Katiba Mpya na Nguvu ya Rais: Ya Kuachwa, Ya Kudhibitiwa na Ya Kuondolewa...

Chichanga,

Asante kwa mchango wako katika bandiko namba 68. Umezungumza masuala mengi ya msingi. Nilichoelewa ni kwamba tujaribu kufikiria Urais kama ni Kiti, sio Mtu, huku tukiweka jitiaha katika maeneo mawili makuu- kwanza kuhakikisha kwamba tunapata mtu anayefaa, lakini pili, kujiandaa kuwa na mtu ambae hatopendwa na pande zote za jamii, assuming kwamba hili litatokana na juhudi zake za kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa, sio familia, marafii zake au wafanyabiashara na wageni kwa nia ya kujilimbikizia ten percent. Kama nimekosea katiak kukuelewa, naomba unirekebishe.

Nikija kwenye hoja yangu ambayo ndio ya msingi, unasema kwamba nanukuu:
rai yangu,madaraka ya rais yabaki kama yalivyo katika yale mambo ya msingi sana kwa nchi yetu.

Kwa maana nyingine hapa, unajadili kwamba – "power in the right hands is good and indeed necessary for a young state like Tanzania." Katika mjadala wa awali uliohusiana na hoja ya Balozi Sefue kwamba kuondoa madaraka ya rais ni hatari kwa usalama, amani na mshikamano wa taifa letu, tulijadili sana suala hili lakini zaidi kwa kujikita zaidi katika mjadaka wa Muktadha (Context) ambayo madaraka ya rais yanahitajika kutumika. Kulikuwa na pande mbili za hoja – upande mmoja ukijadili kwamba Tanzania kama Taifa bado ni change hivyo tunahitaji kumwachia Rais madaraka mengi Kikatiba ili afanye kazi yake kama head of state and government kwa ufanisi zaidi; Upande wa pili wa hoja ulipingana na hili kwa hoja kwamba – hatuna good experience na nguvu hii ya rais kikatiba kwani imekuwa abused, lakini pia kwamba pamoja na umuhimu wa hoja ya kuacha nguvu za rais kikatiba zibaki kama zilivyo, its too risky kuacha katiba impe nguvu rais kwa matumaini kwamba siku moja tutapata rais anayefanani ana Nyerere;

Kundi hili la hoja pia lilijenga hoja kwamba Tanzania sio Taifa Changa kwani tumekuwa huru kwa miaka zaidi ya hamsini na wenzetu ambao walipata uhuru miaka ya sitini kama south korea, Singapore n.k, wamepiga hatua kubwa, kwahiyo tusitumie uchanga wa taifa kama kisingizio kwanini hatujasonga mbele. Katika moja ya majibu yangu, nilieleza juu y aumuhimu wa kutofautisha baina ya STATE na GOVERNMENT, kwamba ni kweli tumekomaa katika kuunda GOVERNMENTS lakini katika kuunda STATE, bado tupo wachanga kwani 1961 – 1966, tulikuwa a PARTY STATE, tukaona haifai, hivyo 1967 – 1985 tukawa a DEVELOPMENTAL STATE, nayo ikaonekana kwamba haifai, hivyo tangia 1986 hadi sasa, tumekuwa a CONTRACTING STATE kwa maana ya kwamba the state has been contracting huku market ikiwa ina expand na kuchukua sehemu kubwa ya uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Katika kujibu hoja kuhusu jinsi gani mifano ya nchi kama Singapore na sisi sio mizuri, nilisema kwamba weneztu walipanga na kuchagua na kuwa consistent na walichochagua kwa miaka zaidi ya hamsini sasa, kwahiyo ni sahihikusema kwamba wamekomaa as STATES, lakini sisi kama nilivyojadili hapo juu, tumekuwa ni watu wa kufanya majaribio as a STATE i.e. 1961 – 1966 a PARTY STATE, 1967 – 1985 a DEVELOPMENTAL STATE na 1986 hadi sasa (2013), a CONTRACTING STATE.

Ukitazama kwa makini, ingawa Katiba yetu leo inasema sisi ni Taifa la kijamaa kiuchumi na kijamii, as a STATE, tumekuwa chini ya mfumo wa kibepari na soko huria kwa muda mrefu kuliko mfumo wa Ujamaa i.e. Mfumo wa ubepari 1961 to 1966 PLUS 1986 to 2013 ni jumla ya miaka 32, huku Ujamaa ikiwa ni miaka kumi na nane tu i.e. 1967 – 1985. Ni katika hili nimekuwa nasubiria majibu ya swali la jingalafalsafa kwa wachangiaji kule kwamba je, as a state, tumekomaa katika kipi?

