Kauli ya Waziri wa Elimu na Akili za Wafrika chini ya Jangwa chini ya Jangwa la zahara

Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndo point ya msingi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ina maana wewe akili yako haijadumaa hahaha
Mkuu,akili yangu iko kama ilivyoumbwa na Mungu,nashukuru sijawahi kupigwa na wazee wangu hata siku moja,kila kitu ninachofanya nafanya kwa "experience" yangu...nina uthubutu,nina uwezo wa kujaribu kitu kipya,hali hiyo imenifanya nifanikiwe sana katika maisha yangu,na hivyo ndivyo ninavyowalea watoto wangu

Kumpiga mtoto ni kumlazimisha afanye kitu vile unavyotaka wewe mzazi bila ya kumpa sababu kwanini afanye unavyotaka,asifanye vile anavyotaka yeye,..kwa mantiki hiyo unamchanganya mtoto kiaakili unamdumaza akili,unamtia nidhamu ya woga aaogope kujaribu,asiwe na uthubutu

Mtoto wa jamii za kiafrika chini ya Jangwa la sahara anaanza kupigwa akiwa na miaka 3,huyu mtoto akifika miaka 10-16 anakuwa na akili gani?ndiio maana waafrika tuna "fail" kila kona...

Ukiona mtoto kafanya kitu usichokipenda wewe mzazi,kaa nae uongea nae umfanhamishe kwanini asifanye kile na athari,hapo unakuwa umemsomesha mtoto,umempa maarifa,hivyo ndivyo nilivyo lelewa mimi na wazazi wangu..fimbo azisaadii kitu

Mkuu umeshawahi kumuona Simba anafundisha watoto wake kuwinda,?Binadamu ni viumbe bora kuliko wanyama lakini jamii zetu za kiafrika zinahitaji kusoma kutoka kwa wanyama
 
Mwalimu kutoadhibu ni jambo linalowezekana kwa 100%
Fuatilia mwongozo huu: Mwalimu hakikisha umefika shule muda husika, simamia usafi na kama wanafunzi hawaonyeshi kushiriki kufanya usafi, tafadhali usishike kiboko. Mwalimu kumbuka muda wa vipindi ukifika hata kama mazingira ya shule ni machafu, wanafunzi waingie darasani tayari kwa masomo. Mwalimu fundisha kipindi chako kama mwongozo unavyoonesha, tafadhali usiwafuatilie wanafunzi wasioandika, kwani inaweza kuhamasisha hisia za kutoa adhabu ili kumjenga mwanafunzi husika. Mwalimu, daftari zikikusanywa kwa ajili ya kusahihisha, tafadhali usifuatilie kubaini wanafunzi wasiokusanya daftari kwani kubaini kwako kunaweza kupelekea kuwepo na mazingira yenye kuchochea adhabu.
Mwalimu wakati utakapoita majina, zingatia kuwa wale waliopo darasani kwa wakati huo ndiyo wanaokuhusu, hitaji lako la kutaka kujua mwanafunzi X ana tatizo gani la kutokuja shuleni linaweza kupelekea mazingira yatakayo chochea adhabu, kwani wanafunzi wenzie wakati mwingine watakupa jibu kuwa mwanafunzi X yupo maeneo ya chooni anacheza tu, hivyo jibu ili linaweza kupelekea mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu, mara upatapo kesi za mwanafunzi X kuwa amepigana darasani au kutoa lugha chafu, tafadhali tumia neno moja tu kuwa "LUGHA ZA MATUSI SI NZURI " kisha mruhusu kurudi darasani ili kuepusha mazingira ya adhabu. Mwalimu wangu mzazi akikuletea kesi ya mtoto wake kuhusu tabia za nyumbani na hata mwenendo mbovu wa maendeleo yake darasani, tafadhali mueleze mzazi kuwa amalizane na mwanaye kwa namna inayofaa. Mwalimu wangu ukifuata muongozo huu, shutuma na jazba za wana wa nchi hii utaziepuka pia itakusaidia japo kurudisha mwili wako uliopukutika kwa kufuatilia watoto wasiokuhusu, nakutakia kazi njema mwalimu wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
:cool:,Safi sana Mkuu haya uliyoyaandika ni moja ya maarifa mazuri.,kama mwalimu haitakuwa vizuri kutekeleza mwanafunzi wako, lazima iwepo hali ya kumsukuma mtoto afahamu kwanini yuko shule,adhabu za kisaikologia zinatakiwa zitumike,kumbuka mtoto kama mtoto anakuwa na hamu ya kudadadisi (curiosity)na kusoma mambo mapya mpaka anakuwa na umri wa kujiewa.,Utundu,utukutu ni moja katika "curiousity" ya maisha ya mtoto
 
