Katiba: Saa 72 za matumaini au huzuni kwa watanzania

wana Jf

napenda kupata tofauti kati ya CCM,TLP na CUF katika suala la mswada wa katiba mpya !!! maana mimi sioni tofauti katika fikra na mitazamo yao,leo TLP,
CUF wameshindwa kabisa kuonyesha wapo upande gani upinzani au CCM B,C

Best Regards

Job seeker
 
Tofauti ya CCM na CUF ni jinsia, CCM ni ME na CUF ni KE na wamekuwa mwili mmoja baada ya ile ndoa yao. CCM na TLP tofauti yao ni njaa tu, TLP ambayo ni Mrema pekee njaa ni kali na afya ni gogoro bila magamba ile sukari itamuua yule mzee, hata umwambie alambe viatu vya JK atakubali.
 
Ahsante sana Maggid kwa uchambuzi wa maana sana. Ni matuamiani yetu kuwa mswaada utapita kwa kura nyingi za ndiyo kama ilivyo desuturi yao hao wabunge wetu. Pamoja na matarajio hayo naomba kupitia kwako niwakumbushe hawa wabunge wetu waliowengi hapo bungeni kuwa maamuzi yao katika utayarishaji wa katiba mpya yanatengeneza UZIMA au KIFO cha nchi yetu.

Kwa sababu pia bunge letu limejengwa katika imani ya uwepo wa MWENYEZI mungu, kila asubuhi wabunge umuomba Mungu awajalie BUSARA; NAMUOMBA MUNGU ASIWANYIME BUSARA HIZO SIKU WANAPOPITISHA MUSWADA HUU:
 
Monday, November 14, 2011, 6:00

  • Wanaharakati wageuka mbogo,watoa onyo kali
  • Watishia kuitisha maandamano yasiyo na kikomo
  • Ni endapo Muswada wa Katiba utasomwa leo
  • Wasema hakuna polisi, mgambo atakayewauzia
Na Otilia Paulinus
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mjadala wa Katiba uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, alisema njia pekee ya kuepusha maandamano hayo ni Serikali kusoma Muswada huo kwa mara ya kwanza na si mara ya pili kama ambavyo imekwishatangaza.

"Napenda kuwaambia ndugu washiriki kama kesho (leo), Serikali itasoma Muswada huu kwa mara ya pili, tutaitisha maandamano ya nchi nzima yasiyokuwa na kikomo.
"Tarehe na siku tutawaambia muda si mrefu, tunataka kuona muswada huu unasomwa kwa mara ya kwanza ili Watanzania wapate fursa ya kuujadili,"alisema Kibamba na kupigiwa makofi.

Alisema Jukwaa la Katiba litaongoza maandamano hayo, ambayo lengo lake ni kupinga jeuri ya Serikali.

"Inasikitisha kuona viongozi wa Tanzania ni waoga mno, nawahakikishia kwamba maandamano ya katiba yatatisha, hatuogopi polisi, mgambo wala wanasiasa watakaozuia dhamira yetu,"alisema Kibamba.

Wakichangia kongamano hilo kwa nyakati tofauti, wanaharakati na washiriki wa mjadala huo, walisema viongozi hawajifunzi wala kuonyesha uzalendo, zaidi ya kujadili posho na marupurupu, huku wakishindwa kuwatetea wananchi.

"Wabunge waache kushabikia Serikali ya kikoloni, tunataka waitetee Tanzania, sisi ndio tunaowapa mamlaka ya kwenda mjengoni (bungeni), kama kesho (leo) watausoma Muswada huu kwa mara ya pili, tutadai haki yetu barabarani bila kuogopa chochote,

"Tutakapofanya maandamano hatutahitaji polisi, zile bunduki na mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, wakawapigie mafisadi ambao wanatumia fedha za walipa kodi kwa maslahi yao,"alisema Paulina Makuli.

Naye Renatus Pamba, alisema wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), unatia wasiwasi kwani huenda kukawa na kura nyingi za kutaka kupitisha Muswada huo usomwe mara ya pili kwa maslahi binafsi.

Alisema kamwe hawataogopa kudai haki yao, kwani miaka 50 ya kuburuzwa na hali ngumu ya maisha imefikia kikomo.

"Tunawashangaa sana hawa viongozi wetu, mbona wanapokuja kuomba kura hawatwambii sisi walemavu tusiwapigie, ndiyo kwanza wanakusogeza karibu na kukuonyesha majina ya viongozi na vyama vyao, kwa nini wakati wa kuandika Muswada huu hawakutuwekea mazingira rafiki katika usomaji, au sisi siyo Watanzania, "alihoji mmoja wa wanaharakati hao, Maria Charles.

…Tunawaomba viongozi wetu watutambue makundi maalum katika uandishi wa muswada huo kwa kutumia nukta nundu ili na sisi pia tuweze kusoma bila kuhitaji msaada wa mtu yeyote,"alisema

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba mpya, unatarajiwa kusomwa kwa mara ya pili na tatu bungeni leo huku wananchi na wanaharakati wakizidi kuupinga.

Naipenda Tz,

Asante sana.
Kimsingi KATIBA ni kama nyumba yetu sote tunayotaka kuijenga. Tunngependa idumu hata kwa miaka 200 ijayo. Hivyo, hakuna sababu ya kugombania fito. Kuchagua nani achangie fito na nani asichangie ni ubaguzi. Ni dhambi.
Iringa

Back
Top Bottom