Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Mwenyekiti wa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki - EAC - jana alijisalimisha kwa polisi kutokana na kutoa kauli ya uzushi na yenye kudhaniwa ilikuwa ya kichochezi pale alipodai mmoja wa wastaafu hao aliyemwagiwa maji moto yenye kuwasha sana maarufu kama "maji pilipili" alikuwa ameuawa na maji hayo.
Baada ya mzushiwa ufu huyo kuibuka na kudai maji hayo yalimpa madhara madogo tu lakini hayakumuua basi polisi walianza msako mkali wa kumtafuta kibosile yule wa EAC ili wamfikishe kwenye mahakama kwa uchochezi na uzushi.
Kibosile tajwa alijisalimisha polisi na kukiri ya kuwa taarifa zake hazikuwa sahihi na hivyo aliomba msamaha.
Haikufahamika mara moja kama polisi wataendelea na hatua zao za kumfikisha mahakamani au wamemsamehe. Lakini afande Kova ambaye ni mtu wa busara sana ninahisi atakuwa amemsamehe ili mradi asirudie tena kutoa taarifa ambazo hana uhakika nazo...............