dazu
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 365
- 76
Kwa wale wanajamvi wenzangu ambao ni wakongwe kidogo na wafuatiliaji wa soka, bila shaka tutakua tunakumbuka kwamba kulikua na timu ilikua inajulikana zaidi kama kiboko ya vigogo. Nayo ni Reli ya Morogoro. Kikosi chao cha miaka hiyo huwa kinanivutia hata leo, kwa jinsi kilivyokua kinatoa wakati mgumu kwa timu kongwe kama simba na yanga. Kikosi hiki golini alikua anasimama Athumani Msumari, Full beki 2 Mohamed Mtono, 3 Abdalla Mkali, 4 ni Ramadhani Kilambo, Sentahafu Gasper Lupindo, namba 6 ni Christopher Maiko, winga namba 7 ni Nassib Abbas namba 8 Yusuph Macho wakati mwingine hucheza Bonifas Njohole, Sentafowadi yupo Duncan Butinini, namba 10 David Mihambo halafu winga ya kushoto hucheza Mbui Yondan au Peter Mjata. Kikosi hiki ambacho kilikua chini ya Simkoko, Kilikua ni hatari mno hasa kinapokutana na yanga au simba.