Kesi ya Yanga vs Morisson kusikilizwa

Yanga hawakubaliani na hio kauli ya TFF ndo maana wakaenda kushtaki FIFA na CAS.... Yanga wanasema bado walikuwa na mkataba na Morisson....
Yanga akishinda, Simba watakuwa na kosa la kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa na mkataba na timu nyingine
Morison akishindwa simba anapokwa point, Morison akishinda yanga anapokwa nini? Na Tff wanapokwa nini?
 
Kwahiyo Yanga ni wajinga wale mpaka kupoteza muda na hii kesi ? Amini nakwambia,, Kuna jambo hapa

Kwanini asaini mkataba wa Simba ilhali bado ana mkataba na Yanga ?

Hawana budi, lazima wafate maagizo.... CAS ni kubwa kuliko TFF
Kumuelewesha UTOPOLO ni kazi kubwa sana.
 
Na ndio maana Tp mazembe baada ya kuona As vita wamechezesha mchezaji ambaye bado alikuwa na mkataba timu aliyotoka, moja moja walipeleka kesi yao kule CAS, na mwisho wa siku As vita kupokwa point za mechi alizocheza yule mchezaji na kuchukuliwa Ubingwa wao kabisa
Kumbe na chama cha mpira drc kilisema saini ilighushiwa? au mchezaji lalamikiwa alikuwa huru? au na wao walisema mkataba wa mchezaji unamapungufu hivyo yupo huru?
 
Hivi hamsomi?case imeandikwa Yanga vs Morisson sasa simba anahusishwaje.
Ni kweli kabisa case ni Yanga vs Morrison. Kwenye hii case Yanga akishinda huenda akafungua kesi nyingine dhidi ya Simba kwa kumchezesha mchezaji aliyekuwa na mkataba na Yanga ama dhidi ya TFF kwa kuruhusu mchezaji mwenye mkataba na Yanga akaichezee Simba
 
We jamaa jipe moyo tu,nani alisema morison yuko huru,walichosema kuna karatasi haijasainiwa,sasa hiyo paper isiyosainiwa ndio ivunje mkataba,kwa taarifa yako Yanga wana hadi receipt salary ya mshahara aliyochukua morison kupitia mkataba ule alioukataa,na kama utakumbuka morison mwenyewe wakati yuko Yanga alitoa clip kama simba wanamrubuni na wamempa dola 5000 kama zawadi, lakini yeye bado ana mkataba Yanga,from nowhere baadae akaukataa ule mkataba,Yanga ilionewa na shinikizo lilitoka hadi kwa washabiki wa mikia walioko serikalini akiwemo bashite na wengineo kibao walimuhakikishia wao ndio kila kitu nchi hii iwe isiwe atachezea mikia,ile clip morison aliongea kiingereza fasaha na ile clip ipo cas,kitendo tu cha kuongea na mchezaji wa timu nyingine akiwa ndani ya mkataba ni kosa,nyie jiandaeni tu
Mkuu umejuaje clip ipo CAS?. Ila ile clip ingefika kule ingetusaidia sana!
 
stumainchassi @abdulsportstz

Huyu mdau ameandika;

UFAFANUZI KUHUSU KESI YA MORRISON VS YANGA..

Wapenzi wa Soka wako kwenye maswali magumu juu ya kesi ya YANGA dhidi ya Benard Morrison ... Yanga walifungua kesi hii kwa madhumu Makubwa ya kutaka kubaini uhalali wa contract Extension baina yake na Mchezaji Benard Morrison ... Kwanini Yanga walienda CAS ,Walienda kutafuta suluhu baada ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji chini ya T.F.F ambapo kamati ilimuacha Benard Morrison kuwa huru kwa kigezo Cha Mapungufu ya kimkataba Ambayo yalijitokeza .. Yanga hawakuridhika na maamuzi y kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji kwa kigezo cha kuhoji kuwa Mamlaka y kamati ilikuwa Ni kutanabaisha Kama mkataba ulikuwepo au haukuwepo ... Kamati ili kili wazi kuwa mchezaji Benard Morrison Raia wa Ghana alikuwa na mkataba na Yanga ambapo Hadi thamani ya mkataba ilikuwa imetajwa kuwa Ni dollar 25000 ambapo kamati ilimuamuru Benard kuridhisha fedha hizo kwa Yanga.. Katika msingi huo ndipo Yanga waliona kuwa wanayo Haki ya kusonga mbele kudai Haki ya mchezaji huo .... ENDAPO YANGA WAKISHINDA KESI NINI KITATOKEA....??? Mpira duniani kote unaongozwa na Sheria pamoja na Kanuni ambazo mashirikisho na vilabu na wachezaji wote wanapaswa kufuata ...miongoni mwa Kanuni hizo ni zile zinazo husu maswala ya Usajili..Timu hairuhusiwi kumsajili mchezaji wa timu nyingine angali akiwa na mkataba ikitaka kufanya hivyo italazimika kufanya yafuatayo .. (1)Kuitaarifu klabu Ambayo Ina mmiliki mchezaji huyo na kukubariana juu ya Uhamisho wa mchezaji huyo yaani Transfer ya mchezaji . (2)Timu inayo muhitaji ilazimika kulipa kiasi Cha fedha ambacho timu inayo mmiliki imekitaja au kilichopo katika mkataba wa mchezaji husika ... Kufanya kinyume na hayo Sheria huchukua mkondo wake ikiwa Ni pamoja na Timu iliyovunja utaratibu huo kufungiwa kufanya Usajili ...Pili kupokwa points zote ambazo mchezaji husika alishiriki .... Kwenye Issue ya Morrison ikitokea Yanga kazhinda Basi itafunguliwa kesi nyingine ya msingi dhidi ya Klabu na Shirikisho lilo idhinisha Usajili wa mchezaji Benard Morrison hapo ndipo itaweza kuyaona madhara ya sakata hili ...
 
