Kifupi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Naona inakuwa mazowea ya kutoa kila mtu kujiona alifikirialo ni sahihi. Chama cha Demokrasia na Maendeleo kifupi chake ni CHADEMA, hii ipo kwenye katiba yao sasa pana WATAALAMU uchwala wanaotoa ufupisho mwingine wa CDM. Mie najiuliza WAASISI wa CHADEMA hawakuliona hilo???????????
 
Jamani kwani hapo kuna tatizo gani? Sijaona na sioni tatizo la CHADEMA kuitwa CDM bora unaelewa maana au huelewi maana?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
CDM ni kifupisho cha mitaani sio cha kikatiba sawa na marekani mtu Robert anaitwa bob, william anaitwa Bill haina tatizo ukishindwa kuita CDM ita CHADEMA ila ukiwa unagombea cheo chochote lazima uandike CHADEMA!
 
Naona mzimu wa Christian Democratic Movement (CDM) Unawasumbua
 
Naona inakuwa mazowea ya kutoa kila mtu kujiona alifikirialo ni sahihi. Chama cha Demokrasia na Maendeleo kifupi chake ni CHADEMA, hii ipo kwenye katiba yao sasa pana WATAALAMU uchwala wanaotoa ufupisho mwingine wa CDM. Mie najiuliza WAASISI wa CHADEMA hawakuliona hilo???????????
Nadhani watu wanataka urahisi tu wa kuwasiliana hasa humu kwenye mitandao ya kijamii na hivyo kujaribu kufupisha baadhi ya maneno. Binafsi sioni ubaya kama katika muktadha usio rasmi, mtu ataandika "CDM" badala ya "CHADEMA". Hata mimi nakiri kuwahi kuandika kwa ufupisho huo usio rasmi ingawa sidhani kama ninakidhi kuwekwa kwenye kundi lako la "WATAALAMU uchwala" [sic].
 
kama una kadi nenda kwenye namba ya kadi halafu tazama.usipoteze mda wa kufikiri vitu vya msingi.
 
Mkuu Jacobus, POLE kwa kukerwa na tabia hii, lakini ni vizuri kukumbuka
-Kuna lugha iliyo rasmi
-Lugha isiyo rasmi(kiswahili cha mtaani)

Sasa utumiaji wa lugha iliyo rasmi ni katika ki-ofisi zaidi katika machapisho, maandishi rasmi(official) (ingawa ilipaswa kutumika muda wote)

Lugha isiyo rasmi, hasa hapa JF ..hutumika kutokana na UFUPISHO wa uandishi tu, mfano badala ya kila wakati mtu kurudia rudia kuandika CHADEMA utakuta anaandika CDM ingawa angeweza ku-paste neno hilo kila alipohitaji kuliandika baada ya kuli_copy toka mwanzoni kupitia Computer, iPads, Tabs na simu (LAKINI inapaswa ujue SI wote wanao uwezo huo wa Ku-copy na Ku-paste katika simu zao.

-Lakini pia vijana wa siku hizi wana vifupisho sana visivyoeleweka mfano kwa neno fupi kama SIKU kuita "CKU" au neno la kiingereza "SO" kuliita "XO".. nadhani kwa neno kama hilo kufupishwa au kubadilishwa maana
hapo ndio kuna TATIZO lakini kwa neno kama CHADEMA kuitwa CDM sioni ubaya kwani ni herufi tatu za kwanza za Jina la chama(Acronym)

-Binafsi sioni shida sana kama watu wakiendelea kutumia isiyo rasmi ikiwa TUNAJUA wanamaanisha nini katika muktadha upi! Mfano wakati mwingine utaona
CCM-Sisiemu, CHADEMA-CDM n.k..shida ingekuwa kutumia neno lenye matamshi sawa ila uandishi tofauti(Homophones) kama "CAF" kumaanisha "CUF"!
Hapo?!..Hapo kungekuwa na shida.
 
Naona inakuwa mazowea ya kutoa kila mtu kujiona alifikirialo ni sahihi. Chama cha Demokrasia na Maendeleo kifupi chake ni CHADEMA, hii ipo kwenye katiba yao sasa pana WATAALAMU uchwala wanaotoa ufupisho mwingine wa CDM. Mie najiuliza WAASISI wa CHADEMA hawakuliona hilo???????????

sasa kama CDM haipo kwenye Katiba ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kuna haja gani ya kujadili? unawaambia watu wataalamu 'uchwala' wakati wewe mwenyewe ni mtaalamu uchwara! au huelewi maana ya Katiba?
 
Back
Top Bottom