Kibaden, Julio Ouuut Simba

Hapo ndipo nachoka kabisa na soka la bongo! Simba timu yangu ila mambo mengine yanahitaji subira. Hakuna kosa baya kama kuwaweka Julio na Kibadeni wafundishe at the same time, wangepaswa kumpa mmoja wao na mwingine wampe kazi ingine.

Liwalo na liwe

Inaumiza sana hii mkuu,binafsi mimi si mshabiki wa simba lakini maamuzi haya hayakupaswa kuchukuliwa wakati huu,simba haiko katika nafasi mbaya,simba ya sasa imebadilika na wanafanya vizuri tena sana,ilikuwa ni vyema sana wakatoa muda na hasa huu wa miezi mitatu ya mapumziko.
 
Dah pole sana kibadeni. Huyu mzee amefanana sura na sir elton john.
Kibaden wangemwacha pale hakuwa na uhuru wa kuifundisha ile timu akiwa na Julio. Julio ndo kamharibia Mzee wa watu yule alivyo makini! Aliifikisha kagera sugar mbali sana! Ila li JUU HILO ndo lilitakiwa kuondoka!
 
Sina hakika kama simba imetibu tatizo kwa kuwatimua King Kibadeni na Julio,inawezekana wanamchango wa tatizo lakini je aina ya wachezaji wetu wa Simba nayo siyo tatizo jingine?Ninachokiona hapa na kwamba sisi Simba tunatishwa na kivuli cha Yanga na kwa hali hii tarehe 14th Dec mechi ya mtani jembe kati yetu na Yanga itakuwa ishu kubwa.Safari hii malkia wa nyuki hayupo,huyo mzungu sijui nani atajitokeza kuokoa jahazi kwa kumlipa mishahara yake.Hadi leo Patrick Lewing yupo hapa bongo anaidai Simba,haijamalizza madeni imeleta mzungu mwingine ambaye naye atafukuzwa tu wala hana muda.Afadhali timu wangemkabidhi tu Matola amalizie mzunguko wa pili,

Nimechoshwa na ubabaishaji wa viongozi wetu Simba.Kimoja ambacho kamati ya utendaji imekifanya kwa usahihi na ninawapongeza ni kutuondolea mwanasiasa katika timu.akajiandae na uchaguzi mkuu ujao kwani huko nako kama anababaisha kama alivyokuwa akifanya Msimbazi basi amekwisha
 
wazo la Malkia lilikua zuri kwamba kwa sasa simba haishiriki michuano yyte ya kimataifa, kwa nn tuwe na kocha anayelipwa madola ila sbb watz ni watu wa BRN basi tumeshahererereka kuwa na mzungu maana bila kuona ngozi nyeupe hatuamini kama soka litachezwa
 
Kibaden wangemwacha pale hakuwa na uhuru wa kuifundisha ile timu akiwa na Julio. Julio ndo kamharibia Mzee wa watu yule alivyo makini! Aliifikisha kagera sugar mbali sana! Ila li JUU HILO ndo lilitakiwa kuondoka!

hizi timu kubwa huwa zinang'ata na kutema
 
Back
Top Bottom