Kero: Vodacom, kabla ya tarehe 26 mwezi huu, nitakuwa nimeivunja line yenu

Galadudu

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
2,305
772
Sina neno la kuita zaidi ya kusema huu 'wizi' sasa nimechoka nao, mara ya kwanza mlitaka kunipiga kimya sh 435,000/ nilizokuwa natupia kwny akaunti yangu ya benki kutokea simu ya mkononi line yenu ikihusika.

Baada ya kuifuatilia sana na vitisho vingi hatimae kwa aibu mkanirudishia. Mara ya pili kuna mtu alikosea namba kwny kutuma pesa ikaja kwangu sh 700,000/ nikatumia uungwana nikawapigia na mkanipa maelekezo ya kuituma kwenu, nikaituma, cha kushangaza ni yule aliyekosea kunipigia na kuomba nimrudishie, nikampa maelezo kwa kirefu kuwa nimeirudisha voda.

Huyo mdada aliendelea kunifuatilia kwa zaidi ya wiki hadi nikaamua kuacha shughuli zangu na kuja kwny ofisi zenu na huyo dada eti ndio mkamrudishia pesa yake, Mara ya tatu ni juzi nimeweka vocha ya sh elfu 5, na mtandao wa kujiunga na cheka ulikuwa unasumbua nikaachana nao nikatumia mtandao mwingine.

Sasa maajabu ya mwaka, tangu hiyo juzi cjatumia voda, hadi muda huu naandika hapa (najua mtasoma) imebaki sh 2900!

Sasa nimetoa hizo cku tisa ili mrekebishe hilo tatizo ikishindikana nitachukua maamuzi mazito ya kuipasua pasua line yenu kwa hasira kali, halafu pamoja na udogo wake naitia kiberiti, na familia yangu yote nitaipiga stop kubwa kutumia/kuonekana na line ya voda achilia mbali kuizungumzia, na kampeni hii nitaieneza kwa marafiki zangu wote waachane na hiyo kitu, sintoishia hapo, nitahamia kwa wenye maduka wa mtaani kwetu nako nitapeleka propaganda hizi, halafu mwisho cku muwe kama TTCL.

Naipenda sana Vodacom T Ltd ndio maana ckutaka kuchukua maamuzi magumu kwa haraka,basi jaribuni kurudisha mema kwenye huu upendo wangu kwenu.
 
Ni kweli voda wanaiba sana sasa hivi, sasa sielewi kama ni hawa wafanyakazi chini kwa chini au kampuni nzima inahusika kwa makusudi kabisa, kila siku watu wanawalalamikia sana, kiukweli wanaiba sana vocha, weka usiitumie halafu badae cheki utajuta.
 
Mzalendo Hata Mimi Nimeweka Vocha Ya Buku Mara 3 Zote Nakuta Wamekomba Yani Sijakopa Wala Sijajiunga Na Huduma Yoyote,nimepiga C.Care Voda Wananiambia Piga Baada Ya Nusu Saa Nikapiga Tena Wakaniambia Hivyohivyo Nimeenda Vodashop Wakasema Suala Langu Litashughulikiwa After 2hrs,Leo Ni Siku Ya 4 Kimya Hivi Nikipata Muda Nataka Niende Tena,huu Wizi Sasa Too Much Me Situmii Tena Line Yao Maisha Yenyewe Yakowapi Yakutiana Hasara Kila Cku?Nawauliza Nyie Voda Nyok*
 
Hayo yametokea kwa wengi tu.Muhimu tumia laini ya voda kwa kupokea tu ili usipoteze mawasliano na wale wenye kuijuwa namba ya voda.Nenda airtel haraka.Mimi ilinibidi ninunuwe simu ya laini mbili kwa sababu hizohizo.
 
sipati picha.. unafoka, mvua inanyesha.. mishipa kichwani imechomoza.. unatembea huku na kule.. hapo lazima line ivunjwe..!
 
Me hiyo siweki vocha imebaki ya kupokea na mara mojamoja m pesa tu.
 
Sina neno la kuita zaidi ya kusema huu 'wizi' sasa nimechoka nao, mara ya kwanza mlitaka kunipiga kimya sh 435,000/ nilizokuwa natupia kwny akaunti yangu ya benki kutokea simu ya mkononi line yenu ikihusika.

Baada ya kuifuatilia sana na vitisho vingi hatimae kwa aibu mkanirudishia. Mara ya pili kuna mtu alikosea namba kwny kutuma pesa ikaja kwangu sh 700,000/ nikatumia uungwana nikawapigia na mkanipa maelekezo ya kuituma kwenu, nikaituma, cha kushangaza ni yule aliyekosea kunipigia na kuomba nimrudishie, nikampa maelezo kwa kirefu kuwa nimeirudisha voda.

Huyo mdada aliendelea kunifuatilia kwa zaidi ya wiki hadi nikaamua kuacha shughuli zangu na kuja kwny ofisi zenu na huyo dada eti ndio mkamrudishia pesa yake, Mara ya tatu ni juzi nimeweka vocha ya sh elfu 5, na mtandao wa kujiunga na cheka ulikuwa unasumbua nikaachana nao nikatumia mtandao mwingine.

Sasa maajabu ya mwaka, tangu hiyo juzi cjatumia voda, hadi muda huu naandika hapa (najua mtasoma) imebaki sh 2900!

Sasa nimetoa hizo cku tisa ili mrekebishe hilo tatizo ikishindikana nitachukua maamuzi mazito ya kuipasua pasua line yenu kwa hasira kali, halafu pamoja na udogo wake naitia kiberiti, na familia yangu yote nitaipiga stop kubwa kutumia/kuonekana na line ya voda achilia mbali kuizungumzia, na kampeni hii nitaieneza kwa marafiki zangu wote waachane na hiyo kitu, sintoishia hapo, nitahamia kwa wenye maduka wa mtaani kwetu nako nitapeleka propaganda hizi, halafu mwisho cku muwe kama TTCL.

Naipenda sana Vodacom T Ltd ndio maana ckutaka kuchukua maamuzi magumu kwa haraka,basi jaribuni kurudisha mema kwenye huu upendo wangu kwenu.

Mkuu asante sana kwa kufunguka, mimi wiki 2 zilizopitz nilikosea kutuma fedha badala ya kwenda benk ya access ikaend convenant benk for woman, mara tu nikapiga huduma kwa wateja wakaniahidi kuwa fedha ingerudi ndani ya siku 7 za kazi lakini cha kushangaza toka ziishe hizo siku7 kila nikiwakumbusha wanaahidi kuwa fedha itarudi ndani ya masaa 24, sasa hata mimi nimechoka natarajia jumatatu kama hawatakua wamerejesha niwaburuze mahakamani Pamba*fu kabisa hawa.
 
Mi baada ya kuwatishia kuwaburuza mahakamani wakaniambia watairudisha baada ya masaa 48 nikawaambia sintoweza kusubiri kwa muda huo..... Na kweli baada ya masaa matatu hela ikarudi
 
Huna haja ya kulalamika , dawa ya hawa Voda ni kuungana na kuwahama kwa siku moja. Mbona madereva wakagoma kwa masaa machache tu serikali wakatii amri. Lini tunasitisha kutumia lini za Voda???
 
Kwakweli Voda ni wezi hawana mfano

niliacha Tsh 2,000 kwenye mpesa, baada ya wiki nimekuta Tsh 400 !
Kwa sasa natumia kwa kuangalia miss calls na kutuma pesa nimeamua kurudia utaratibu wa zamani wa kudeposit katika Bank Acc. ni bure na ni instantly.
 
Back
Top Bottom