Nikirudi kwenye quote yako hapo juu kwamba
rai yangu,madaraka ya rais yabaki kama yalivyo katika yale mambo ya msingi sana kwa nchi yetu.
Nadhani tutanufaika zaidi na mjadala huu kuhusu content za kuacha na kupunguza iwapo tutazingatia muktadha husika, sio kwa mazingira ya nyumbani tu bali mfumo mzima wa kimataifa wa ubepari pamoja na dunia ya sasa ya utandawazi.

Mwisho ningependa kusikia kwa undani ni masual again ambayo kwa mtazamo wako ni ya msingi na hivyo katika Katiba Mpya, yabakie chini ya mamlaka ya Rais kama ilivyo chini ya Katiba ya sasa (ya 1977).


Cc: nguruvi3, EMT, kichuguu, jingalafalsafa, jounegwalu, bongolander, Raia Fulani, Jasusi, JokaKuu…
 
Mwanafalsafa1,

Nashukuru kwa mchango wako kuhusiana na bandiko namba 73; Kimsingi, suala la checks and balance bainay a bunge na taasisi ya urais, nakubaliana na wewe mia kwa mia; Lakini tatizo langu linakuja katika pracvticalities zake na ningependa kujadili hilo kwa mara nyingine tena (nilijadili huko nyuma sijapata comments), huku nikiunganisha na hoja yako muhimu sana kuhusiana na mfano wa marekani na institutions zake ndani ya demokrasia;

Hapo awali, nilijadili kwamba kimsingi ni muhimu sana kuweka checks and balance kupitia separation of powers katika 3 pillars of the state ambazo ni bunge, mahakama, na executive, kwani nje ya hii, hakuna njia nyingine ambayo imekuwa proven effective duniani, tukiachana na nchi kama China ambayo ni mjadala tofauti, hasa unaohitaji to take into account of nuclear warheads kama deterrent, massive population and massive investments in S&T; anyways, tuachane na wachina kwa sasa.

Nikirudi kwenye hoja yangu - pamoja na umuhimu wa ku apply in practice dhana ya separation of powers, nika hoji kwamba je – to we have watumishi wenye competence na integrity katikam ahakama na bunge wa kusimama masuala mazito ambayo kwa sasa yapo chini ya mamlaka ya Rais? Kwa mfano ukitazama aina ya majaji ambao wamekuwa wanateuliwa, wengi ni useless kabisa when it comes to suala zima la competence na Tundu Lissu amelijadili hili kwa kirefu; Kibaya ni kwamba, hawa ndio watakuja kuwa Majaji wakuu, majaji kiongozi, na ma JR huko mbeleni chini ya katiba mpya; Je tutafika kweli bila ya kurekebisha tatizo hili kwanza na kuzuia majuto huko mbeleni? Nilijadili pia sifa za wabunge kwa mujibu wa katiba, sifa nyingi hazitusaidii kupata wabunge wa maana na wenye competence and integrity kwani kwanza wanachohitaji ni elimu ya darsa la saba kuwa wabunge, umri wa miaka 21, na pia hakuan sheria ambayo inawazuia kuingia bila rushwa, ndio maana hata kama ushindani unazaa wabunge wasomi n.k, suala la competence and integrity kwa bunge linaendelea kuwa ni tatizo kubwa.

Ndio maana hoja yangu has always been kwamba – pamoja na umuhimu wa kuanza kuzipa meno mihimili ya bunge na mahakama ili kujenga dhana ya separation of powers kwa manufaa ya taoifa letu, ni muhimu tukalitazama suala hili in a holistic way, badala ya sasa ambapo tunalitazama in an atomistic way; Hakika bila uangalifu kitakachofuata ni majuto.

Nimalizie na hoja uliyojenga kupitia mifano ya marekani na formal institutions; Katika hili, nakubaliana na wewe, umejadili mambo muhimu na ya msingi sana; Tatizo letu Tanzania tunakimbilia to catch up na wengine huku tukiwa ni jamii ambayo ipo more loyal to informal and community based institutions (udini, ukabila n.k) katika kuendesha nchi, badala ya kuwa loyal on formal and civic institutions of the state. Viongozi wetu hawazaliwi na formal and civic institutions bali informal and community institutions, iwe ni wabunge, madiwani na hata marais; Kwa mfano rahisi – wewe kama mgombea udiwani, ubunge au urais, usipowekeza katika informal and community based institutions kama makanisa, dini, makabila, makundi Fulani ya wazee, you will not make it to the political office, kwani kuwekeza katika institutions ambazo ni more formal and civic haitakusaidia. Mwalimu alifanya kazi kubwa sana kujaribu kujenga taifa letu, kujenga, udugu, umoja, na mshikamano lakini alisahau kitu kimoja – he never turned former colonized people into Citizens first. Na mpaka kesho, masuala kama haya yataendelea kupelekea point yako hapo juu kwamba: “taasisi zetu hazija koma…. Kwa wenzetu mfano Marekani political culture yao imekua sehemu ya formal institutions zao ila kwetu sisi bado formal institution zetu hazi reflect our political culture”
 