:cool:,Safi sana Mkuu haya uliyoyaandika ni moja ya maarifa mazuri.,lakini katika hali ya kumsukuma mtoto afahamu kwanini yuko shule,adhabu za kisaikologia zinatakiwa zitumike,kumbuka mtoto kama mtoto anakuwa na hamu ya kudadadisi (curiosity)na kusoma mambo mapya mpaka anakuwa na umri wa kujiewa.,Utundu,utukutu ni moja katika "curiousity" ya maisha ya mtoto
Kama umesifia alichokiandika mkuu Hardq basi kiufupi ni kuwa hujamuelewa alichomaanisha. Msome taratibu.

Anyways! Hizo adhabu za kisaikolojia unazosemea unadhani hazitumiki mashuleni? Hivi unadhani walimu 13 kushinda na watoto 700 ingekuwa kila anayekosea anatandikwa hao walimu si wangelala hoi? Kwamba wana shinda wanapiga piga tu.

Unajinasibu kuwa kutochapwa hata kiboko kimoja kumekufanya kuwa mbunifu, mwenye uthubutu, kujiamini, mafanikio n.k. Kwa hiyo utaka kutuambia wewe una mafanikio sana, una uthubutu mkubwa na ni mbunifu kuliko sisi sote tuliowahi kuchapwa? Una nini hicho za ziada?
 
Mkuu kama huungi mkono kupigwa kwa watoto shuleni basi hujatafautiana na mimi aina yoyote ya kumuadhibu mtoto kupitukia ikiwa kwafi mbo au matusi ni kitu kibaya kwa kwani mtoto anapozaliwa anakuwa hajui chochote kile,mtoto anasoma kila kitu kutokana kwa wazazi au jamii iliyomzunguka

Kama jamii inayotaka mazuri kwa watoto tujifundishe kuiga mazuri na tuache mabaya,kiukweli nimeshatembea nusu ya dunia,lakini sijawahi kuona sehemu ambayo watoto wanaadhibiwa na wazazi wao aua shuleni kama watoto wa kiafrika,..

Matokeo yake tunayaona,Afrika ndio inayongoza kuwa na Viongozi madikteta,Afrika ndio inaongoza kwa umasikini,Afrika ndio inayongoza kwa kuwa na watu wajinga,hii inatokana na vipi tunawalea watoto wetu,unacholima ndicho unachovuna,mtoto umleaavyo ndivyo akuavyo,ukimlea mtoto kwa kumpiga na yeye atakuja kuwapiga anaowaongoza kama mtoto huyo atapa nafasi ya kuwaongoza wenziwe
Mkuu, katika hizo nchi 98 ulizowahi kutembelea. Ulifanya utafiti wa kisayansi na kubaini kuwa Africa ni maskini sababu ya kuchapa watoto?

Katika hizo nchi 98 unazosema umetembelea, ulitafiti na kubaini kuwa maendeleo makubwa yalipatikana mara baada ya wao kusitisha viboko?

Ulifanya utafiti gani na kubaini viongozi wote madikteta wa Africa walichapwa utotoni na wale democratic hawakuwahi kuchapwa? Uliwahoji wangapi?
 
