Kibao kiko mbioni kuwageukia waliokuwa wanamcheka/kumkejeli Edward Lowassa na kundi lake!

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Historia ya CCM imejaa maajabu ambayo kama siyo taranta ya wepesi wa kusahau waliobarikiwa Watanzania wengi kwa sasa CCM ingekuwa ni chama kilichobaki kwenye vitabu vya historia achilia mbali ya kuwa chama cha upinzani nchini.

Tarehe 7 Februari 2008 ilikuwa ni siku iliyoingia kwenye vitabu vya histoaria baada ya Waziri Mkuu wa Serikali ya CCM kwa mara ya kwanza kujiuzuru kutokana na kuhusishwa na kashfa ya ufisadi kupitia kampuni ‘’feki’’ iliyokuwa inaitwa Richmond Development Company LLC.

Hii ilikuja baada ya Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge alipoamua kutaja mambo waliyodokezwa kwenye tume na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliposema Richmond ilikuwa mradi wa Bwana Mkubwa na Mshiriki wake mkubwa kibiashara akimaanisha Edward Lowassa na Rostam Aziz.

Repoti ya Tume ya Bunge kuhusu sakata la Richmond iko
HAPA

Baada ya Kamati Teule ya Bunge kusoma taarifa yake tarehe 6 Februari 2008 kuhusu sakata la Richmond Development Company LLC, Edward Lowassa akajikuta akiwa mmoja wa maadui namba wani wa taifa.

Baadaye Februari 5, 2011 kwenye sherehe za miaka 34 ya CCM mjini Dodoma, tukasikia Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Jakaya Kikwete akiwaasa wana-CCM kwamba itabidi CCM ijivue gamba.

Tarehe 16 Julai 2011 tulishuhudia Samuel Sitta, Dkt. Harrison Mwakyembe, Nape Nnauye, Lazaro Nyalandu, Ole Sendeka, Prof David Mwakyusa , Asha Abdallah Juma na viongozi wakuu wa CCM Mkoa wa Mbeya wakijitokeza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Mbeya katika lengo la kuufikisha ujumbe wa kujivua gamba. Hawa walikuwa ‘’vinara’’ wa mapambano yaliyopelekea kujiuzuru kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kuwa public enemy number one.


Nape-1.jpg

Samuel Sitta, Dkt. Harrison Mwakyembe, Nape Nnauye, Lazaro Nyalandu, Ole Sendeka, Prof David Mwakyusa , Asha Abdallah Juma na viongozi wakuu wa CCM Mkoa wa Mbeya wakielekea kwenye mkutano wa hadhara, Mbeya katika lengo la kuufikisha ujumbe wa kujivua gamba.

Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Harold Wilson aliwahi kusema, A week is a long time in politics.

Miaka minne baadaye, tunaanza kushuhudia wale waliokuwa wanataka kuwavua magamba kina Edward Lowassa na kundi lake wakiwa katika hati hati ya kuanza kuchekwa na waliokuwa wanawacheka au wako ukingoni kukosa kazi au kufukuzwa ndani ya CCM!.

Vyombo vingi vya vya habari kwa sasa hivi vinawashambulia wapinga rushwa/ufisadi ndani ya CCM kiasi kwamba hata jamii imeanza kununua hoja za vyombo vya habari kwa kuwaona wapinga rushwa/ufisadi kama ni debe tupu. Money talks hasa kwenye jamii yenye ufinyu wa uelewa!

Kuna uwezekano mkubwa wanaojiita CCM Imani/wapinga rushwa/ufisadi ndani ya CCM wako mbioni kufagiwa na kutupwa nje ya CCM na fagio la mafisadi

Wapinga rushwa/ufisadi are about to learn a stern lesson about the vigour of mafisadi!.

Mmarekani aitwaye Jim Henson aliwahi kusema, If you can't beat them. Join them.

Kuna baadhi ya wapinga rushwa na ufisadi wameanza kukubaliana na maneno ya Jim Henson!

Hii ndiyo Tanzania!
 
Kuna wengi watakuambia umetumwa na Lowassa, lakini kwa watu wanaoangalia hali halisi ndani ya uwanja wa vita (kama mimi) watakupongeza. Watakupongeza sio kwasababu wanapenda mafisadi washinde ila kwasababu wanaona mafisadi wameshakamata kila kona na sisi wanyonge tupo katikati bila msaada. Najua hata wewe (kama mimi) unahuzunika kwa mafisadi kuonyesha dalili za wazi za ushindi....
 
Hiyo ni tamthilia au hadithi au story au makala ya habari au maelezo au ujumbe au taarifa au onyo au ushauri au kichwa chako...!!

Ur mixed up, confused and diffused to public...!!!
 
Hiyo ni tamthilia au hadithi au story au makala ya habari au maelezo au ujumbe au taarifa au onyo au ushauri au kichwa chako...!!

Ur mixed up, confused and diffused to public...!!!
Mkuu;
Hii ni vyote ulivyovitaja kutegemea na fikra na mtazamo wako.
 
Kawaulize waghana kipindi cha JJ ambaye alipinga ufisadi na serikali ilio kuwa madarani ikatakumnyonga siku ya kumnyonga jeshi likahasi mpaka leo Ghana ipo na imesonga mbele siamini kama tutakuwa na viongozi wajinga amambao watakupali mafisadi wapite siamini siamini na nina imani kuliko hilo litokee jeshi bora lishike hatam na hilo ndio ninalo lisubiri waibe pesa zetu watuonge pesa zetu nawatusulubishe kwa pesa zetu bora jeshi lishike hatam basi.
 
SIRI YA MTUNGI IJUAE NI KATA......

KITRNDAWILI TEGA TEGA NIKUTEGE MWIBA......

USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA......./ii
 
Unaonekani unapinga rushwa/ufisadi lakini baadhi ya maneno uliotumia kwenye "heading" yako yanatia shaka kama kweli una dhamira ya kupinga rushwa/ufisadi.
 
Kumbe Live and fine performing arts ndo inawafanya mfikilie jamaa yenu atakanyaga Ikulu ama mmesahau kozi yake inamfanye kuwa muigizaji mzuri sana, anachokifanya Lowassa ni kuapply maigizo huko mikoani alafu na nyie mnashindwa kulitambua hilo na mnashindwa kutambua CC haikuundwa kusimamia maigizo bali taratibu na kanuni za chama ...endeleeni kushsbikia maigizo shauri lenu
 
Back
Top Bottom