Nguruvi3,

Asante sana kwa mchango wako bandiko namba 71; Ni kweli kwamba kuna tatizo kubwa linalotokana na suala zima la usimamizi wa mchakato wa Katiba Mpya, na hii ni sababu moja wapo ambayo imekatisha sana watanzania wengi matumaini, na hata mwenzetu Mzee Mwanakijiji anaumia sana na hili kiasi cha kukosa nguvu hata kujiunga nasi humu; Binafsi naungana na machungu haya miongoni mwa wengi lakini nadhani uchungu utakuwa mkubwa zaidi iwapo wahusika wataendelea kuamini kwamba watanzania wamelala na hawaelewi kinachoendelea na kwamba hata katika vijiwe vyetu vya kuchezea drafti na bao, hatuna uwezo wa kuzungumzia mapungufu yao kama watawala; Hili ni jambo ambalo we need to prove them wrong na ndio moja ya nia kuu za mijadala kama hii; Ni muhimu historia ije kutuona kwamba ingawa sisi tulikuwa ni Dagaa tu katika mfumo mzima na watu ambao hatukuwa na influence ya kubadilisha lolote kwa manufaa ya vizazi vijavyo, lakini ni muhimu watawala wajue kwamba hata tukiwa Dagaa na wao Mapapa na Manyangumi, hata Dagaa pia wanajua kuogelea kama Papa na Nyangumi, na ni muhimu vivazi vyetu vijavyo vikaja kuona hili – kwamba miongno mwa mapapa na manyangumi, pia walikuwepo dagaa waliokuwa na upeo na uelewa juu ya mfumo mzima wa nmaisha ndani ya bahari husika!

Nikianza na hoja zako za sehemu “A” kuhusu nguvu zipi zibaki kama zilivyo, suala la Kwanza ulilojadili ni la Rais kuwa Head of State na Head of Government; Kimsingi nakubaliana na hoja yako katika hili ingawa kuna mapungufu machache of which I want to comment as follows:

As we speak, Rais tuliyenae ni Executive President as he is the head of State and Government, per 1977 constitution; Kwa mujibu wa article number 37 ya katiba, the president is to run the government in his own wisdom without being bound by any one’s advice. Haitaji to consult mtu yoyote au kuchukua ushauri wa mtu yoyote unless Katiba imtake afanye hivyo. Kiini macho kinachofuatia hapa ni kwamba - chini ya sub- article (3) ya article (54), vyombo vya juu kabisa vya kumshauri Rais ni Baraza la Mawaziri; Rais huyu huyu ni mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lakini sio mjumbe wa Baraza la Mawaziri. Kwa maana hii, hes not bound to Cabinet’s advice per se;

Nikiingia kwenye hoja yako nyingine katika sehemu “A” – nakubaliana na mtazamo wako na wa Shivji na kwa kweli naendelea kushangaa sana kwanini mtaalaum kama huyu – wakili wa masuala ya Katiba kutoka Camrbidge University na mmoja ya wataalam wa masuala haya bara la Afrika ameachwa katika tume hii. Hii ni ishara kwamba mchakato mzima wa Katiba Mpya unahusisha watu ambao wangekuwa very critical (constructively) kwa manufaa ya Taifa; As you rightly put it, hoja ya Shivji itaendelea kuwa relevant kwa kipindi kirefu sana hadi pale nchi itakapo pata uongozi wenye Vision, hasa ambayo ni home grown and formed from the bottom – up (not top – bottom) kama hii ya sasa. Na katika hili, nimekuwa nahoji je, katiba iseme nini kuhusiana na mfumo wetu wa kiuchumi na kijamii ili Rais wa nchi aweze kuendesha nchi kwa dira inayoeleweka na kukubalika na walio wengi as head of state and government? Je, iwe ni Ujamaa? Ubepari? Kwa sababu nizizojua, sijapata maoni kutoka kwa mchangiaji yoyote juu ya hili. Pia kwa mtazamo wako nguruvi3, unadhani hatuwezi ku deal na hoja ya Shivji kuhusiana na umuhimu wa watanzania kuamua wanataka taifa la namna gani kupitia mchakato wa Katiba mpya?