Ndio mkuu nimefanya utafiti ndio maana naandika haya niyaoandika,Haina haja kumuhohi Dikteta, ukiangalia vitendo vya mtu utajua huyomtu kakulia katika famila gani,mafano wewe kutokana na commets zako inaonyesha umetoka katika familia ambayo mtoto anapigwa anaadhibiwa bila kupewa nafasi ya kujielezea..

Moja, katika tafiti ya kwanza niliyoiona nafikiri ilikuwa Marekani,waliwekwa watoto wa nchi tafauti lakini watoto wa Kiafrika wanaoishi chini ya jangwa la Sahara walikuwa ndio wenye IQ ndogo kupita wengine,nilisikita na kutafakari kwanini imekuwa vile,hapo ndipo nilipoanza kufanya tafiti vipi wenzetu wanawalea watoto wao

Pili ,ukiangalia maamuzi yetu yanakuwa ya kukurupuka,bila ya kuyafanyia utafiti kwababu ubongo wetu umeshazoea kuamuliwa tangu tukiwa watoto,mtoto wa kiafrika chini ya Jangwa la sahara hawana maamuzi katika familia yake,

Kutompa uwezo mtoto kuamua kinamfanya mtoto akiwa mkubwa awe hana uwezo au anakuwa na uwezo mdogo wa kuamua, ubongo wake unakuwa umedumaa kwa kulazimishwa kwa fimbo au matusi,..."Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" waswahili wamesema

Tatu, ni tabu kumkuta mwafrika chini ya Jangwa la Sahara anaejiamini au kujisifu kama yeye ana thamani kama mwanadamu,watoto wa nchi za Afrika chini ya jangwa la sahara wanakulia bila ya kusifiwa na wazazi wao,

Watoto hawaambiwi wanapendwa au kusifiwa kama kafanya kitu kizuri anachofanya,wazazi hawana tabia ya kuwasifu watoto wao hii inamwathiri mtoto kisaikologia inamfanya asijipende na ndio maana utakuta wafrika wa nchi za chini ya jangwa la Sahara wote wana tabia moja ya kusifu watu wengine,watasifu wazungu,wahindi,nk lakini hawajisifu wao wenyewe wajiona hawana uwezo

Mkuu hizo ni baadhi za tafiti,kama nitaziandika tafiti zote nilizofanya naweza kuandika kitabu na hilo ndio lengo langu,Mkuu kuna mzee wako yoyote ameshawahi kukwambia anakupenda,wewe ni mtoto mzuri,...au wewe umeshawahi kuwasifu watoto wako kama unao!??,wenzetu hayo ni maneno ya kawaida kwa watoto wao kila siku
 
Kama umesifia alichokiandika mkuu Hardq basi kiufupi ni kuwa hujamuelewa alichomaanisha. Msome taratibu.

Anyways! Hizo adhabu za kisaikolojia unazosemea unadhani hazitumiki mashuleni? Hivi unadhani walimu 13 kushinda na watoto 700 ingekuwa kila anayekosea anatandikwa hao walimu si wangelala hoi? Kwamba wana shinda wanapiga piga tu.

Unajinasibu kuwa kutochapwa hata kiboko kimoja kumekufanya kuwa mbunifu, mwenye uthubutu, kujiamini, mafanikio n.k. Kwa hiyo utaka kutuambia wewe una mafanikio sana, una uthubutu mkubwa na ni mbunifu kuliko sisi sote tuliowahi kuchapwa? Una nini hicho za ziada?

