Kifo cha Kanumba: Ni uzembe tu? Sio Lulu!

Mapema mno kumuingiza au kumta huyo Lulu kwani yeye na marehemu ndio waliokuwa ndani mpaka marehemu anakutwa na mdogo wake akitokwa mapovu mdomoni (umauti ukianza kumkaribia)Ikumbukwe kuna tahruki hapo msiwe kama hawa jayakuta na kama bado msiombe mumkute wenu akiwa kwenye hiyo hali ya umati (Hatua moja ngumu sana wewe muombe mungu aitoe roho yako kwa upole sana)kwa waislam semeni amini mliobakia sijui msemaje?
Mada..kifo ni kama vifo vingine vitatafuta sababu na wakati ukikaribia hamna jinsi.Hatujuani kamakweli sisi ni wazima au la wengine wanahisi ni wazima wa afya kumbe hamna kitu binadamu tuko kama hewa ikipuliza inakwenda zake na kuja nyengine kuumwa na kupona ni mipango ya mungu

Nakuachia swali wewe uliebahatika kusoma nilichoandika,Wanaokaa karibu na hospitali hawafi kwa ajali au kuumwa?
 
Pasco,

Kwa kweli umefanya uchambuzi mzuri wa kina,lakini sisi ni binadamu na linapotokea jambo kama hilo huwa linatengeneza kitu kinachoitwa panic especially kwa wale watu walioko karibu na muhusika,hebu tujiulize what is panic? Kwa ufupi Panic is a sudden sensation of fear which is so strong as to dominate or prevent
reason and logical thinking, hivyo unapopata kitu kinachoitwa panic inakua ngumu sana kufanya maamuzi ya busara,mtu labda kasukumwa kaanguka chini povu linamtoka kawa baridi lazima panic itokee,hatuna huakika kama alifariki palepale au baadae unless doctor awe amethibitisha.Kutokana na hiyo panic mie naweza kusema hayo maamuzi mazuri ambayo umeyachambua hapo hayakuweza kufanyika,watu wengine mtu anaangua anazimia anampigia baba mama au mke wa muhusika badala ya kumkimbiza hospitalini,kwa kweli vitu namna hiyo vinatokea,mtu ambaye angeweza kutoa ushauri mzuri ni huyo doctor wake lakini labda na huyo doctor naye binadamu labda alikumbwa na hili gonjwa panic.
 
Mbu hivi kweli kabisa niambie relevance ya hiLi hitaji la PF3 form...

...ni urasimu tu, pengine na utoe chochote wakuandikie fasta...

bht hakuna ni ujinga fulani tu, hili swala lilijadiliwa sana bungeni miaka ya 90 mwanzoni lakini wapi...PF3 liko tu!

ilitakiwa mtu anapatiwa huduma, hospitali wanatoa taarifa polisi, wakati anapatiwa huduma ..polisi wanakuja pale kuchukua taarifa kama majeraha ni criminal cases au la

....au kila hospitali iwe na police office kuratibu hizo PF3....

hata mahakama ikisema hana hatia..mtoto huyu kwa jamii hachomoki...ameishapatiwa a.k.a yake as 'serial killer'

...khaa, kiongozi...'serial' tena? Hapana bana...hi ni kesi ya awali...

huyu mdogo wake Kanumba nani kamruhusu kutoa maelezo na lawama? kwa nini ajitoe ilihali alikuwa nyumbani? kwa nini polisi walimuacha an hawakuondoka naye?

....kawaida ya mambo haya, ushahidi muhimu upande wa prosecutors wa kesi hii ushaharibika...
defence lawyer mzuri kwenye cross examination anauwezo mkubwa sana sasa kuipangua evidence ya
prime witness...
 
Waberoya, hapa umeongeza chimvi kidogo. Killer? YES, but a Serial Killer? Mhhh, kwani Kanumba ni wa pili, tatu, ......?

a.k.a zinazotolewa na waswahili zina maana nyingi sana mkuu

'eti' wanasema bado ray

wengine wanasema ametumiwa na freemason

wengine wanasema ametumiwa na UWT kwa sababu kanumba alisema atagombea ubunge kwa tiketi ya chadema shinyanga mjini

wengine wanasema kale ka-ugonjwa ndiko kanapelekea apewe hiyo aka


sio mimi mkuu ndio wanavyosema......atapewa a.k.as nyingi mno!!
 
