Kesi zinazoikabili JamiiForums: Serikali ya Rais Magufuli kweli ina dhamira ya kupambana na ufisadi?

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Wakuu,

Leo nimefanya kuzipitia kesi zinazoikabili JamiiForums (kimsingi mimi nazichukulia kama kesi dhidi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti kwa ujumla) na kusoma mashtaka yanayowasilishwa na Jamhuri huku mashahidi wakidhihirisha kuwa kuna msukumo nyuma ya kesi hizi.

Tuwe wakweli, Rais Magufuli na vyombo vya dola vinayo dhamira ya kupambana na ufisadi kama wanavyojaribu kuuaminisha umma?

Kama kweli Serikali hii kupitia ofisi ya DPP wameweza kufuta kesi zilizoonesha walau dalili za ukweli (dhidi ya Manji, Masamaki n.k) kwanini wanaendelea na kesi hizi?

Serikali yenye dhamira ya kweli kupambana na ufisadi inatumia chombo chake (Polisi) kupambana na platform ya wananchi kukamata yeyote anayeanika ufisadi/uozo tena wa kampuni binafsi? Does this make sense? Huko kwenye serikali ya Magufuli kuna think tankers?

Nakumbuka Nape akiwa Waziri wa Habari aliviambia vyombo vya habari viendelee kuibua taarifa zote za kifisadi na Rais Magufuli anayo dhamira ya dhati ya kupamba na waliokuwa wakiibia nchi.

Ni wakati huo hapa JF ulianzishwa mjadala ambao kwangu nilichukulia kama unaunga mkono jitihada za Rais, waliotiririka kwenye mnakasha huu watakuwa salama na serikali hii? Soma Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...

Pia, hapa JF upo uzi unaoongelea mafanikio ya Rais Magufuli; Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020 lakini shaka langu ni kama kweli haya mafanikio yanaendana na mafanikio ya kuruhusu Uhuru wa Kujieleza.

Ukisoma kesi 3 zinazoikabili JamiiForums inakufanya ufikirie mara mbilimbili; Is Magufuli for real?

Mfano:
Kesi namba 456, anayetuhumiwa kwa ukwepaji wa kodi/uchakachuaji mafuta ni Oilcom, shahidi wa Jamhuri ni Askari Polisi. Yaliyomo kwenye kesi hii si kama yanashangaza tu bali yanakera kutambua kuwa Serikali imedhamiria kupambana na raia wake kwa njia hii.

Soma:
Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

Then, Sehemu ya II: Jamhuri vs JamiiForums kuhusu Oilcom na Uchakachuaji mafuta/Ukwepaji Kodi bandarini Dar

Na eti kwakuwa waliona inaelekea kubaya, inafanyiwa marekebisho (tayari shahidi amesikilizwa), Kesi namba 456: Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji mafuta bandarini kufanyiwa marekebisho tena!

Kisha, nikasoma kesi namba 457: Kampuni hii nakumbuka wakati wa sakata la bandarini na ukwepaji kodi ilikuwa kwenye orodha ya TPA, sijui imekuwaje Serikali inataka kuwakamata wananchi waliokuwa wakitoa ushirikiano.

Soma ‪Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai Polisi hawana utaalamu wa kulazimisha kuingilia mawasiliano kimtandao‬

Na pia ipo kesi ya JamiiForums kutosajiliwa .tz. Shahidi wa Jamhuri ambaye ndiye msajili wa kikoa cha dot-tz alikiri JamiiForums kuwa na domain mbili jamiiforums.co.tz na jf.co.tz na akasema zimesajiliwa zamani hata kabla ya kukamatwa kwa Maxence Melo. Sijui watabadilisha mashtaka?

Soma: Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums yaanza kuunguruma Kisutu na Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums imeendelea

Najiuliza, kama hiki ndicho kilichompeleka jela mwanzilishi wa mtandao wa JamiiForums, tuna serikali inayojali watu wake?
 
Asante kwa mtazamo ... wenye akili wafikirie ... sio kumwaga mapovu kishabiki tu ... soma then tafakiri halafu tiririka ...

Maelezo yamenyoooka kabisa ...
kwa mwenye busara zake anaona ukweli halisi ...

Sio mtu unabwatuka tu bila kuelewa na kutafakari kilocho ongewa ili mradi tu ubishe kishabiki

Na kwa hoja kama hizi wakija hapa kubwatu na kuropoka ... utaona haizidi sentensi Moja kajitahidi saaana sentensi mbili tena na tusi juuu ...
 
Mimi pia ni mmoja wapo kati ya watu wasioelewa dhamira za mkuu wa nchi, juzi kati bunge limeunda kamati ripoti ikapelekwa bungeni, wakasema hakuna kuijadili, maana watapoteza muda kwavile wanataka kupeleka mambo fasta. Kesho yake akakabidhiwa ripoti ya kamati, tena akasema taarifa huwa analetewa na vijana wake + video alikuwa nayo.

Siku hiyo hiyo akatoa agizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama wafanye kazi zao mara moja, tena atashangaa kama mpaka jion watakuwa hawajakamatwa. Watuhumiwa wakakamatwa, lakini juzi akiwa ameenda kufungua barabara ya Merarani - Kilimanjaro International Airport, alitoa amri kuwa waachiwe ili waende kusaidia kusaini mikataba na serikali. Watuhumiwa mpaka sasa wapo mitaani, kesi haijaenda mahakamani mpaka dakika hii.
Kinachoongelewa kwa sasa ni habari ya ukuta tu, tusubirie kuona updates za JKT kuhusu ukuta

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom