Tairi bovu
JF-Expert Member
- Sep 28, 2017
- 3,063
- 2,983
Nilifuatilia kwa kina mazungumzo yako na ndugu Tido Mhando hapo jana kupitia Azam tv hakika umedanganya na kujichanganya sana. inatia shaka hata kukuita dr. hasa ikizingatiwa kwamba wewe ni mwalimu wangu najisikia vibaya
1. Uliulizwa juu ya kusimamishwa shughuli za kisiasa ambazo zipo kisheria. ukasema zinaruhusiwa kwa wabunge na viongozi kwenye maeneo yao nawewe unafanya kwasababu unatembelea wanachama nchi nzima kwakuwa ni mpya. Sawa, mbona Maalim Seif ni mwanachama mpya wa ACT amekatazwa kufanya hivyo? mbona mashinji haruhusiwi kufanya kama ufanyavyo wewe? mbona makene haruhusiwi polepole anaruhusiwa?
2. Uliulizwa kuhusu hamahama ya wabunge kuja ccm na kwann wanagombea maeneo yaleyale na kwamba ndio utaratibu wa chama? Ukajibu kwamba ndio utaratibu na kwamba hakuna haja ya kura za maoni. Ukatolea mfano jimbo la Korogwe kwamba alichukuliwa watatu. Ulisema wanaomba kwanza kujiunga na chama kwenye matawi. Sio kweli hata kidogo. Ushahidi upo kwamba mh GEKULI na yule wa Serengeti hata maudhui ya barua zao yalishabihiana pakubwa waliomba uanachama wapi, lini na walikubaliwa wapi na lini na wakajiunga na chama lini?
3. Uliulizwa kuhusu Lowassa kurudi CCM. Ukajibu kwamba aliomba kupitia kwenye tawi huko Monduli na mlimkubalia kupitia vikao vya chama na wakati wa kujiunga alisindikizwa na mwandani wake bwana Rostam Azizi. Ukweli ni kwamba Lowassa alijiunga na CCM kwanza na kadi alienda kuchukua baadae kule Monduli ushahidi upo
4. Uliulizwa juu ya dhamira ya kupambana na rushwa na kwannini ripoti ya tume yako imekuwa siri kama ya maiti na kaburi. ukadai uliwasilisha kwenye vikao vya chama kwa masaa manne na dk 20. Ukweli ni kwa mapendekezo ya ile tume hayajawahi kutekelezwa popote na kwamba chama chako hakina nia ya dhati ya kupambana na rushwa nakupa mfano.. kwenye uchaguzi wa marudio kule Ukonga wapiga kura walipewa kati ya 100000 na 20000 ili wasipige kura wewe ulikuwepo na uliona hilo lipo wazi kabisa. Kinondoni watu walikimbia mpaka na mabox tena askari uliona na kushuhudia.
5. Uliulizwa kuhusu kuongeza muda wa kutawala kwa magufuli na msimamo wako ukajibu kuwa hataongeza muda .. ukweli ni kwamba Juma Nkamia sio mjinga na hajaamka na kuota alitumwa na mwenyekiti na baada ya kuona haiwezekani akaondoa hoja mezani.
6.uliulizwa juu ya wabunge machachari wanaoenda kinyume na misimamo ya chama wakitajwa kina nape, ukasema kwakuwa hawajapitia kwenye vyuo vya chama. wewe ulipita chuo gani cha chama ndugu Bashiru? mbona hujamtaja bwana polepole anayewatukana mpaka wabunge wenzie wa upinzani? anasema wamepatikana kwa kutoa ngono? mbona husemi Anna kilango malecela na anna Abdalla kutaja wachache walipatikanaje?
Hitimisho:
Nitaendelea kuamini kwamba serikali ya CCM ndiyo inayohusika na jaribio la kumuua Mh. Tundu Lissu na bunge ni dhaifu kwa viwango vyovyote vile... tangu lini mtu msafi akaogopa kukaguliwa?