Watunga sheria hawajali maana wao huwa wanatibiwa wakisema tu "Mimi mbunge" hawaoni umuhimu wa kusawazisha sheria

Sijui mantiki gani inayotusukuma watanzani kutaka PF3 kwanza kabla ya tiba....

Sisi si wazima kichwani
Umegandisha mno mawazo yako. kama mgonjwa ana hali mbaya anapokelewa Hospitali, PF-3 inafuata baadae baada ya taarifa kufika polisi. kwa kukusidia,ukiona mtu yupo serious,wengine wanampleka Hospitali na wengine wanakwenda Polisi.
 
Binafsi sijawahi kuwa mpenzi wa movie star yeyote wa bongo. Nimekuwa naangalia movie za Kanumba na wasanii wengine kupitia mabasi niendapo mikoani, na nimemfahamu huyo LULU kupitia huu msiba.

Ni wazi kabisa huyu LULU hawezi kuepuka kunyooshewa vidole kwa kuwa ndiye mtu wa mwisho aliyekuwa na marehemu angali mzima. Nenda uendako, LULU atakuwa mshukiwa wa kwanza. Hasa ukizingatia alikimbia baada ya kutoka kwenye chumba ambacho Kanumba alikuwa kaanguka akiwa kapoteza fahamu na anahitaji msaada (Naamini alikuwa amechanganyikiwa baada ya kukumbana na hali hiyo).

Ninamwonea huruma kwa shida anazopata binti huyu na jinsi saikolojia yake itakavyoharibika, ila sijui kama anastahili au hastahili. Haijalishi kama Kanumba alikuwa anacheza karate au alikuwa na umbile kubwa bado binti huyu anaweza akawa anahusika au hahusiki na kifo hiki. Poleni sana ndugu na jamaa za Kanumba na LULU ambao kwa wakati huu mnapitia kipindi kigumu sana.

But She can not escape this unless the court clear her of any wrongdoing. LULU is still guilty until proven otherwise.

I read you mkuu....We are what we live.The girl has been looking for trouble for a very long time and i definitely think that this time she has hit the jackpot.
 
Ok,
so wangemuua kwasababu na yeye kaua?

....ahhh, mob justice ya kibongo, wangem skin alive yule binti....na alivyo na
'bahati' mbaya, nani angemsikiza her side of story?

Amepata ushauri mzuri kutosema/kutotoa ushahidi wowote bila wakili wake, halafu
wabongo wengi hatujui umuhimu wa hili...

Mdogo wake Kanumba 'District attorney office' au police wangemu warn asiropokwe
kuepusha kuharibu ushahidi...
mfano; anasema walikuwa anawasikia tu wakigombana, hakuwaona! Iweje a speculate
Lulu alimsukuma?

kwa mtazamo wangu, Lulu bado innocent until proven guilty, considering her physique compared
na Mar SK.
 
Pasco kwa kuwa umeonyesha 'upendo' kwa Lulu kuwa aachiwe huru..ili bandiko la Kitalolo kwenye thread nyingine inaweza kumtoa Lulu...kumbe marehemu alikuwa na kesi nyingi tu za kupiga wanawake!!

akishinda kesi mwambie awe anarudi nyumbani saa kumi jioni!!! mpaka atakapokuja kuchumbiwa, kutolewa mahari na kuagwa kwa sendoff...ndivyo mabinti wa kiafrika wanavyotakiwa kuishi!!



HII NILIISOMA KULE GLOBAL NA HUWA KILA MARA NILIKUWA NIKIMWONA KANUMBA NAKUMBUKA HII NA MWISHO NILIPOSIKIA HABARI YA KIFO CHAKE NA CHANZO CHAKE STORY HII ILI- CLIK KWENYE KICHWA CHANGU

kanumba anahitaji tiba

Posted by GLOBAL on October 4, 2011 at 9:30am
View Blog

Madaktari wasema anaumwa Personality Disorder
Steven Charles Kanumba ni staa mkubwa Bongo. Jina lake kwa sasa lina hadhi ya kimataifa. Inawezekana akawa ndiye msanii kijana mwenye mvuto kijamii kuliko mwingine yeyote.