Mkuu nina kila kitu cha ziada lakini hii sio mada ya kuelezea uwezo wangu,kitu kikubwa nichojisifia ni kuona ambacho watanzania wenzangu hawakioni,au wanakiona lakini wanakipuuza kwa vile wanakiona ni kiti cha kawaida kwa vile na wao walikuwa wahanga wa hilo jambo

"Child abuse" (unyanyasaji kwa watoto),hicho ndicho ninachokiona katika jamii yetu ya kitanzania,wewe hukioni au unakiona lakini kwa vile ni muhanga wa mateso hayo unaona ni kawaida tu kwa mtoto kupigwa mpaka kufa na mwalimu,jamii inzima imekaa kimya,kifo cha huyu mwanafunzi ni "wake up call",hatua za haraka zinatakiwa zichuliwe,lakini unakuta Waziri anatoa kauli ya porojo

nikisoma hii comments yako imejaa hazira,hizo hasira zinasababibwa na kichapo,na adhabu za kupitukia ulizozipata ulipokuwa mtoto,mimi sioni kwanini umejawa na hasira wakati huu ni mjadala(debate) tu,una hasira kwasababu hujalelewa katika mazingira ya kujadiliana...

Najisifu sijawahi kuchapwa na wazee wangu,najisifu sichapi watoto wangu,nataka na wewe na watanzania wengine mbadilike msichape watoto wenu wala msiwape adhabu za kupitukia kwani hamsaidii chochote mtoto,haisadii chochote taifa letu,..

Serikali inatakiwa iondoe adhabu ya kuchapwa wanafunzi mashuleni,tutafika,matokeo tutayaona

teac.jpg
 
Mtoto mwengine kapigwana na mwalimu hadi kuzimia Geita,hivi sasa mtoto huyo yuko hospitali haijulikani hatma ya maisha yake,inasikitisha sana kuwa habari kama hizi hivi sasa zimekuwa ni stori za kawaida katika mitandao ya kijamii,Juzi tu huko Bukoba mtoto amepigwa na mwalimu wa "Nidhamu" mpaka amefariki..

Katika tukio la mwanzo lililotokea Bukoba,Waziri wa Elimu alijitokeza na kutoa kauli kuwa kile kitendo cha mwalimu kumpiga mwanafuzi mpaka kupoteza maisha ni "bahati mbaya",kwa ufupi kauli ile kama mzazi niliipokea kwa huzuni sana,kwani niliona kama huyu waziri amehalalalisha kupigwa yule mtoto mpaka kifo kumkuta,kama kawaida yetu wafrika chini ya Jangwa la sahara mwalimu hajakosea ni mtoto mwenye makosa..

Kwa upande mwingine sikumshangaa sana Waziri kwa ile kauli yake,kwani pengine yeye mwenyewe kapigwa sana na wazazi wake,labda katika famili yake kuchapa na kuwadhibu watoto kwa kuwachapa ni kitu cha kawaida tu,anawafanyia watoto wake kama vile alivyofanyiwa yeye na wazazi wake..

Kitu kilichonishangaza sana kuwa huyu waziri wa elimu ni mwanamke,hivi kweli kama yeye ni mzazi hakuona uchungu au huruma kwa yale yaliyomkuta yule mtoto kule Bukoba,?kwanini hakukemea kile kitendo ikawa ni fundisho kwa Walimu wengine!?Waziri anatakiwa aondoshe adhabu ya kuchapwa wanafunzi mashuleni,walimu hawalipwi kuchapa wanafunzi wanakipwa kwa kusomesha,takribani dunia nzima sasa wanafunzi hawapigi mashuleni,ni nchi za Afrika chini ya Jangwa la sahara tu ndio mpaka leo wanafunzi wanapewa adhabu ya kuchapwa..

Mfano wa Waziri wa Elimu ni mmoja katika mifano mingi inayotokea katika nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara,Majuzi waziri wa mambo ya Ndani alitoa kauli na maagizo ya utata,kuhusu Watanzania wanaosafiri na kufanya kazi Ughaibuni,kauli yake ile iliwapa mateso makubwa sana watanzania wanaoishi au kufanya kazi nchi za nje,wako waliokataliwa wasisafiri,wako waliombwa waonyeshe pesa au kibali cha kufanya kazi huko waendako,yaani mashaka juu ya mashaka..

Kama wiki mbili zilizopita katika mitandao ya kijamii zilijaa stori za mwandishi wa habari aliempiga picha Askali Polisi aliekuwa amelewa kwa kunywa pombe huku akiwa amevaa nguo za jeshi hilo,kama kawaida yetu waafrika chini ya Jangwa la Sahara,badala ya kumpongeza yule mwandishi wa habari kwa kumuanika Askari mtovu wa Adabu aliekuwa hana nidhamu,hapana haikuwa hivyo,imekuwa kinyume chake,kibao kikamgeukia yule mwandishi akawaa anasakwa kwa kila kona na vyombo vya usalama kwa kosa la kumpiga picha askari akiwa amelewa..

Katika nchi yetu kuna mifano na visa vingi ambavyo maamuzi yake hutolewa kwa hisia kuliko uhalisia wa lile jambo, na hiyo ndio hulka ya Waafrika waishio chini ya Jangwa la Sahara,mfano kila siku tunasikia madereva wanapewa shutuma na lawama nyingi za ajali za barabarani,lakini ukitizama kiundani zaidi utaona kwaukweli Madereva sio wenye makosa, wenye makosa ni wasimamizi wa Barabara nafiikiri ni "Tanroad" kama sikosei,barabara za Tanzania ziko chini ya kiwango,Barabara haziwezi kumuongoza Dereva barabrani,dereva inabidi atumie akili ya ziada kuendesha gari Tanzania,..

Kuna siku nilipata "shock" nilikuwa naendesha gari mitaa ya Mjini Daresalam ambapo nilikutana na "junction" inayopita mabasi ya mwendo kasi,cha kushangaza kulikuwa hakuna "sign" yoyote iliyokuwa inanitahadharisha kuwa huko uendako kuna njia ya mabasi ya mwendo kazi,hiko..

Naomba wale tuliowapa majukumu ya kutuongoa waache kutoa maamuzi yao kwa kutumia Hisia zao wajaribu kuangalia uhalisia wa jambo,sio kila siku kulaumu na kuwapa raia shutuma zisizo za lazima,watawala mnatupa raia nidhamu ya woga,taifa lenye raia wenye woga,raia wanaokosa uthubutu wa kujaribiu ni taifa ambalo ni rahisi kukosa maendeleo,rahisi kuangamia...
Mtu akishakuwa kiongozi anapungukiwa na hekima.
 
Mtoto hana ujinga,mtoto ana uthubutu mkubwa na ndio maana wazazi wengine hawawezi kuvulia vitendo vyengine wanavyofanya watoto wao,mtoto kama mtoto anapozaliwa nakuwa hajui chochote kwake kila anachokifanya ni kusoma,kama mzazi unamkatisha mtotoyale anayoyafanya kwa kumchapa badala ya kumfahamisha unamfanya mtoto awe mjinga,unapunguza uwezo wa IQ yake,na ndio maana ukimchua mtoto wa kizungu au wakihindi na kumwekana mtoto wa kiafika,mtoto wa kiafrika anaonekana ana IQ ndogo,..

Nakumbuka tulikuwa tunasema watoto wa kihindi na wakiarabu wanadekezwa na wazee wao, kwahiyo wataregea,hawatoyamudu maisha,lakini ukitizama katika jamii ya Tanzania jamii iliyopiga hatua kimaendeo,kibishara,kielimu,kiutajiri ni jamii za kiarabu na za kihindi!!, Waafrika wako wapi!?,Vichapo walivyopewa watoto wa kiafrika kimewafanya akili zao zidumae,

tafakari
Mkuu hoja yako inahitaji akili ya kufikiria nje ya boksi kuielewa. Ndio maana naona kama wengi hawakuelewi. Lakini usemacho ni ukweli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio mkuu nimefanya utafiti ndio maana naandika haya niyaoandika,Haina haja kumuhohi Dikteta, ukiangalia vitendo vya mtu utajua huyomtu kakulia katika famila gani,mafano wewe kutokana na commets zako inaonyesha umetoka katika familia ambayo mtoto anapigwa anaadhibiwa bila kupewa nafasi ya kujielezea..

