Elections 2010 Katibu wa CCM Jijini Mwanza alishwa sumu

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Kuna taarifa za kuwa Katibu wa CCM kata ya Isamilo ambako katibu wake aliuawa kwa kuchoma kisu na Meya wa Jiji Bihondo akakamatwa kwa mauaji, amelishwa sumu na sasa yupo mahututi Bugando kwa matibabu, katibu huyu nimeambiwa anaitwa Emma Chacha na tukio limetoka majira ya saa 1:45 usiku.

Bado nafuatilia zaidi
 
Tukiwaambia hameni huko hicho ni chama cha majasusi kina wenyewe hamtaki shauri yenu na bado.
 
Tunasubiri Taarifa lazima Hii ni laana toka kwa Allah (God) Nakwambia dhambi za kula nchi peke yao ndio zinawatokea puani Ua kabisa hao:cheer2:
 
Ameanza kutibiwa, lakini hali yake ni mabaya, na imebainika kuwa allikunywa sumu hiyo katika bia maana baada ya kula aliamua kunywa moja moja moto kusukumia msosi, ila taarifa zinaeleza kuwa baa aliyokula chakula na kunywa Kinyaji hicho ni mali ya mmoja wa waliogombea udiwani akashindwa katika kula za maoni na alikuwa akipingana na mgombea udiwani aliyeshinda ambaye katibu huyo alikuwa mtu wake. Polisi pia wameanza kazi.
 
Nimeingia kwa kasi kwenye hii thread nikidhania ni yule katibu Mkuu mwenye Kamba! get well soon katibu na karibu huku kwa wapinga ufisadi
 
Pamoja na uadui katika sera na majigambo lakini TU WAMOJA KITAIFA NA KIZALENDO
waliofanya tukio hilo wanapaswa kuchukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wenye nia kama hizo.
Ila nawashauri wanaccm makini waachane na hicho chama kisha waje huku nyikani tutafakari namna ya kuikomboa Tanzania yetu kutoka kwa wakoloni baba na ndugu zetu.
 
Kweli hivi vinafasi vya uongozi ni vitamu kiasi cha kutaka kumtoa mwenzio maisha! CCM TENA!!!!!! Kuna nini huko? Mungu atamjalia hatokufa na atakapokuwa amepona, inabidi amlete mwenzie mbele za watu, amuulize ndugu yangu kwani ulitaka kuniua ili nini, miaka 5 ya kuitwa mheshimiwa tu, haya chukua uheshimiwa! Hatothubutu! Ataambuliwa kifungo na taabu tu kwa ujinga wa kitoto
 
Makamba inasemekana kuwa alibaka mtoto wa shule.

Huyu Sumu alijipa mwenyewe na ndiyo akafuzwa mwalimu mkuu shule wa msingi..........

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa vigogo wa CCM hawana ubavu wa kumnyooshea kidole kuhusu maisha yake binafsi.

Akihutubia wananchi katika mji wa Babati, mkoani Manyara, Dk. Slaa alisema iwapo wataendelea kuacha masuala ya kitaifa na kujihusisha na maisha yake binafsi, naye atawavaa na kuwavua nguo mmoja baada ya mwingine, kwani anawajua.

Na kwa kuanzia, alimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, awaeleze Watanzania kwa nini alifukuzwa ualimu wa shule ya msingi.

Dk. Slaa alisema yeye hakufukuzwa upadri, kama Makamba anavyodai; bali aliamua kuacha kwa kufuata sheria za kanisa, na akapewa kibali kutoka Vatican kinachomruhusu kuwa mlei na kuoa.

Alisema iwapo Makamba atadanganya wananchi kuhusu kilichosababisha afukuzwe ualimu, Dk. Slaa atamuumbua. Wajuzi wa mambo wanajua kuwa Makamba alifukuzwa ualimu (mkuu) wa shule kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mtoto wa shule.Source: Ansbert Ngurumo blog
Nimeingia kwa kasi kwenye hii thread nikidhania ni yule katibu Mkuu mwenye Kamba! get well soon katibu na karibu huku kwa wapinga ufisadi
 
Get well soon Katibu.
Polisi lazima uchunguzi ufanywe na aliyefanya hili afikishwe mkwenye mkono wa haki!! lol!!
 
Kwa nini wanachezeana rafu? Kwa nini wasikubali kuwa karne hii kuna kushinda na kushindwa?? too sad!!
 
Back
Top Bottom