Ki-Man u Man u /EL Mangush

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Wakati umeenda wapi wana JF?

Napata uchungu nikikumbuka raha iliyokuwa inapatikana kwenye michezo wakati ule, nilisoma Tanga na wakati ule tulikuwa na timu mbili daraja la kwanza African Sports (wana Kimanumanu) na Coastal Union (El Mangush) palikuwa hapatoshi hasa watani hawa wa jadi walipokuwa wakikutana.

Nyimbo za vijembe '' KIMANUMANU KINAMANUMANUA AASEGA SEGA KAULEGEZA'' ''KIMBWA KOKO CHATEMBEA NA WAHINDI CHARINGA NINI'' washabiki maarufu akina Bwana Kaka,Power Jabir Kababayee.

Wachezaji kama Twaha Omari, Victor Mkanwa, Mhando Mdeve, Kurwa Shaaban, Yasin Napili, Juma Mgunda, Ali Maumba na wengine wengi, leo hii kumepooza, wanaopajua na waopasikia Tanga nawauliza kunani pale?
 
hamna zama zisizo na mwisho my furendo.
hata Tukuyu Starz na Mecco hazipo tena,
Sigara na Pan imebaki historia.
Watoto wa Askofu Arusha wala hawapo kwenye ramani ya hii dunia tena.
 
Mwadui na Biashara za SHinyanga
Tumbaku na Reli Morogoro
CDA na Kurugenzi Dodoma
Kariakoo Lindi
RTC Kigoma
Bandari Mtwara
 
Nakumbuka mechi ya kwanza Coast na African Sports, Mzee Balozi Majid alikwenda kuwaambia WADIGO kuwa leo kuna vita ya WADIGO na WAMANGA!!!
 
Mwadui na Biashara za SHinyanga
Tumbaku na Reli Morogoro
CDA na Kurugenzi Dodoma
Kariakoo Lindi
RTC Kigoma
Bandari Mtwara

Zote hizi hazipo au zimelala usingizi na kipindi hicho si kila siku mshindi yanga au simba tu. mwamuzi dakika 90.
 
raha hakuna tena miaka hii, ya kale ni dhahabu ndugu yangu, vitu vilikuwa ni original,

Mpira kupasuka uwanjani sio mchezo
 
raha hakuna tena miaka hii, ya kale ni dhahabu ndugu yangu, vitu vilikuwa ni original,

Mpira kupasuka uwanjani sio mchezo

Kituko unanikumbusha Yasin Napili wa Coastal Union alibaki na kipa, pira likapasuka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom