Kazi Tunayo Mbona!

Eliaona

Member
Jun 22, 2009
72
56
Mwl. JK Nyerere aliandika kijitabu kidogo kiitwacho "Uongozi na Hatima ya Tanzania".
Juzi juzi hapa habari ya Zimbabwe ikiwa joto juu Mzee Mandela akiwa huko London kwenye Birthday yake alisema hivyo hivyo juu ya Zimbabwe..
Sasa hapa kwetu tunasikia kila siku sakata juu ya sakata sio ndani ya CCM sio ndani ya Chadema sio CUF. Kweli tunaenda wapi, kwani tumeshindwa kabisa kuandaa viongozi wa nchi yetu hii?
 
Nyerere alikuwa hana jipya

anaendelea kututawala toka kaburini na la kufanya hatuna


Kama ingekuwa hivyo basi kusingekuwa na hata harufu ya Rushwa. Kila siku najiuliza kama angekuwepo EL saa hizi angekuwa wapi. Au viongozi wa Chama wanaokumbatia ufisadi wangekuwa wapi. Yeye aliweza kuwatolea uvivu hata PM Malecela na Secretary General Kolimba enzi hizo. Sidhani kama angeshindwa kufanya hivyo leo, hata kama angetembelea mkongojo.

Mkuu yule Mzee alikuwa na mabaya yake lakini la ufisadi au kuutetea hakuwepo. Let him have a good rest.
 
Nadhani ishu siyo chama. Anayepewa madaraka ndani ya chama, ndiyo tatizo. Kwani hata dini; japokuwa zinahubiri wema, lakini wengine, miongoni mwao wanafanya mambo ambayo hata shetani mwenyewe huwa haamini kama yanaweza kufanywa na wanadamu. Nikupe mifano. Ni kwa nini pope wa Roma alinusurika kupigwa risasi mwaka 1982? Sababu gani zilisababisha hata Kennedy, F (rais wa Marekani) kuuawa?

Majibu ya maswali haya na mengine yanaonyesha ni kwa jinsi gani dini zetu zinatumika kufanya mambo ya siasa na kusahau lengo lake kuu la kuhubiri ufalme wa Mbinguni.

Kwa hiyo, sishangai chama kikiwa kinavurugwa na watu wachache wanaokuwa wanakitumia vibaya na wengine wengi kukubali kufuata na hata kusifia matendo yao hata kama ni mabaya. Haya ni matokeo ya kutokutumia vizuri akili zetu na kuwaacha wengine wazitumie badala yetu. Hivi, tukubadilishana nchi; Watanzania wote wakahamia Marekani na Wamarekani wakaja Tanzania (kila watu waende kama walivyo, bila kuchukua kitu chochote), maisha ya Watanzania hawa wakiwa Marekani, yatakuwa endelevu kimaendeleo (sustainable)?

Think critically.
 
Back
Top Bottom