Khutba ya Ijumaa ya wiki iliyopita kutoka mtukufu wa Al Aqswa Palestina

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Khutba ya ijumaa wiki iliyopita naitafsiri kutoka katika msikiti mtukufu wa tatu duniani msikiti mtukufu wa (Aqswa) uliopo katika mji mkuu wa palestina (Al Quds) ambayo imetolewa na Sheikh (Muhammad Hussein) Mufti wa Quds na Palestina , na haya ni baadhi ya aliyoyasema.

"Kutoka juu ya mimbari hii takatifu mimbari ya msikiti wa Aqswa uliyobarikiwa na kibla ya kwanza tunapeleka salamu zetu za baraka kwa ndugu zetu waliothubutu huko Gaza ya izza na utukufu tukimuomba ALLAH awape msaada kutoka kwake kwani yeye ni muweza wa hilo.

Enyi waumini wakaazi wa mji wa Israa na miiraj ALLAH anatuambia katika hali ngumu kama hii: (Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Sala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui) na amesema ALLAH akiwapa rambi rambi waislamu: (Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda.

Na wabashirie wanao subiri,) , enyi vijana wa Israa na Miiraj huu ni mwenendo wa historia na hii ndio historia ya mtume Muhammad kwani alizingirwa na kushambuliwa na jamii mbali mbali lakini alisubiri na akathibiti na akabeba daawah hii ya Uislamu kwa utukufu akiutetea uislamu kwa kila njia aliyopewa"
 
Khutba ya ijumaa wiki iliyopita naitafsiri kutoka katika msikiti mtukufu wa tatu duniani msikiti mtukufu wa (Aqswa) uliopo katika mji mkuu wa palestina (Al Quds) ambayo imetolewa na Sheikh (Muhammad Hussein) Mufti wa Quds na Palestina , na haya ni baadhi ya aliyoyasema.
Tafsiri yako hola inaweza kuwa chai tu iwapo hutaambatanisha ile hotuba og ya sheikh Muddy
 
Back
Top Bottom