Power G
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,886
- 1,194
Asema anaamini kuuawa kwake si sahihi
Ahofia yanayotokea Libya kuingia nchini
Ahofia yanayotokea Libya kuingia nchini
Akizungumka katika misa ya mavuno ya Parokia ya Mtakatifu Petro Oysterbay jana ambako pia aliendesha harambee na kufanikiwa kupata Sh milioni 111.65 zikiwa ni fedha taslimu na ahadi, Pinda awataka Watanzania kuenzi amani iliyopo nchini kwani yanayoendelea katika nchi za jirani yanatisha na si ya kuomba yatokee kwa Watanzania.
"Tuangalie yanayotokea Libya, si mambo mazuri hata kidogo. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa kifo cha Gaddafi si sahihi hata kidogo, ni bora angekamatwa akashtakiwa kuliko watu kujiamulia kutoa roho ya mtu mwingine hivi hivi. Watanzania tuombeane tusifike huko," alisisitiza.
Source: Nipashe
My Take: Iwapo CCM wataendeleza jadi yao ya kubaka demokrasia na kuchakachua katiba ili watawale daima, wajue wazi kwamba ya Libya yatawakuta tu.