Mathias
Senior Member
- Apr 22, 2009
- 118
- 12
Huu ni upuuzi na ujinga wa kupitiliza, hizi sherehe za miaka 50 ya uhuru kwanini tuongelee mafanikio? Ingekuwa jambo la busara kuongelea changamoto na wapi tumeshindwa na tufanyeje kwa miaka 20-50 ijayo. Hii tabia ya kutaka kusifiwa niya kijinga naniya viongozi wasiopenda kuwajibika. Kama serikali imejenga barabara hakuna maana ya kuongea manake wananchi wataona na kusema, kama kuna maji yanayotoka bombani 24/7 kwanini uongee na kuomba kusifiwa wakati hali halisi inaonekana? Tuache sifa zisizokuwa na msaada. Hakuna kiongozi yoyote anayestaili sifa, manake ni wajibu wake kutekeleza na aliomba kazi ya kuwatumikia wananchi kwa hiari yake mwenyewe, sasa akifanya alichoomba anaitaji sifa za nini? Wananchi tunalipa kodi kwa Serikali ili watimize wajibu wao kwetu, kwanini viongozi hawawasifii wananchi kila siku kwa kulipa kodi na wao wanazitafuna bila mpango?