma,,, sheria iwe ni msumeno isimbane mtu mmoja
Serikali inaweza kusema haikusomeshi ili ikuajiri.
 
Ni ukweli unaosikitisha sana. Nilikuwa mkoa fulani nikakuta fundi anafanya finishing nyumba fulani na ana vibarua. Nikamuuliza alisomea wapi kazi hii. Akanijibu nikasome ili iweje ikiwa vibarua wangu hawa wawili ni graduate wa sheria?

Niliumia sana.
Hii imenikumbusha mbali aiseeee.
 
Elimu yenyewe hata kama wewe ni msomi huoni hamasa ya kumshawishi na mwingine asome. Ni mwendo wa kusoma historia ya vitu badala kujifunza kuvifanya vitu vitokee. Kwa historia hizi zinazoendelea kufundishwa nawashngaa hata wanaosema elimu ni Ufunguo wa Maisha. Elimu ya bongo inachosha
Very true
 
Wengi ni wakimbizi kutoka congo na Burundi wazazi wao wanawaza vita tu sasa elimu ya kibongo itawasaidia nini? Wale watanzania wanajua umuhimu wa elimu na ndiyo waliofanya mtihani
 
Elimu imekuwa useless ukijua kusoma, kuandika na kuhesabu inatosha.

Hakuna bright future kwenye elimu ya bongo.
Kuna point hapa Ila nashauri mtoto afike angalau kidato Cha nne,kwani ndio elimu ya msingi kwa Sasa.
 
Hali hii inasikitisha sana, yaani nilidhani Wazazi walishabadilika kumbe Bado watu wanaona Elimu Haina maana hadi leo hii, duu.

My Take: Kwa Hali hii, sidhani kama kuna siku wajinga watakuja kuisha hapa Tanzania.

========

KIGOMA; WAKATI wanafunzi wa darasa la saba wakimaliza mtihani wa elimu ya msingi nchini kote leo, imeelezwa kuwa mkoani Kigoma nusu ya wanafunzi hawakuweza kufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali ikiwamo utoro.

Ofisa Elimu wa Mkoa Kigoma, Paulina Ndigeza akizungumza mjini hapa jana alisema kuwa wanafunzi 53,000 walifanya mitihani yao kati ya wanafunzi 102,948 waliotarajiwa.

Ndigeza alisema pamoja na changamoto hiyo ya idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kufanya mtihani, alibainisha kuwa mwamko mdogo wa wazazi kuwasimamia watoto wao imekuwa changamoto kubwa na kwamba mkoa umeshaanza kutekeleza mikakati ya kupambana na changamoto hiyo.

HabariLeo
Jamaa wamekanusha wakati taarifa ikitokea na Habari Leo 🤪🤪

Sio Kila kitu ni kukanisha Ili kificha tatizo

View: https://www.instagram.com/p/CxNXsvCgcmU/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Upo sahihi mkuu mzazi wa kijijini/maskini hayupo tayari kuuza mali zake tena kwaajili ya kusomesha.

Anawatoto wamekaa nyumbani baada ya kugraduate, tofauti na matarajio aliyokuanayo mzazi.

Kipindi cha regime ya Kikwete ndio wakati ambao wazazi walihamasika kupeleka watoto wao shule kwasababu walikuwa wanaona wahitimu wanapata ajira punde tu baada ya kuhitimu.

Ajira ilitumika kama ndoano, kwamba ukisoma utapata kazi nzuri na kwa wakati huo wa Kikwete unaona kweli watu wanapata ajira.

Ndio maana, wakazi wa vijijini walihamasika kusomesha. Wale watoto waliopelekwa shuleni kwa hamasa ya ajira ndio hawa ambao wamezagaa mtaani bila ajira wala kazi zenye staha.

Utamwambia nini mzazi na mtoto wa kijijini/maskini akuelewe?
Umenena, japo wapo wanaoponda ooh mkwere Mbaya, wakati watu wamelamba kazi bwelee, watoto walisoma kwa Moyo wanajua nikimaliza nipo kazini, Leo hii wasomi waendesha bodaboda,masaidia fundi yaumiza Moyo kwa kweli.
 
Back
Top Bottom