Moja, katika tafiti ya kwanza niliyoiona nafikiri ilikuwa Marekani,waliwekwa watoto wa nchi tafauti lakini watoto wa Kiafrika wanaoishi chini ya jangwa la Sahara walikuwa ndio wenye IQ ndogo kupita wengine,nilisikita na kutafakari kwanini imekuwa vile,hapo ndipo nilipoanza kufanya tafiti vipi wenzetu wanawalea watoto wao

Pili ,ukiangalia maamuzi yetu yanakuwa ya kukurupuka,bila ya kuyafanyia utafiti kwababu ubongo wetu umeshazoea kuamuliwa tangu tukiwa watoto,mtoto wa kiafrika chini ya Jangwa la sahara hawana maamuzi katika familia yake,

Kutompa uwezo mtoto kuamua kinamfanya mtoto akiwa mkubwa awe hana uwezo au anakuwa na uwezo mdogo wa kuamua, ubongo wake unakuwa umedumaa kwa kulazimishwa kwa fimbo au matusi,..."Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" waswahili wamesema

Tatu, ni tabu kumkuta mwafrika chini ya Jangwa la Sahara anaejiamini au kujisifu kama yeye ana thamani kama mwanadamu,watoto wa nchi za Afrika chini ya jangwa la sahara wanakulia bila ya kusifiwa na wazazi wao,

Watoto hawaambiwi wanapendwa au kusifiwa kama kafanya kitu kizuri anachofanya,wazazi hawana tabia ya kuwasifu watoto wao hii inamwathiri mtoto kisaikologia inamfanya asijipende na ndio maana utakuta wafrika wa nchi za chini ya jangwa la Sahara wote wana tabia moja ya kusifu watu wengine,watasifu wazungu,wahindi,nk lakini hawajisifu wao wenyewe wajiona hawana uwezo

Mkuu hizo ni baadhi za tafiti,kama nitaziandika tafiti zote nilizofanya naweza kuandika kitabu na hilo ndio lengo langu,Mkuu kuna mzee wako yoyote ameshawahi kukwambia anakupenda,wewe ni mtoto mzuri,...au wewe umeshawahi kuwasifu watoto wako kama unao!??,wenzetu hayo ni maneno ya kawaida kwa watoto wao kila siku
Mkuu, nilitegemea utaniwekea summary ya utafiti wako na si hisia na fikra binafsi baada ya kuona jambo. Unless uwe hujui utafiti ni nini, japo naamini unajua.

Tafadhali nitajie tittle ya utafiti wako ilikuwa ni nini? Research design yako ni ipi? Research methodology yako ilikuwa ipi? Qualititative, quantitative or both? Sample yako ilikuwa ipi? Sample size? Findings ulizopata ni zipi n.k

Kuhusu mimi. Nimelelewa na wazazi waliokuwa wananisifu, kunitia moyo, kunipa zawadi ninapofanya vizuri, kunishauri, kunishaurisha, kuniongoza na hata kunionya. Lakini hii haikuzuia nisichapwe. Ninaonywa mara ya kwanza, ya pili, ya tatu ni bakora.

Hata shuleni nimechapwa (si kikatili) japo si kila wakati coz i tried to follow what i had been instructed by my teachers. Watukutu walitulizwa kwa viboko. Na sijaona athari zozote. Hizo sifa unazosema unazo eti sababu hukuchapwa, ni za kawaida kwangu. I have the same attributes.

Ni kweli Africa tunaweza kuwa na matatizo katika malezi na hasa kuwajengea watoto wetu uwezo ila si kweli ni sababu ni viboko viwili ninavyomchapa mwanangu pale napoona hataki kufata maelekezo.