Mvuto wake unatambulika ndiyo maana makampuni mengi ya kibiashara na kijamii hupenda kumtumia kama balozi wao. Kanumba ni fahari ya Tanzania, ni kivutio cha vijana wengi wa kizazi kipya.

Lengo la makala haya ni kumshauri Kanumba. Pamoja na sifa nyingi alizonazo kuna makosa machache huwa anayafanya, hivyo anahitaji kupokea ushauri ambao utamsaidia kuepuka visa vya hapa na pale ambavyo humvunjia heshima.

MATATIZO NI NINI?
Hapa kuna baadhi ya matukio ambayo yamewahi kuripotiwa, hivyo kumchafua Kanumba, kwa hiyo anapaswa kujitenga nayo ili heshima yake ibaki kuwa juu.

MOSI: Ugomvi na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu mpaka kufikia hatua ya kupelekana polisi.
PILI: Sylvia Shally alikuwa mpenzi wake lakini naye waligombana mpaka kufikishana polisi. Mrembo huyo alitinga ubaoni akidai Kanumba alimtishia maisha.

TATU: Alizama kwenye dimbwi la mahaba (kama alivyodai mwenyewe) na Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed. Walipoachana, alifunguka kuwa mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, alikuwa anamtesa sana.
NNE: Anadaiwa kuwa na uhusiano wa siri na Aunt Ezekiel (ingawa wote wanakanusha), juzikati walitibuana, kisha yeye alimpa mitama mrembo huyo na kusababisha soo hilo litinge polisi.

ISHU IKOJE?
Kwa nini kila siku ugomvi na wanawake? Inakuwaje polisi na yeye kwa makosa ambayo yana alama za kimapenzi?
Daktari aliye pia bingwa wa saikolojia, Godfrey Chale aliiambia Showbiz kuwa tatizo linalomsumbua Kanumba linaitwa Personality Disorder na tiba yake ni ushauri na nasaha.
"Personality Disorder ina matawi mawili, inferior (kujihisi unyonge) na superior (kujiona unahitaji kuogopwa). Vitu hivyo hutengeneza wivu na migogoro mingi (conflicts).

"Mtu kama huyo atakuwa anajiona superior, kwa hiyo hujikuta ana chembechembe za dharau kwa kuamini ni maarufu na ni lazima mpenzi wake amnyenyekee. Ikiwa atakutana na hali tofauti, mfano akigundua mwenzi wake hafuati anavyotaka au anamsaliti, kwa kawaida hujisikia vibaya.

"Ile tabia ya kujiona superior ndiyo humfanya ashindwe kukubali matokeo hasi kutoka kwa mwenzi wake, kwani anaamini yeye ni mtu wa kunyenyekewa. Kutokana na hilo, ndiyo maana hupata kesi za kugombana au kusumbuana na wapenzi wake kwa sababu ya kutokubali matokeo," alisema Dk. Chale ambaye ana hospitali binafsi, pia hutoa ushauri wa afya kupitia magazeti ya Global Publishers.

Dokta Patrick Mirumbe wa Hospitali ya Capricorn alisema: "Tatizo lake ni wivu. Hiyo naweza kuzungumza kwa kifupi na tiba yake ni ushauri na nasaha. Akipata ushauri wa kutosha anaweza kubadilika na kuwa mtu safi.

KANUMBA ASHIKE NINI?
Mwanasaikolojia ambaye hutoa ushauri wake kwenye magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota alisema kuwa jambo ambalo Kanumba anapaswa kushika ili kuepukana na vitu ambavyo vinaweza kushusha heshima yake ni kujitambua.

"Katika makundi ya saikolojia, lipo linaloitwa Legal Psychology. Hili linamtaka mtu atambue mazingira anayoishi na ufahamu wake. Kanumba anatakiwa ajijue yeye ni mtu maarufu na heshima yake ipo juu, kwa hiyo asipojitambua itakuwa tatizo sana.

