Kesi ya wizi wa wanyama hai: Mashahidi waeleza namna Twiga hai walivyotoroshewa nje

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Mashahidi wawili wa upande wa mashtaka, wameieleza mahakama namna wanyamahai, wakiwamo twiga wanne, walivyosafirishwa kwenda Doha nchini Qatar kwa kutumia ndege ya jeshi.

Mashahidi hao, akiwamo mmoja wa madereva wa lori, walitoa ushahidi wao juzi wakiongozwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Evetha Mushi, Pius Hilla na Stella Majaliwa.

Shahidi wa sita, Davis Kimei aliyekuwa dereva wa lori aina ya Mitsubish Fusso, alieleza namna alivyosafirisha wanyama hao toka Arusha hadi Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia).

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo shahidi huyo alidai Novemba 25, 2010 alikodishwa kubeba wanyama hao na watu watatu, wakiwemo wawili wenye asili ya kiasia hadi uwanja wa Kia kwa ujira wa Sh150,000.

“Baada ya kuelewana tulikwenda hadi kwenye nyumba moja eneo la Kwamrefu, Arusha na humo ndani nilikuta vijana wengi ambao walikuwa wakitengeneza mabox yaliyokuwa na Twiga na Swala,” alisema.

Shahidi huyo alidai baada ya kuwapakia wanyama hao, msafara wa malori manne ulielekea Kia na kufika saa 8:00 usiku na kuelekea moja kwa moja uwanjani ambapo walikuta ndege kubwa ya jeshi imeegeshwa.

“Maboksi yale yalishushwa na kupakiwa katika ndege hiyo usiku ule wa manane,” alisema.

Shahidi wa saba, alidai siku ya tukio saa 4:00 usiku aliwasikia wafanyakazi wawili uwanjani hapo, wakisema kuna wanyama wangesafirishwa usiku huo.

“Nilimdokeza mkuu wa upelelezi… Nilipokuwa nyumbani bosi wangu alinipigia simu na kuniambia ile taarifa niliyompa ilikuwa ni ya kweli kuna ndege ya Serikali inasafirisha wanyamapori,” alisema.

Shahidi huyo alidai kuwa saa 6:00 usiku alirudi kazini na ilipofika saa 8:30 usiku lilikuja basi aina ya Toyota Coaster ambapo walishuka watu wenye sare za jeshi wenye asili ya kiarabu.

Washtakiwa katika kesi hiyo inayovuta hisia za Watanzania wengi ni Kamran Ahmed, Hawa Mang’unyuka, Michael Mrutu na Patrick Paul na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Agosti 13 na 14.

Kwa hisani ya Mwananchi.

Baadhi ya picha za Doha zoo nchini Qatar.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    67.5 KB · Views: 2,695
  • image.jpg
    image.jpg
    48.1 KB · Views: 2,456
  • image.jpg
    image.jpg
    12.4 KB · Views: 2,232
Ni kweli Uzalendo kwa sasa ni historia nchini?.

Wakati wa Utawala wa Mwl. Nyerere karibia kila mwananchi mwema alikuwa ni mpelelezi na mlinzi katika jamii. Tuliona wananchi wakianzisha vikundi vya ulinzi kama sungusungu iliyoanzishwa miaka ya 1980 ili kukabiliana na watenda maovu kwa sababu taasisi kama polisi ilikuwa na manpower na vitendea kazi vichache, wananchi walikuwa kama ndugu katika kukabiliana na maovu bila kujali wasifu, rangi ya mtu na imani ya dini yake.

Kwa sasa hakuna tena hamasa kama hii kutoka kwa wananchi wema. Watu kwa sasa wako tayari kufumbia macho maovu au kusaidia watu kutenda maovu ( accessory to a crime ) kama tunavyoona katika kesi hii ya kushangaza na ya aina ya pekee kutokea kwenye nchi ambayo ni Sovereign state.

Kuna maswali ya msingi kabisa yanahitaji soul searching kufahamu kilikoni nchini kwa sasa.

Is this happening because of negative perceptions of the national security institutions as corrupt, unprofessional, predatory and ineffective or watanzania hawana tena uzalendo.

Something, somewhere is wrong nowdays in Tanzania.
 
Kinana anahusika moja kwa moja hapa, na nashangaa bado tu anapeta mitaani huku akivaa magamba yake.
 
