Kesi ya Wabunge 19 wasio na chama dhidi ya CHADEMA inaendelea Mahakamani, Leo ni zamu ya Cecilia Pareso

..juzi Mnyika kasema Tunduma peke yake kulikuwa na wanachama 80 wamebambikiwa kesi.

..nilitegemea watu hao habari zao zisambae ktk vyombo vyote vya habari ikiwemo hapa J
Opportunity missed.

Sijui kama wanalielewa hilo.
Kuna kitu kimewapata CHADEMA, hawapo makini tena kama walivyowahi kuwa makini wakati hali yao ikiwa ngumu zaidi.
 
..makada wa Chadema wanapeana updates wenyewe badala ya kuuhabarisha umma.

..wakiacha hii kesi iendelee kwa kificho bila umma kujua uozo uliofanyika wanatoa nafasi kwa Jaji na System kuwakandamiza.

Cc Erythrocyte
Kwani ile ya Mbowe na makomandoo, iliyokua na updates za kutosha, Jaji na System waliifanyaje ile kesi. This is Tz mkuu.
 
Ndio maana nimesema kwenye hili wako ovyo sana. Wangetumia robo ya juhudi walizofanya kutujuza kuhusu kesi ya Mwenyekiti wao kwenye mambo mengine wangekuwa mbali. Si hii kesi peke yake. Wana kesi kibao zinazohusu wanachama wao lakini taarifa zinapatikana kwenye twitter binafsi za wanachama wao au kwa Maria! Twitter page yao imelala. Wanashangaza sana.

Amandla...
Vipi ile ya Mbowe, updates zilisaidia nini?
 
Usisubirie, ingia fb kwenye account ya Twaha Mwaipaya. Mtu ana omba poo kwa maswali ya Kibatala
mkuu hebu weka link hapa tupate kupitia kinachojiri mana naona kama watoa taarifa wengi wa kujitolea ni kama wameipotezea.. hii si sawa
 
mkuu hivi hata kukopi hivi nayo ni shida jamani!!! mnatuangusha sana




WAKILI PETER KIBATALA AKIMUHOJI JESCA KISHOA MAHAKAMANI.
SEHEMU YA 4.
Kibatala: nisomee minutes kuanzia hapa 9- 14
Jaji: Mr Kibatala asome yote uwezi kuwa namna nyingine maana ndefu sana
Kibatala: ok Mh jaji nitaona namna ya kufanya
Kibatala: ni kweli kwenye Barua ya November 25 ya katibu mkuu aliweka Anwani yake E-Mail yake namba ya simu na fax
Shahidi: namba ya simu hainonakani vizuri
Kibatala: ila E-Mail IPO
Shahidi: ndio IPO
Kibatala: licha ya kuweka E-Mail ila Wewe ukaona ujibu kwa WHATSSAP?
Shahidi: Mh jaji ilikuwa haraka
Kibatala: role aliyotumia Mnyika iliseme nani atakaa kwenye kikao Cha kamati KUU
Shahidi: mimi sio mjumbe wa kamati kuu ila walikuwepo yeye na Mkt
Kibatala: kwenye minutes Katibu mkuu alitumia Lugha Gani?
Shahidi: katika kitu natamani ni ile video ichezwe
Jaji: Mh Shahidi utajibu ulichombiwa
Wakili Panya:
Mh jaji Shahidi ameshasema anataka video ichezwe
Kibatala:
Tukiplay video tutaona sehemu Katibu mkuu akiplay role za kamati KUU kwamba mh Mbowe atakuwepo?
Shahidi: mh jaji kwenye video imeelezwa Mnyika akisema hayo.. video ichezwe tatizo nini!?
Sasa video inawekwa...
Tutaendelea baada ya video kuisha.
1667998464558.png

