Katiba mpya ya Kenya na uchaguzi wa Machi 4

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Katika mfululizo wa makala zetu juu ya uchaguzi mkuu nchini Kenya,tunamulika katiba mpya ya Kenya na namna ilivyobadilisha utaratibu wa uchaguzi ujao, ikilinganishwa na chaguzi za hapo nyuma.

Moja ya nguzo kuu za mabadiliko ya kisiasa nchini Kenya ni katiba mpya iliyoidhinishwa rasmi Agosti 27 mwaka wa 2010. Na tangu hapo unapozungumza na wakenya mara kwa mara utawasikia wakielezea haki zao na kunukulu katiba yao mpya kwa majivuno..kwamba hili na hili limewezekana kutokana na katiba mpya.

Katiba mpya ya Kenya ni matokeo ya juhudi za wakenya, waliotumia muda wao mwingi kutoa maoni katika rasimu ambayo hatimaye ilipigiwa kura, kukubalika na kuandikwa na wataalam.

Mojawapo ya mabadiliko makubwa katika siasa za Kenya yaliyotokana na katiba hiyo ni utaratibu wa uchaguzi mkuu. Hapo awali uchaguzi huo ulihusu rais na wabunge. Lakini ifikapo Machi 4, wakenya watachagua wawakilishi sita. Kuna rais, wabunge, magavana, maseneta na wengine wengi.

Patrick Ochieng ni mkereketwa wa haki na demokrasia nchini Kenya na pia mkurugenzi mtendaji wa shirika la kitaifa la Ujamaa. Anasema , “katiba imeleta utaratibu mpya kwenye uongozi na kwenye uchaguzi.” Kutokana na mabadiliko hayo kutakuwa na serikali kuu, na pia serikali ya ugatuzi na uwakilishi kwenye mabaraza 47 ya Kenya.
 
Back
Top Bottom