"Namuomba Kanumba ajijue yeye ni nani, awe mwepesi kuepukana na shari ndogo ndogo ambazo mwisho wake huwa ni mbaya, kama kupelekana polisi. Nadhani akijitambua, akiwa mwepesi kuelewa dalili za ugomvi, ataweza kujirekebisha.
"Anaweza kwenda kwa washauri zaidi lakini hapa mimi nampa kitu muhimu zaidi na akishike. Anaweza kuishi kwa amani maisha yake yote bila migogoro. Akijitambua, hata anapoachana na wapenzi wake, amani itatawala na hakutakuwa na fujo za polisi," Manyota.

HITIMISHO
Naamini kuwa maneno ya madaktari akiyashika sawasawa pia ushauri wa mwisho wa mwanasaikolojia Manyota, bila shaka atashinda mitihani inayomkabili. Lengo ni kuona heshima yake inazidi kupaa juu na msimamo ni kwamba Kanumba bila polisi inawezekana.

IMEANDIKWA NA LUQMAN MALOTO


MY TAKE: Tujaribu kuwa tunafwata ushauri wa wataalamu pengine leo tungekuwa tunaongea tofauti
 
Foundation, asante kwa hoja hii. Mimi naamini katika kweli daima, na ni kweli siku zote ndio husimama. Haka kabinti katatakiwa kusema kweli. "Lulu should tell nothing but the truth" na kwa kutumia hii kanuni "Seek the truth and the truth will set you free" katakuwa huru!.

Mkuu Pasco naamini kabisa ni wewe ndio unaandika haya kwa hisia za kuona LULU anaonewa badala ya kuangalia sheria inataka nini
Unaposema "ukweli utamuweka huru", what if ukweli wenyewe kama ni walikuwa wanapigana akamsukuma akaangukia kichwa, is this will set her free?

Maana unasema as if huo ukweli wa kumuweka huru wewe unaujua...................
 
Umegandisha mno mawazo yako. kama mgonjwa ana hali mbaya anapokelewa Hospitali, PF-3 inafuata baadae baada ya taarifa kufika polisi. kwa kukusidia,ukiona mtu yupo serious,wengine wanampleka Hospitali na wengine wanakwenda Polisi.

Wengine wende polisi wengine hospitali, kwani kila anaefikwa na tatizo kunakuwa na watu wengine?
Mbona tunatakiwa kuishi maisha ya kijima hivi? Kuwa mimi lazima mambo yangu ayajue jirani?

Watanzania mnachosha
 
Binafsi sijawahi kuwa mpenzi wa movie star yeyote wa bongo. Nimekuwa naangalia movie za Kanumba na wasanii wengine kupitia mabasi niendapo mikoani, na nimemfahamu huyo LULU kupitia huu msiba.

Ni wazi kabisa huyu LULU hawezi kuepuka kunyooshewa vidole kwa kuwa ndiye mtu wa mwisho aliyekuwa na marehemu angali mzima. Nenda uendako, LULU atakuwa mshukiwa wa kwanza. Hasa ukizingatia alikimbia baada ya kutoka kwenye chumba ambacho Kanumba alikuwa kaanguka akiwa kapoteza fahamu na anahitaji msaada (Naamini alikuwa amechanganyikiwa baada ya kukumbana na hali hiyo).

Ninamwonea huruma kwa shida anazopata binti huyu na jinsi saikolojia yake itakavyoharibika, ila sijui kama anastahili au hastahili. Haijalishi kama Kanumba alikuwa anacheza karate au alikuwa na umbile kubwa bado binti huyu anaweza akawa anahusika au hahusiki na kifo hiki. Poleni sana ndugu na jamaa za Kanumba na LULU ambao kwa wakati huu mnapitia kipindi kigumu sana.

But She can not escape this unless the court clear her of any wrongdoing. LULU is still guilty until proven otherwise.

mkuu ni hivi

binti ana miaka 18 tu!

alitakiwa muda huo na saa hiyo awe kwao ndani!! asubiri posa, na sendoff ndio aende kwa mumewe!

ni heri yako umesema haumjui...but believe me...kwa wasanii wa kike wengi wanasema 'AFADHALI' ...kakome...kamezoea.....sasa mwisho wake......wengine wanafanya furaha

mama yake alikashindwa haka katoto

the girl started this long ago....kuna wabunge wetu wamezama pale wengi tu...hawa vijana vijana...ninaposema vijana vijana sija refer Malima tu
 
Back
Top Bottom