Na hao twiga wasahau labda waarabu wote wafe Ukimwi.Kuliko wawarudishe watawaua.km wanaweza hata wapiga denda ngamia, basi twiga watalala nao kabisa.Waarabu si wajerumani waliorudisha mjusi na faru na wanyama wengine waliokwend anao kwao.Km hawajawahi mba msamaha africa kwa kuwatumikisha,itakuwa kuwarudisha hao wanyama?

Mtawafuga wenzetu bure ambao pengine walionyeshwa documents...Akina JK wakishavalishwa kanzu ila chu.pi ndio mambao yao haya.Watu wa pwani watajulia wapi wanyama km hata migomba kuotesha hawajui.

mankissingcamel.img_assist_custom-600x425.jpg
 
Kweli Mwinyi atajuta san akam anayo sense ya fahamu hata kidogo ktk akili yake.....Jk ndio itabidi ajinyonge hata akiwa ahera....
 
Na hao twiga wasahau labda waarabu wote wafe Ukimwi.Kuliko wawarudishe watawaua.km wanaweza hata wapiga denda ngamia, basi twiga watalala nao kabisa.Waarabu si wajerumani waliorudisha mjusi na faru na wanyama wengine waliokwend anao kwao.Km hawajawahi mba msamaha africa kwa kuwatumikisha,itakuwa kuwarudisha hao wanyama?

Mtawafuga wenzetu bure ambao pengine walionyeshwa documents...Akina JK wakishavalishwa kanzu ila chu.pi ndio mambao yao haya.Watu wa pwani watajulia wapi wanyama km hata migomba kuotesha hawajui.
You can be radical to same extent.

Mawazo yako yanavuka mipaka mpaka inakuwa ni vigumu kutofautisha na ubaguzi wa dini na kabila. I'm sorry kama sivyo.
 
ilianzia kwa Mwinyi, akauza hadi Kasuku wa Ikuru, JK amefungakazi, eti tunausarama wataifa, tunamakanjanja wa taifa, kama walikabizi Ikuru ikamilikiwa na OBAMA, wakati JK hawezi kupewa hata ofisi ya kitongoji cha USA hapo unategemea nini?
 
Tulikofika ni mbali sijui hata nani atairudisha ile tz ya zamani . Hii mpya haina uimara kabisaa.
 
Sasa wanawato akafara watz, tena kwa kufuru yao waliwategea na kuwashikwa kwa mbwembwe wale wasio vaa kanzu bila chupi...Kwani kupitia Un na kuwaambia Qatar warudishe hao wanyama na kuwanyang`anya Loliondo ni shida?Si wamevunja mkataba.Ten aitaokoa taifa letu.JK atacheza drama kwa vile haruhusiwi shtaki muumin mwenzie....

Hii ni laana ya nchi,ndio maana tutachapwa, ndio maana wanachoma makanisa.
 
.View attachment 103307

Desert queen.....waarabu wana mashindano ya urembo kwa ngamia wa kike..thread yangu mods waliitoa kabisa.Sijui kwanini wakati CCN siku hizi ni highlight.

Sasa km linyama libaya hivyo wanalipiga denda.Itakuweje Kwa twiga,,si wanalala nao kabisa hawa binadamu waliopiga mgongo civilizations.
 
ilianzia kwa Mwinyi, akauza hadi Kasuku wa Ikuru, JK amefungakazi, eti tunausarama wataifa, tunamakanjanja wa taifa,
Sina budi kukubaliana na wewe. Huwezi ukawa na usalama wa nchi ambao haujui sababu ya ndege ya kivita kuwepo nchini. Hii ni kashfa ambayo watu waliopewa jukumu la kukiongoza kitengo cha usalama wa taifa walitakiwa wawajibike bila hata kuambiwa kufanya hivyo. It's a disgrace.

kama walikabizi Ikuru ikamilikiwa na OBAMA, wakati JK hawezi kupewa hata ofisi ya kitongoji cha USA hapo unategemea nini?
Swala la ulinzi wa Obama halina mjadala.

Rais Obama hata anapotembelea UK ulinzi huwa ni kama huo uliokuwa wakati akiwa Tanzania. Huwa kuna misuguano na watu wa ulinzi UK kwa vile huwa wanaona wanakuwa undermined na walinzi wa Obama.

Kwa hiyo siyo jambo la ajabu kama walinzi wake walichukua ulinzi wa ikulu kuwa chini yao ikichukuliwa kuwa ulinzi wetu hata haufikii ulinzi wa UK ambalo huwa unakuwa hauaminiwi na walinzi wa Obama.
 
