Kauli ya Ole Medeye itazamwe

JANA chombo kimoja cha habari kilimkariri Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye, akisema kuwa kampuni moja imewahi kumpa dola za Marekani 800,000 (sawa na takriban shilingi bilioni moja) za hongo ikitaka atoe upendeleo katika kugawa eneo.

Kilichotufanya hadi kufikia hatua ya kuandika tahariri hii ni kitendo cha naibu waziri huyo kutoi taja kampuni iliyotaka kumpa hongo hiyo, eneo ambalo lilihusika na hatua ambazo aliichukulia.

Kauli hiyo imetushangaza kwa sababu, Ole Medeye kama kiongozi, anafahamu kwamba kitendo kilichofanywa na kampuni hiyo ni kosa na yeye kukaa bila kuchukua hatua pia ni kosa.

Sisi Tanzania Daima tunajiuliza, kama Ole Medeye ambaye ni mfano wa kuigwa amelichukulia jambo hilo kimzaha, je, anatoa somo gani kwa watu wengine?

Sote tunafahamu ya kwamba kuna migogoro mingi ya ardhi katika nchi yetu ambayo inahitaji mapinduzi ya kweli katika kuishughulikia.

Wakati tukiwa katika wimbi la migogoro hiyo, inashangaza kusikia bado kuna watu ambao wanataka kupitia njia za mkato ili kunyang?anya haki za watu wengine kwa kupewa upendeleo.

Cha ajabu, naibu waziri anayeongoza wizara nyeti ya serikali analiacha jambo hilo lipite hivi hivi bila kuchukua hatua stahiki, ili uwe mfano kwa watu wengine wenye tabia na mwenendo wa kampuni iliyotaka kumpa hongo ya shilingi bilioni moja.

Sisi Tanzania Daima kama chombo huru cha habari, tunaamini njia sahihi ya kuanza kupunguza migogoro ya ardhi inayoikabili nchi yetu sasa hivi ni kuanza kupambana na rushwa.

Tunasema hayo kwa sababu rushwa imekuwa ni kikwazo kikubwa kinachochangia migogoro mingi ya ardhi.

Kuna baadhi ya watu leo hii wamepokonywa haki yao ya kumiliki ardhi kwa sababu tu kuna mtu mwenye pesa aliwarubuni viongozi nao wakabariki dhambi hiyo.

Kutokana na hilo, kwanza, tunamtaka naibu waziri kuiweka hadharani kampuni anayodai kwamba ilitaka kumpa hongo ya sh bilioni moja.

Pili, tunahitaji kusikia hatua ambazo ataichukulia, na asipofanya hivyo tutakosa imani naye kama naibu waziri wa Ardhi ambaye kwa nafasi yake anaweza kushughulikia migogoro ya ardhi kwa mamlaka makubwa, hasa katika eneo la rushwa ambalo limekuwa kikwazo kikubwa.

Tatu, tunaamini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesikia kauli ya naibu waziri huyo wa Ardhi na tunaamini itachukua hatua zinazostahili ili kuisaidia wizara katika kushughulikia migogoro ya ardhi inayoanzia kwenye rushwa.

Tunaamini Naibu Waziri Ole Medeye kama kweli kwa kushirikiana na Waziri wake, Anna Tibaijuka, wanataka kuleta mageuzi katika wizara hiyo ambayo baadhi wanaiita ya migogoro ya ardhi, atoe ushirikiano wake kwa kuitaja kampuni hiyo na nyingine kama zipo ambazo hajazisema, zilizoonesha kutoa hongo kwa nia ya kunyang?anya haki za wengine ili ziweze kuchukuliwa hatua.

Ole Medeye asipofanya hivyo, tutakosa imani na yeye kama kiongozi aliyepewa wadhifa na mamlaka ya kushughulikia mambo ya ardhi na maendeleo ya makazi kutekeleza wajibu wake kwa malengo yaliyokusudiwa.

Na Mtu wa namna hii ndio sasa anatafuta uspika aongoze muhimili.
Chadema mna dhihaka..mmemtangaxa hafai kisha mnampa kugombea.
Inakula kwenu sasa hv.
 
Kwa ratio ya wabunge hakuna namba yoyote mwanachama wa vyama mbadala anaweza kushinda uongozi wowote bungeni. Ila kwa uhakika Jenista Muhagama atakuwa Naibu Spika. Maana JPM kastuka kuona anataka kutumiwa
 
Wanachadema na maccm mnashangaza sana na mtaendelea kuibiwa kura mpaka muache ndimu mbili na kuwapokea maccm, japo maccm majizi nyie matapeli
 
Hili swali la Tanzania Daima lilijibiwa?

Lilijibiwa kuwa hiyo hela aliyoikataa naibu waziri,waziri wake aliichukua kwa ajili ya kubadilisha mboga nyumbani kwake.
Ina maana hukumsikia au unataka kumchokonia prof.Tiba?
 
Lilijibiwa kuwa hiyo hela aliyoikataa naibu waziri,waziri wake aliichukua kwa ajili ya kubadilisha mboga nyumbani kwake.
Ina maana hukumsikia au unataka kumchokonia prof.Tiba?

Huu ni uongo.
'Pesa ya mboga' ni maswala ya escrow.
Haihusiani kabisa na maswala ya kuhongwa ili mtu apewe kiwanja.
Na hii ishu ya Medeye ni dola laki nane wakati pesa ya mboga ni mshiko tofauti kabisa.
 
Na Mtu wa namna hii ndio sasa anatafuta uspika aongoze muhimili.
Chadema mna dhihaka..mmemtangaxa hafai kisha mnampa kugombea.
Inakula kwenu sasa hv.
Anayetembeza rushwa usiku kucha kwenye hotel na kupiga watu nani bora si afadha;li Ole Mdeye,
 
Back
Top Bottom