Katika Mikenge wananchi wa kawaida tuliwahi kuingizwa na kununua hisa za Voda

Hawatoi hata mya mbofu sijui labda wenye mahisa mengi ... binafsi toka ninunue sijawahi pata gawio na mahisa yenyewe hayauziki yanazidi kuporomoka
Mkuu unachojaribu kufanya ni propaganda au nini? Hujawahi pata gawio lako hata mara moja?

Mbona mi nimepokea mara mbili ya mwaka jana hawajatoa walisema biashara haikua nzuri sijui mwaka huu watakuja na sababu gani. Umenishangaza kusema hujawahi kupokea gawio kabisa
 
Mlionunua hizo hisa hamna tofauti na hawa 👇🐒

20220427_213135.jpg
 
Nenda kwa wakala ukaweke order ya kuuza hisa zako za Vodacom iwe kwa bei ya soko uwekeze sehemu nyingine au utumie chako. Kaa mbali na hisa za Presicion Air(PAL) na Mwalimu Commercial Bank(MCB) kwani hawajui ni kwa nini waliamua kutafuta mitaji kwenye soko la hisa, hawajui wajibu wao kwa wanahisa au wanatumia mwanya wa kukosa usimamizi imara wa DSE kupata mitaji rahisi inayofanana na DECI.
 
Yaani huu ulikuwa mkenge mmoja matata sana. Hakunaga gawio hata 100 ningejua milioni 3 yangu ningekunywa windoki tu. Dustbin.

Ova

Hivi unafahamu hata maana ya soko la HISA kwanza.
sijui hata kama uchumi unaendeshwaje kama unavofikiria.
kuna mda hata ccm walishatuona wajinga sisi wananchi acha ninyamaze maana kama ujuhi hisa bora kaa kimya acha wafaidi wakubwa na wanaojitambua kama kimei,jk,rostam,majaliwa na wananchi ambao wasije kutesa watoto kama baba zetu waliokataa kununua mjini dar leo tupo nje matako ya mji
 
Nilipoona rostam aziz anauza hisa voda nikajua hilo chaka halifai tena
Walionunua sijui walipigwa na upofu gan tena waliingia dse kwa kulazimishwa😀😀😀
Yaani huu ulikuwa mkenge mmoja matata sana. Hakunaga gawio hata 100 ningejua milioni 3 yangu ningekunywa windoki tu. Dustbin.

Ova
Hamna mkuu mbona wanatoaga gawio shng 7 kwa hisa
 
Yaani huu ulikuwa mkenge mmoja matata sana. Hakunaga gawio hata 100 ningejua milioni 3 yangu ningekunywa windoki tu. Dustbin.

Ova
Mimi nilidhani ni mimi peke yangu sipati gawio kumbe tuko wengi. Sasa fedha zetu walizotunyang'anya wamezipeleka wapi?

Afadhali wewe hizo 3 mimi zilikuwa nyingi kweli baada ya kutafakari na kuona kampuni ilikuwa inafanya business nzuri, kumbe ni utapeli mtupu. Nilitaka kuziuza pia nikaambiwa haziuziki kwa hivyo nimeganda nazo tu.
 
Vod
Yaani huu ulikuwa mkenge mmoja matata sana. Hakunaga gawio hata 100 ningejua milioni 3 yangu ningekunywa windoki tu. Dustbin.

Ova
Vodacom gawio wanatoa ila ni kidogo sana aisee...nenda karekebishe taarifa zako za benki upate kiwango chako
 
Kwenye uwekezaji kuingia chaka ni kitu cha kutegemea has ukiwekeza bila kufanya utafiti mzuri. Sehemu sahihi au salama ni UTT au kwenye govt securities, japo huko returns ni ndogo. Kama unafuata "the higher the risk the higher the returns" ujue ni risk ipi uko tayari kuipokea.
Mimi nilikosea kwenye precision air nikaja nikakosea tena kwenye vodacom.
Ndio maisha lakini
 
Back
Top Bottom