Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Mkuu Pasco,
Katika hili mie sina haja ya kutafuna maneno!! Hata kama nimehuzunishwa na kifo, bado napinga kwa nguvu zote huyu binti kuhusishwa na hiki kifo! Ikumbukwe kwamba, Kanumba kwa Lulu ni Kama Daud kwa Golliath ..!! Sina shaka yoyote kwamba, kutokana na wivu wa kimapenzi, Marehemu alianza kumshushia kisago Lulu! Bila shaka, kwa jinsi wanaume tulivyo, asilimia kubwa ya wengi wetu tungechukua uamuzi wa marehemu wa kuanza kumshushia binti kipigo!
Kwa upande mwingine, Lulu alikuwa na haki ya kujitetea! Kama nilivyosema hapo awali, Lulu kwa Kanumba ni sawa na Daud kwa Golliath! Ninachomaanisha, asingeweza kuchapana nae hivyo suluhisho pekee kwake ilikuwa ni kujinasua toka mikononi mwa marehemu! Kama chumba kisingekuwa kimefungwa (may be kilifungwa ili kichapo kitolewe sawasawa na asiwepo wa kukimbia) basi suluhisho la Lulu lingekuwa kutimua mbio! Lakini kwavile mlango ulikuwa umefungwa, Lulu alilazimika kwanza ,kumsukuma marehemu ili apate nafasi ya kutimua mbio na kufungua mlango! Jambo hili, lingefanywa na yeyote yule with exception of very few! Hata ningekuwa mimi, nisingekuwa na njia mbadala zaidi ya hiyo ya kumsukuma Kanumbe ili nipate uchochoro wa kutimua mbio! Hivyo, vyovyote iwavyo, Lulu hakuwa na namna zaidi ya hiyo ingawaje ni bahati mbaya hatua yake ya kujiokoa imezaa mauti kwa mwenzake!
Tukija kwa mdogo wake Kanumba, huyo ndie mpuuzi kuliko wote .!!! Nazani ujinga kama sio upumbavu aliofanya ni kutaka kujaribu kuifunika hii issue kwavile aliona ingekuwa skendo kwa kaka yake!! Bila shaka, wakati akichelea kuchukua hatua ya kumpeleka hospitali au kuita majirani (ili kuficha skendo) kumbe ndo alikuwa anakaribisha kifo kwa kaka yake! Na hata hiyo hatua yake ya kuanza kwanza kumuita daktari wa Kanumba ilikuwa na lengo lile lile la kuficha skendo!
WASWAHILI WANASEMA, MFICHA MARADHI KIFO UMUUMBUA hiki ndicho kilichotokea kwa Mpendwa wetu Kanumba!!
Mimi naamini tunavuna tunayopanda. Trust me most of us don't know well Kanumba. His mysterious Death is just a manifestation of that fact. A tale tell sign that all was not that well behind the curtains!