Vipi kesi ikipinduka: Morrison mechi za awali wakati anatua Yanga hakua na mkataba itakuaje?

Maana Hanspop aliwahi kuligusia hilo kua Morisson kwenye usajili wa dirisha dogo alichelewa kusajiliwa na alicheza mechi ya kwanza dhidi ya Singida bila mkataba
Hanspope ni Nani?! Ni Tff?
 
H
Yanga vs morison,ikithibitika morison mchezaji wa Yanga ni kwamba morison ni mchezajibwa Yanga aliekua anacheza simba kimakosa,automatically simba ilikua inamtumia mchezaji asie wa kwao
Hivi katika mgogoro huu huyo Morrison ameichea Simba mechi ngapi za ligi? Kama ni mechi 15 kwa mfano na Kati ya hizo Simba ameshinda 10 in maana Simba atanyang'anywa point 30? Kama ni hivyo madhara yake katika msimamo wa ligi ni yapi?
 
Mkuu acha ushabiki zungumzia uhalisia, hukumu haikusema Morrison yupo free ilitoka kwamba ana mkataba wenye mapungufu, angekua huru hata CAS wasinge hangaika na kesi ya kijinga hivyo kumbuka mpka case ipangwe kusiliza hua wana jilidhisha kama kuna hoja za msingi

Hakuna kesi ya kijinga hata siku moja,lakini ujinga wa hiyo kesi utaonekana tu pale Yanga watakaposhindwa.Ni kipi haswa kinawafanya mshupalie Simba kupokwa point? Yani Simba achezeshe mchezaji kwa vibali vyote tena halali,Mchezaji huyo huyo acheze hadi CL na CAF wakaridhia,leo uje usubirie Simba kupokwa Point kwa kesi ya Morrison kushindwa (kitu ambacho hakiwezekani).

Yanga jitahidini walau leo mfiche aibu yenu ya kukosa ubingwa mara nne mfululizo.Habari za kusubiri ushindi wa mezani hazipo.Nyie ni Wanaume pambaneni uwanjani mshinde.
 
Atapokonywa na nani?
Simba anahusika vipi kwenye kesi yenu?
TFF walithibitisha kuwa morrison yupo huru, na usajili wake ulikuwa halali sababu TFF walithibitisha kwamba yupo huru.
Hujui kuwa sheria hizo zinawalinda wachezaji kuendelea kucheza vilabu wavitakavyo wakati kesi zao zikiendelea?
Yanga hatoambulia chochote
Akili zenu na TFF hizi subir mana mkisema mwanzo hakuna kesi hapa
 
Yanga hawakubaliani na hio kauli ya TFF ndo maana wakaenda kushtaki FIFA na CAS.... Yanga wanasema bado walikuwa na mkataba na Morisson....
Yanga akishinda, Simba watakuwa na kosa la kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa na mkataba na timu nyingine
Kama ndio hivyo ilitakiwa Simba wasubiri mpaka kesi ya CAS iishe ndio waanze kumchezesha Morison.
 
Swali kwa wadau hivi kipindi anacheza Champions League inamaana wao CAF huwa hawafatilii issue za mikataba ya wachezaji? Je wao hawakuona kama bado ni mchezaji wa yanga au simba?
 
Na mapungufu ya mkataba sio jambo linaloweza kufanya mkataba usiwe halali, kwa mapungufu yaliyo kuwepo mkataba ulikuwa halali kabisa, na TFF wakasahau kwamba Yanga wanaweza kwenda kwenye mamlaka ya juu zaidi
Mkuu naweza kukubaliana na wewe. Unajua sisi Watanzania tuna tatizo la weledi.
 
Back
Top Bottom