Kero katika mchakato wa kuandikisha vitambulisho vya TAIFA

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Zoezi hili linaloendelea Dar limekua kero sana,,,,wahusika hawajajipanga kabisaa uwe umewahi au umechelewa,,,,,,ukifika unapaswa kuangalia majina ukutan,kwa bahat mbaya hayapo kwa mfumo wa Al-fabeti,yameandikwa kwa mkono,,,,mchakato huo unaweza ukala saa nzima,,,kisha ndo ukapange foleni sasa ya kwenda kujiandikisha,,,ukifika kwa karani kama huna baadhi ya particulars let say namba ya nyumba unarudi ulikotoka,,,,,,mfano eneo nililokatiza mimi kuna dada ambaye ni karan amemchania form mmoja wa raia kwakua hana namba ya nyumba,lakini ukiangalia sana uhamasishaji wa zoez hili si mkubwa sana kama vile wa kupiga kura,,,,,,sijui wewe ambae umejiandikisha umekumbana na kadhia gani??????
 
1. Foleni isiyoeleweka.....
2. Nyumba yangu mpya huku uswazi, hata namba sina, hivyo nimebuni
3. Nilitumia muda mrefu (maana sikuandikishwa mtaaani, ikabidi nisubirie niandikishwe)
4. Niliulizwa jina la mjumbe..... Kwa kuwa silijui nikataja tu thanx to orodha ya wajumbe iliyobandikwa ukutani kwenye ofisi ya serikali ya mtaa.
5. Wasajili wenyewe wapo super slow.......
 
dah,,,,hiyo kadhia ndo nakumbana nayo hapa mdau
 
Hakuna chochote kile ambacho Serikali hii DHAIFU itakifanya na kisiwe na matatizo chungu nzima.
 
pole sana,
funny enough mbele yangu kulikuwa na ndugu watatu,
wakiulizwa makazi ya kudumu wanamuuliza mwezao tujaze wapi?
anawaambia karagwe....
imagine watu wazima hawajui makazi yao ya kudumu ni wapi.....

namba za simu wakaweka za huyu ndugu yao, ikabidi dada wa watu afute then kila mmoja amwandikie namba yake ndo aziandike.....

foleni zinachangiwa na mengi...

halafu uswahilini kwetu wametuandikisha tu, wanadai zoezi la picha litafanywa baadae....
sipati picha itakavyokuwa...

Nadhani sina haja ya kuwa na hiki kijitambulisho...! Kuna siku (miaka minne ijayo) tutaanza upya hili zoezi kwa hiyo usipoteze muda wako sasa...!
 
the same to here,,,hiyo itaambatana na finger print,,,,sasa basi ni lini hatujui.....pia kuna wazushi wa usalama wa taifa wanaingia kuja kutibuatibua zoezi hapa,,,,,
 
hahahahahahaaa,,,usemayo yana tija,,,,nimemuuliza karan amenambia ni zoez endelevu
 
sitoshangaa wakidai fomu za baadhi ya watu zimepotea....
sioni sababu za msingi za kufanya hayo...
unless kama wanataka kugawa ulaji tu kwa watu wachache maana nchi hii kila kitu dili...

the same to here,,,hiyo itaambatana na finger print,,,,sasa basi ni lini hatujui.....pia kuna wazushi wa usalama wa taifa wanaingia kuja kutibuatibua zoezi hapa,,,,,
 
pole sana,
funny enough mbele yangu kulikuwa na ndugu watatu,
wakiulizwa makazi ya kudumu wanamuuliza mwezao tujaze wapi?
anawaambia karagwe....
imagine watu wazima hawajui makazi yao ya kudumu ni wapi.....

namba za simu wakaweka za huyu ndugu yao, ikabidi dada wa watu afute then kila mmoja amwandikie namba yake ndo aziandike.....

foleni zinachangiwa na mengi...

hapa kuna mtu hajui namba ya nyumba yake wala namba yake ya simu........weweeeee
 
1. Foleni isiyoeleweka.....
2. Nyumba yangu mpya huku uswazi, hata namba sina, hivyo nimebuni
3. Nilitumia muda mrefu (maana sikuandikishwa mtaaani, ikabidi nisubirie niandikishwe)
4. Niliulizwa jina la mjumbe..... Kwa kuwa silijui nikataja tu thanx to orodha ya wajumbe iliyobandikwa ukutani kwenye ofisi ya serikali ya mtaa.
5. Wasajili wenyewe wapo super slow.......

hayo yote yapo hapa,kuna wengine wanaomba form wakajazie nyumban kwao
 
Binafs nimeamua nisijisumbue na kujibebesha na usumbu toka kwa serikali yangu Dhaifu badala ya kwenda kutafuta mkate wa kila siku
Nimeamua kuachana nao kwanza,na kwenda kutafuta riziki,haya mambo mengine ya vitambulisho yatafata tu badaae,poleni sana nyie ambao mpo bize na vitambulisho badala ya mkate wa watoto
 
Hawa NIDA hovyo kabisa. Watu wana PASSPORTS na DRIVERS LICENCE sijui kwa nini wasitumie database za UHAMIAJI na TRA kuhakikisha kuwa watu wote wenye PASSPORTS na D/L hawahitaji kupanga foleni.
 
kwa mfumo huu wa bongo???tena basi so simple ila wao wameamua kujitengenezea mahela ya bure,,,,maana kama issue ya pass kuna fingaprinti na huku itakuwepo
 
Binafs nimeamua nisijisumbue na kujibebesha na usumbu toka kwa serikali yangu Dhaifu badala ya kwenda kutafuta mkate wa kila siku
Nimeamua kuachana nao kwanza,na kwenda kutafuta riziki,haya mambo mengine ya vitambulisho yatafata tu badaae,poleni sana nyie ambao mpo bize na vitambulisho badala ya mkate wa watoto

kwa baadae wengine hawatakua na muda,,,wapo ambao muda huu wapo free usiku KAZINI,,,,,,
MFANO MKENYA WA KOVA,anateka watu usiku,
 
Back
Top Bottom