WAKILI PETER KIBATALA AKIMUHOJI JESCA KISHOA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 3.
Kibatala; kwa hiyo ufahamu TEHAMA ni nini?
Shahidi: Kwa kweli mh jaji Sifahamu TEHAMA ni nini
Kibatala: Kwa mujibu ya Katiba ya CHADEMA ibara
6.3.7 (a) unafahamu TEHAMA
Shahidi: naomba nisome
Shahidi anasoma
Shahidi; nakuomba soma na hii D
Kibatala: ufahamu kilichoandikwa hapo?
Shahidi: nafahamu Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA
Kibatala: 6.3.7 inasemaje haitambui matumizi ya TEHAMA?
Shahidi anasoma hiyo ibara... Ila Mh jaji mwogozo unatolewa na Baraza kuu
Na mimi nilishukuwa kiongozi wa chama muda mrefu
Kibatala: huo muongozo tutaona wapi?
Shahidi: chama kinaongozwa Kwa mujibu wa Katiba
Kibatala: soma kichwa Cha habari Uk. 86
Shahidi: Mh jaji taito anayotaka nisome inasema muongozo wa matumizi teknonojia habari na Tehema
Kibatala: ambayo inasemaje
Shahidi: inasema CHADEMA DIGITAL
Kibatala: ibara 6.3.7 (d) ni ibara tofauti?
Shahidi: mh jaji ananiwekea mdomoni
Kibatala: unasema Hiyo Ibara 6.3.7.d
Shahidi: Mh jaji mimi sio mwanasheria
Kibatala: msingi wa Kesi yenu kuwa hamkupewa nafasi ya kusikilizwa
Shahidi: kweli niliomba muda walau week moja kutokana na mazingira yaliyokuwepo kutokana na press conference ya Katibu mkuu na vurugu zilizokuwepo na presha ilyokuwepo maana nilinza kuhukumiwa na katibu mkuu Kwa maneno makali hivyo Mh jaji naomba video ichezwe hapa
Kibatala: Ile Barua ya November 25 ilikuwa na tatizo Gani?
Shahidi: ilikuwa haina hati ya mashtaka na ilitumwa kwa njia ya Whatsapp ambayo sio mawasiliano rasmi ya chama
Kibatala: mwogozo upi kwenye Katiba unakataza Whatssap?
Shahidi: Kwa mujibu wa alichokuwa ananionyesha ni Tehema sio whatssap
Kibatala: niambie kwenye Katiba mwongozo upi unakataza
Shahidi: mh jaji narudia Whatssap haijakuwa njia rasmi ya mawasiliano ya chama
Kibatala: Ukupewa sababu ya kusikilizwa kwa nini?
Shahidi: Mh jaji Barua naikumbatanisha hati ya mashtaka
Ila badae walikuja kuweka minutes za Baraza kuu
Kibatala anamsomea kiapo chake..
Kibatala: haya sio mashtaka?
Shahidi: mh jaji haya sio mshtaka
Mahakama kicheko
😀
😀

