Katika hali inayoonyesha hali ngumu ya kiuchumi, Mahanga amwangukia Msemakweli

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740

Katika hali inayoonyesha hali ngumu ya kiuchumi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga ameamua kujisalimisha na kumwangukia Kainerugaba Msemakweli ili amsamehe deni analomdai.

Hata hivyo Msemakweli amesema hawezi kumsamehe Mahanga kutokana na kwamba ameshatumia gharama katika kesi yake hivyo lazima alipwe fedha zake.

Mahanga anatakiwa kumlipa Msemakweli jumla ya Sh11, 097,000, na anatakiwa kulipa Sh2 milioni kila mwezi kwenye akaunti ya

Msemakweli na kisha kuwasilisha mahakamani risiti ya malipo, hadi deni hilo litakapomalizika.

Deni hilo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli katika kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na Mahanga dhidi yake baada ya kumtaja katika kitabu chake cha Orodha ya Mafisadi Sugu wa Elimu kuwa ni mmoja wa vigogo wenye shahada za Udaktari wa Falsafa za kughushi.

Chanzo: mwananchi.co.tz
 
Ngoja ntaongea na msemakweli maana ni mtu wangu wa karibu sana.....jana nlikuwa naye ssehemu fulani tumekaa filóloga moja moto moja baridi msema kweli aliniacha hii sana baada ya kuniambia kuwa anataka mfungulia kesi basht kama yeye.....na nimjuavyo Jamaa atafanya kweli

Ova
 
Katika hali inayoonyesha hali ngumu ya kiuchumi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Maendeleo ya Vijana, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga ameamua kujisalimisha na kumwangukia Kainerugaba Msemakweli ili amsamehe deni analomdai.

Hata hivyo Msemakweli amesema hawezi kumsamehe Mahanga kutokana na kwamba ameshatumia gharama katika kesi yake hivyo lazima alipwe fedha zake.

Mahanga anatakiwa kumlipa Msemakweli jumla ya Sh11, 097,000, na anatakiwa kulipa Sh2 milioni kila mwezi kwenye akaunti ya

Msemakweli na kisha kuwasilisha mahakamani risiti ya malipo, hadi deni hilo litakapomalizika.

Deni hilo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli katika kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na Mahanga dhidi yake baada ya kumtaja katika kitabu chake cha Orodha ya Mafisadi Sugu wa Elimu kuwa ni mmoja wa vigogo wenye shahada za Udaktari wa Falsafa za kughushi.

Chanzo: mwananchi.co.tz
Aandike kitabu kingine kuna wasukuma wawili wenye degree fake na phd fake
 
Duh!! Leo hii umekuwa mdogo kweliii unaomba msamahaa kabisa kilichobaki upige goti umsujudie msemakweli tuuu au makamanda wamekukachaaa??????
 
ha ha ha... kwa maana hiyo ni kweli phd yake ni ya kughushi???? maana alishindwa kesi. kaazi kweli kweli.
 
Hivi si kuna mafusadi wengine wa elimu aliwataja, nakumbuka kuna mmoja wa darasa la saba kama sikosei vile, huyu naye alidai atakwenda mahakamani sijui kama alitimiza azma yake hiyo!
 
Jamaa huyu ndio alisema watu wanajiuliza, kwanini nimekaa unaibu miaka kumi na wala sijapandishwa...
 
Kwan msema kweli ni nan hasa MSAADA PLZ
Msemakweli ni Mwandishi wa kitabu cha watu wenye vyeti vya kughushi na.wameshika madaraka makubwa. Aliwataja wengi akina Marry Nagu, Kamala , Nchimbi n.k.akiwemo Mahanga wakati wa uongozi wa JK..Mahanga hakifurahishwa na kitabu hicho akaenda mahakamani kudai haki kwa kuchafuliwa jina. Msemakweli akshinda kesi na kufungua kesi ya kudai gharama za kesi. Nafikiri hizi Mahanga ndo anahangaika kumalizana na Msemakweli ambaye amekataa. Kwahiyo story ndo hiyo. Watuhumiwa wengine walipuuza kitabu chake ndo maana hawana mgogoro naye.
 
Kwa usawa huu wa msemakweli ni mpenzi wa Mungu mbona atauza hadi vikombe vya chai
 
Back
Top Bottom