Kauli za Lissu na Lipumba ni changamoto sana kwa UKAWA

Wakati akichangia mjadala wa Bunge Lissu alisema haiwezekani kuungana na chama ambacho kimeunda serikali na chama tawala. Nae LIPUMBA akiwa msikitini akasema kuna chama kinafadhiliwa na mataifa ya ulaya yenye itikadi kama chama hicho ili kuchukua rasilimali za nchi. Nilifikri kauli hizi wangezifuta kwanza kabla hawajachkua jukumu la kuungana na kuwa UKAWA ili kuwarejesha wanachama wao kwenye mitazamo mipya ya vyama vyao

sikiliza kauli ya LIPUMBA akiwa msikitini:
.... UKAWA ni umoja kama umoja mwingine wowote ule,hii ni dalili zuri sana ya kuleta siasa za ushindani ktk nchi.Nawashauri baada ya issue ya katiba kwisha wawe na goal moja tu ambayo ni kuondoa ccm madarakani baada ya hilo ndio mengine yatafuata.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa namheshimu sana Prof. Lipumba lakini kutokana na clip hii nimemtoa katika kundi la watu wa maana kabisa. Anasimama anazungumza kama mtu ambaye hakwenda shule kabisa kuchochea udini kwa sababu tu anataka kuwa Rais mwaka 2015? Kwa msingi wa clip hii CUF ni chama cha kiislamu bila shaka hasa ukizingatia alichosema kwa nini ameendelea kugombea urais tangu 1995 kwamba ni ili kuwafanya waislamu kundi la raia first class. maana ya maneno hayo ni nini? Na anapowaambia waislamu wajipange kwa ajili ya mwaka 2015 maana yake nini? na anaposema raslimali nyingi ziko ukanda wa pwani ya bahari na wengi wanaokaa huko ni waislamu maana yake ni nini? mimi natilia mashaka sana uprofesa wake. Kosa la alilosema Mary Nagu kwamba katiba isiwe ya kidini kosa liko wapi? Mbona Nagu hakuwaandaa wakristo kwa mwaka 2015? Profesa umenisikitisha sana na kuanzia leo ninakutazama kwa jicho la tatu?
 
kitendo cha CUF kupinga serikali mbili, maana yake wamesamehewa madhambi yao yote, na sasa wako on truck. haiwezekani kusamehe dhambi moja moja.

Habari ya mjini ni wajumbe wa baraza kuu la CHADEMA kutoka Kigoma, Singida na Tabora hawajapewa hela zao zote na Mchange.

na mchange amewatukana matusi ya nguoni
 
kitendo cha CUF kupinga serikali mbili, maana yake wamesamehewa madhambi yao yote, na sasa wako on truck. haiwezekani kusamehe dhambi moja moja.

Habari ya mjini ni wajumbe wa baraza kuu la CHADEMA kutoka Kigoma, Singida na Tabora hawajapewa hela zao zote na Mchange.
Mkuu umewasahau wale wa Lindi na Nachingwea ambao wapo tayari kujisalimisha kwa Dr. Slaa kuomba nauli ya kurudia kwao!
 
Back
Top Bottom