Kuhusu mwanangu, anajua nampenda, nampa zawadi inapobidi, namsifu na kumjengea uwezo ila kwa mengine lazima ale fimbo. Mf. Nilishamwambia kuwa simu ya baba haichezewi, ana vitu vyake kibao vya kuchezea. Anajifanya hasikii, kanivunjia kioo, unataka nimuite nimpe ushauri nasaha? Then kesho arudie kwa kunivunjia tablet nimuite kumpa ushauri? Ni fimbo kidogo na kuanzia hapo hagusi tena hata niiache wapi.

Sasa wewe mwanao akipasua laptop endelelea kumpa ushauri nasaha. Eti ni udadisi
 
Mkuu hoja yako inahitaji akili ya kufikiria nje ya boksi kuielewa. Ndio maana naona kama wengi hawakuelewi. Lakini usemacho ni ukweli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,najaribu kuwafahamisha watanzania wenzangu kadiri iwezekanavyo,kweli ni tabu sana kwao kufahamu,kwasababu wengi wao wamekuwa wahanga wa kichapo kutoka kwa wazee au walimu mashuleni

Hili ni janga la Taifa,lakini watanzania uwelewa wao mdogo,kama haya ninayoyasema kasema Mzungu basi moja kwa moja wangeliyatia maanani, kwasababu ndio tulivyolelewa,hatujapewa thamani na wazee wetu au walimu wetu,tumelelewa kuwasifu wengine na kujidharau weneyewe...
 
Mkuu nina kila kitu cha ziada lakini hii sio mada ya kuelezea uwezo wangu,kitu kikubwa nichojisifia ni kuona ambacho watanzania wenzangu hawakioni,au wanakiona lakini wanakipuuza kwa vile wanakiona ni kiti cha kawaida kwa vile na wao walikuwa wahanga wa hilo jambo

"Child abuse" (unyanyasaji kwa watoto),hicho ndicho ninachokiona katika jamii yetu ya kitanzania,wewe hukioni au unakiona lakini kwa vile ni muhanga wa mateso hayo unaona ni kawaida tu kwa mtoto kupigwa mpaka kufa na mwalimu,jamii inzima imekaa kimya,kifo cha huyu mwanafunzi ni "wake up call",hatua za haraka zinatakiwa zichuliwe,lakini unakuta Waziri anatoa kauli ya porojo

nikisoma hii comments yako imejaa hazira,hizo hasira zinasababibwa na kichapo,na adhabu za kupitukia ulizozipata ulipokuwa mtoto,mimi sioni kwanini umejawa na hasira wakati huu ni mjadala(debate) tu,una hasira kwasababu hujalelewa katika mazingira ya kujadiliana...

Najisifu sijawahi kuchapwa na wazee wangu,najisifu sichapi watoto wangu,nataka na wewe na watanzania wengine mbadilike msichape watoto wenu wala msiwape adhabu za kupitukia kwani hamsaidii chochote mtoto,haisadii chochote taifa letu,..

Serikali inatakiwa iondoe adhabu ya kuchapwa wanafunzi mashuleni,tutafika,matokeo tutayaona

View attachment 854458
Hasira iko wapi kwenye comment yangu? Unaweza ku quote nilipoonesha hasira? Au ni wewe ndio hujui majadiliano ya hoja mkuu?

Sijasifu kupigwa na kuuwawa kwa mtoto wa Bukoba na nina laani kwa nguvu zote na kukemea any kind of child abuse. Lakini hii haimaanishi adhabu ya viboko haifai kabisa kuwepo. Kama ikitolewa kwa utaratibu mzuri uliowekwa basi inafaa.

Hata hizo nchi walizofuta na wao sasa wako kwenye debate ya kurudisha au la.
 
Mkuu, nilitegemea utaniwekea summary ya utafiti wako na si hisia na fikra binafsi baada ya kuona jambo. Unless uwe hujui utafiti ni nini, japo naamini unajua.