.View attachment 103307

Desert queen.....waarabu wana mashindano ya urembo kwa ngamia wa kike..thread yangu mods waliitoa kabisa.Sijui kwanini wakati CCN siku hizi ni highlight.

Sasa km linyama libaya hivyo wanalipiga denda.Itakuweje Kwa twiga,,si wanalala nao kabisa hawa binadamu waliopiga mgongo civilizations.
kila jamii ina mila na desturi zao pamoja na kwamba kwa jamii nyingine inaweza ikaonekana ni makosa.

Hiyo haina tofauti na wazungu wanaobusu mbwa,
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    24.2 KB · Views: 463
  • image.jpg
    image.jpg
    159.7 KB · Views: 424
Inasikitisha inatia huruma,kwa jinsi maelezo tu yalivyo kama ndege ya jeshi na wanajeshi wa Qatar walihusika basi kahusika kigogo mkubwa sana jeshini -wanajeshi kikawaida hawaruhusiwa kuingia nchi ya watu tena na ndege la kijeshi bila Supreme order ndo inavyojulikana,na kama ni hvyo basi hyo kesi itakuwa ni zuga tu na hao walioshtakiwa ni chambo tu ipo siku watakuja achiliwa huru

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
sina budi kukubaliana na wewe. Huwezi ukawa na usalama wa nchi ambao haujui sababu ya ndege ya kivita kuwepo nchini. Hii ni kashfa ambayo watu waliopewa jukumu la kukiongoza kitengo cha usalama wa taifa walitakiwa wawajibike bila hata kuambiwa kufanya hivyo. It's a disgrace.


Swala la ulinzi wa obama halina mjadala.

Rais obama hata anapotembelea uk ulinzi huwa ni kama huo uliokuwa wakati akiwa tanzania. Huwa kuna misuguano na watu wa ulinzi uk kwa vile huwa wanaona wanakuwa undermined na walinzi wa obama.

Kwa hiyo siyo jambo la ajabu kama walinzi wake walichukua ulinzi wa ikulu kuwa chini yao ikichukuliwa kuwa ulinzi wetu hata haufikii ulinzi wa uk ambalo huwa unakuwa hauaminiwi na walinzi wa obama.

nyerere aliwah mkatalia kiongoz mmoja wa usa kisa hicho, huwez kabidh ikulu kwa fbi na cia ni upumbavu, mara 100 tungeshirikiana na wawekezaji wengine kuzitumia rasirimal kwa maendeleo ya watz
 
kila jamii ina mila na desturi zao pamoja na kwamba kwa jamii nyingine inaweza ikaonekana ni makosa.

Hiyo haina tofauti na wazungu wanaobusu mbwa,

na waswahili tunaokashifu au kuabudu chochote anachofanya mzungu au mwarabu!
Hivi ni lazima uchague side either mwarabu au mzungu? Huwezi kuwa huru hapo katikati?
Tanzania tuna mikataba mibovu mingi sana. Mingine ya wazungu, waarabu wachina, waafrika watanzania waislamu wakristu. Tatizo sio hao na huko watokako tatizo ni SISI.
 
Twiga wetu wanalishwa tende, daaah! Hivi hiyo ndege imewezaje kutua KIA na hadi kuondoka na wanyama bila serikali kujua! Kuna mambo mengine huitaji hata kuwa Genius.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mbua itawashukia tu madamu walishapatikana na jk hatetei waharifu ngoja waone moto wake.
 
Hii ni zuga tu. Kila kitu kilipangwa na kuratibiwa vizuri kabisa chini ya usimamizi wa JWTZ, TISS, Jeshi la Polisi, Maafisa uhamiaji, TANAPA, Ikulu ya Magogoni, KIA, Askari wanyama pori, Wizara husika, Baraza la mawaziri na rais Kikwete mwenyewe.

Kama kuna mtu anabisha juu ya hili, embu ajiulize swali hili: Kwanini Serikali ya Tanzania mpaka sasa haija-react vikali dhidi ya nchi ya Quatar ikiwemo kushinikiza wanyama hao kurudishwa nchini haraka iwezekanavyo, kushtaki kimataifa, kuvunja uhusiano wa kibalozi, Kudai fidia na kuombwa radhi nk.?
 
Back
Top Bottom