mamabaraka
Member
- Oct 18, 2011
- 92
- 14
wana jf wenzangu nakerwa na tabia ya baadhi ya waajiri wanaopiga simu. Unakuta ni mishare ya saa nne na nusu asubuhi unapigiwa cm kama hii. Nanukuu "haloo naongea na flani?napiga simu kutoka ....... Njoo leo saa tano na nusu asubuhi ofisi kwetu kinondoni kwa ajiri ya usaili fika na vyeti original tafadhari" Hii taarifa ni nzuri lakini kwa nini usinipigie siku tatu au nne kabla. Inaudhi manake huu uzembe umenifanya nikose interview mbili na huwezi jua yawezeka ndo ilikuwa nafasi yangu ya kazi. Unapigiwa simu ya hivyo saa nyingine umesafiri hauko Dar, au upo Dar lakini vyeti umeacha nyumbani na uko mbali huwezi kuvifata na ukawahi kwa muda uliopewa. Jamani kama inawezekana naomba hili lilekebishwe.