Kibatala anampa Katiba ya chama
Shahidi: Mh jaji hayo anayasoma nikitaka kwa kufafanua nitachukua siki 3
Kibatala: Barua ya November 25 ya katibu mkuu ulijibu kwa njia Gani?
Shahidi: njia aliyotumia yeye
Kibatala: ya Whatsapp?
Shahidi: njia hiyo Hiyo
Kibatala: njia ulitumia uliamini kuwa angeiapata kwa haraka
Shahidi: inategemea na yeye mwenyewe yupo katika hali gani maana illikuwa Kwa njia Whatssap
Kibatala: Title ya hicho taru 5 inasemaje?
Shahidi anasoma kuwa inahusu hati ya mashtaka
Kibatala: taru 5 inasema hati ya mashtaka ambayo uliyakaaa
Shahidi: Mh ndio
Kibatala: nashukuru wewe umeitambua
Kibatala: hiyo taru 5 uliyotambua unajua kuwa ndio Kuna taarifa za wito wa katibu mkuu kukuita
Shahidi: Mh jaji nilishasema
Kibatala: unafahamu kuwa minutes hizo za kamati KUU zilikuwa zinasema kuwa kamati KUU inaweza kuendelea bila wewe?
Shahidi: Mh jaji samahani mimi sio mwanasheria
Kibatala: kwenye hizo minutes za taru 5 kamati KUU
Zinasema Mnyika ndio akimkaribisha Mkurengezi wa sheria Walter Mndeme asome
Shahidi: Mh jaji mimi sio mjumbe wa kamati KUU
Inaendelea
Kesi ya Halima Mdee vs CHADEMA inaendelea leo Jumatano
November 9,2022 hapa mahakama kuu jijini Dar es Salaam
Mbele ya Jaji
Cyprian Mkeha.
Jaji anaingia Mahakamani muda huu saa 7: 50 mchana huu
Watu wote hapa Mahakamani tunasimama kama kawaida
Karani wa mahakama:
Kesi namba 36/2022
Halima James Mdee na wenzake kumi na nane dhidi ya CHADEMA...
Mh Jaji:
Karibuni
Anasimama Wakili wa Serikali:
Mh Jaji naitwa
Tausi Mlonzo
Leonia Maneno
Namwakilisha mjibu maombi wa pili nawa watatu
Na upande wa Waleta maombi namba wanawakilishwa na
Mawakili wasomi
Ipilinga Panya
Emanuel Ukashu
Aiko Mwamanenge
Edsono Kilatu
Na upande wa Wajibu maombi wa Kwanza anawakilishwa na Wakili Msomi
Peter Kibatala
Hadija Aron
Nashon Nkungu
Diskon Matata
Maombi haya yamekuja Kwa ajili Cross examination mleta maombi wa 12 Jesca Kishoa Kwa upande wa pili na tatu tupo tayari kuendelea
Shahidi Jesca Kishoa anaenda Kizimbani
Jaji: Jina lako?
Shahidi: Naitwa Jesca Kishoa
Jaji: Umri wako?
Shahidi: Nina miaka 33
Jaji: Dini yako?
Shahidi: Mkristo
Jaji shahidi utaapishwa
Jaji:Mh utachagua kukaaa au kusimama..
Mniwie radhi Kwa kuchelewa kuanza
Jaji: Mr Kibatala unaweza kuendelea
Kibatala: Katika hati yako ya kiapo unasema wewe ni mwanachama wa CHADEMA?
Shahidi:
Mimi ni mwanachama wa CHADEMA
Jaji: ni sahihi
Shahidi: ni sawa mimi ni mwanachama wa CHADEMA
Kibatala: unafahamu kuwa katiba hii inaitambua na mahakama inatambua katiba hii jinsi ilivyo?
Shahidi; nimefungua Kesi kwa mujibu wa kiapo chako
Kibatala: Ulipewa taarifa za wito wa kikao lini?
Shahidi: November 25,2020
Kibatala: Uliambiwa pia tuhuma kwenye wito huo?
Shahidi: Barua niloyotumiwa na Katibu mkuu ilikuwa na tuhumu ya kuwa mimi nilijiapisha mwenyewe
Inaendelea
ILIKUA HIVI NDANI YA MAHAKAMA.
Saa 4 na Dk 10
Anakuja Askari Na Kutangaza Kua Oda Ya Jaji kwamba
1 .Watu Waliosimama Watoke Nnje,
2.Kwamba Kusiandikwe Chochote Kinachoendelea Mahakamani
3.Wanachama Wa Chadema Wawapishe Wabunge Walioishitaki Chadema Kukaa Kwenye Viti.
Mwisho Wa Oda, Wakatoa Amri Watu Waanze Kutoka
Wanachama Wa Chadema Wakagomea Oda Na Kutaka Kauli Hizo Aje Jaji Azitoe Mwenyewe
Ikatokea Taharuki Kati Ya Wanachama Wa Chadema Na Police,
Ndipo Ikabidi Wakili Wa Chadema , Wakili Wa Serikali Na Wakili Wa Washtaki Waende Kwa Jaji Kwaajili Ya Mjadala.
Baada Ya Mjadala Wa Dk 15 hivi
Majibu Yaliyotolewa Ni Haya.
Mahakama Imeona Ni Busara Tubreak Kwa Muda Kadhaaa Ili Kesi Iamishwe Kwenda Ukumbi Mwingine Wenye Nafasi.
Mahakama Imeahirishwa Mpaka Baada Ya Muda .
Tukutane Baadae.
 
Sheria huwa tamu sana. Kwa maendeleo ya chama ni vyema wangefunika kombe mwana kharam akapita.
 
Kesi iliyofunguliwa na Wabunge Mamluki , Wasaliti walionunuliwa , dhidi ya CHADEMA inaendelea Mahakamani , Ambapo leo ni zamu ya Msaliti wa Karatu Cecilia Pareso.

Kama kawaida Wakili Msomi Peter Kibatala Anaendelea kumsulubu huyu mama kwa kumtandika maswali magumu bila huruma yoyote , Mama wa watu anaonekana kutetemeka.

Ngoja tuendelee kusubiri.
Mahojiano kamili yapo wapi?
 
Back
Top Bottom