Tafadhali nitajie tittle ya utafiti wako ilikuwa ni nini? Research design yako ni ipi? Research methodology yako ilikuwa ipi? Qualititative, quantitative or both? Sample yako ilikuwa ipi? Sample size? Findings ulizopata ni zipi n.k

Kuhusu mimi. Nimelelewa na wazazi waliokuwa wananisifu, kunitia moyo, kunipa zawadi ninapofanya vizuri, kunishauri, kunishaurisha, kuniongoza na hata kunionya. Lakini hii haikuzuia nisichapwe. Ninaonywa mara ya kwanza, ya pili, ya tatu ni bakora.

Hata shuleni nimechapwa (si kikatili) japo si kila wakati coz i tried to follow what i had been instructed by my teachers. Watukutu walitulizwa kwa viboko. Na sijaona athari zozote. Hizo sifa unazosema unazo eti sababu hukuchapwa, ni za kawaida kwangu. I have the same attributes.

Ni kweli Africa tunaweza kuwa na matatizo katika malezi na hasa kuwajengea watoto wetu uwezo ila si kweli ni sababu ni viboko viwili ninavyomchapa mwanangu pale napoona hataki kufata maelekezo.

Kuhusu mwanangu, anajua nampenda, nampa zawadi inapobidi, namsifu na kumjengea uwezo ila kwa mengine lazima ale fimbo. Mf. Nilishamwambia kuwa simu ya baba haichezewi, ana vitu vyake kibao vya kuchezea. Anajifanya hasikii, kanivunjia kioo, unataka nimuite nimpe ushauri nasaha? Then kesho arudie kwa kunivunjia tablet nimuite kumpa ushauri? Ni fimbo kidogo na kuanzia hapo hagusi tena hata niiache wapi.

Sasa wewe mwanao akipasua laptop endelelea kumpa ushauri nasaha. Eti ni udadisi
Ungemuelekeza kwa maneno angekuelewa vizuri sana kuliko kumrarua mafimbo.

Too bad.

Mkuu,Title, Summary,methodologies,theory nk, ya utafiti wangu itakusaidia nini?jibu hoja ya hii mada naona ndio muhimu kuliko Title au Summary za utafiti wangu,

Mkuu umeleta ubishi wa kijiweni,Madhumuni ya hii mada ni kuelimishana,,,,lakini kama kawaida ya watu walipigwa utotoni umetoka katika maudhui ya mada umekuja na majibu na ubishi wa kijiweni..

Mkuu,una kila "tendency" ya kuwa "abused" ulipokuwa mtoto,mengi uliyoyandika katika hii "comment" yako ni ya uongo,cha kweli ulichokiandika ni kuwa unampiga mwanao,pole sana..

Ningekushauri acha kuchapa mtoto wako,je huyo mwanao utaanza kumpa kichapo bila ya kuuliza kwanini amevunja hiyo "Tablet",je kama ni bahati mbaya,!?Je kama yuko "curious" ya kutaka kujua nini hiyo "Tablet" kwasababu hujawahi kukaa nae hata siku moja ukamfahamisha hicho ni kitu gani..

Watoto wanazaliwa na shauku la kusoma kitu kipya,ni jukumu lako wewe mzazi kumfamfahamisha mtoto pale unapoona mtoto anashauku la kuchezea hicho kitu...

Kumpiga fimbo kwamadhumuni ya kuwa asiguse tena hicho kitu ni kumdumaza akili mtoto wako,hapo hujamfundisha kitu isipokuwa umemfanya awe mjinga,umempunguzia shauku lake lake la kutaka kujua mambo mapya,umepunguza uwezo wa IQ yake..tafakari

Unamlea mtoto wako kama ulivyolelewa na wazee wako,"cut the abused chain my friend", jirekebishe kaka
 
Back
Top Bottom