Nikija kwenye hoja yako ya Pili katika kipengele hiki hiki “A” kuhusiana na nguvu zipi za Rais kikatiba ziachwe kama yalivyo chini ya katiba mpya, ni suala la Amiri Jeshi Mkuu vis a vis mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Ni sahihi kabisa kwamba haya ni mambo mawili tofauti, at least kwa uelewa wangu. Pia kimsingi nakubaliana na wewe kwamba kuwamchia Rais kuhodhi masuala haya kwa pamoja ni hatari kwa taifa, hasa itakapotokea nchi inapata rais mwehu au anayepandikizwa na wenye fedha au majajusi kutoka nje ili awatumikie wao badala ya wananchi, kwani you never know, especially given the fact kwamba a new type of Cold War is on the Rise; Lakini nilikuwa naomba kusikia mawazo yako katika hili: Je, Katiba iweke devices gani ambazo zitazuia uasi au mazingira ambayo wenye fedha au external agents za kijasusi zinaweza kuteka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa matakwa yao? Hakika uwepo wa sheria peke yake ndani ya katiba haitoshi;

Nikija kwenye sehemu “B” kuhusiana na nguvu zipi ziachwe lakini kwa kudhibitiwa, nakuunga mkono katika yote uliyoeleza, kwani mimi pia nina mtazamo kama huo. Lakini nina tatizwa kidogo na suala la bunge kupewa madaraka makubwa sana huku katiba ikiwa haijengi mazingira ya kuwa na bunge lenye uzalendo, integrity and competency, among other things, kama nilivyojadili hapo awali; Nini mtazamo wako katika suala hili? Na je, unadhani kuna umuhimu wa kuwa na two houses in the parliament kama house of commons and house of lords in the west minster system? Kwani kama sijakosea, (per mjadala wa balozi Sefue), wewe pia unapendelea tuwe na mfumo wa presidential, na sio parliamentary; Actually hata humu, kwa hoja yako juu ya umuhimu wa kumwacha Rais kuwa head of state and government bila ya udhibiti wowote, it means unaegemea kwenye presidential form of governance than parliamentary; Swali linalofuatia ni je - tukiwa na mfumo presidential, yet tukalipa bunge nguvu kama hizi as a substitute kwa mamlaka ya Rais maana yake tunaingia katika mfumo ambao ni semi – presidential; Sina tatizo na hili per se lakini we have to choose what we really want – Presidential au hybrid between the two, huku tukielewa faida na hasara zake;

Nikirudi kwenye hoja yangu kuhusu two houses within the parliament, nia hapa ni kuhakikisha kwamba parliamentary form of governance ambayo inherently leads to instability in governments (mfano Japan) lakini more government accountability, basi angalau tuhakikishe kwamba tunapata angalau reasonable stability katika mazingira yenye bunge lenye meno makali; Njia moja wapo kwa mtazamo wangu ni kuweka kikatiba kanuni ya special majority au absolute majority badala ya simple majority katika ku approve mapendekezo ya Rais, kuyatengua au kuiadhibu serikali isiyowajibika; Hii itasaidia serikali kuwa accountable, yet kuwa stable kwani ili suala lipite katika bunge, litahitaji nguvu kubwa ya hoja kushawishi wengi; ni mtazamo wangu tu lakini, I might be wrong on this one;

Kuhusiana na suala la ardhi, kimsingi nakubaliana na hoja yako, lakini pia ukipata muda naomba upitie mchango wangu juu ya hili kwenye bandiko langu namba 80 ambalo ilikuwa ni majibu yangu kwa muchetz.

Sehemu C ya bandiko lako linahusiana na hoja juu ya nguvu zipi ziondolewe kabisa kutoka kwenye mamlaka ya Rais na kuhamishiwa kwingine; nakubaliana nawe katika mengi juu ya hili, actually almost mstari kwa mstari; Na hoja yako kuhusu mahakama, hasa jinsi gani Jaji Mkuu apatikane, na jinsi tawi hili la utawala lijiendeshe bila kuingiliwa ni hoja ya msingi sana; Kwa kuongezea tu kidogo katika hili, inasikitisha sana kuona jinsi gani Serikali kupitia Wizara ya Sheria na Katiba imekuwa bado inaendesha tawi hili la utawala kama vile ni idara ya Serikali, kwani inaiachia uhuru kwa mkono wa kushoto, lakini uhuru unakabwa kwa mkono wa kulia, hasa kupitia suala zima la bajeti ambapo maamuzi hufanywa na Serikali bila ya kushirikisha the judiciary kikamilifu katika maamuzi na vipaumbele vya judiciary;

Madhara yake ni pamoja na ukosefu wa haki kwa wananchi kwani moja ya sababu zinazofanya kesi nyingi zichelewe kutolewa maamuzi ni ukosefu wa fedha na vifaa, pia hakuna morale na motivation miongoni mwa watumishi wa mahakama, tofauti na reforms ambazo zimegeuza bunge kutoka hali yake ya zamani; Watumishi wa mahakama wanaishia kuwa corrupt, na wanakosa hamasa ya kuwa wabunifu hasa in terms of application of Information and Communication Technologies kuhusiana na masuala ya court registry na e-justice kwa ujumla wake kwani modernization ya aina yoyote inahitaji resources; Modernization hii per mtazamo wa mahakama (sio wizara ya sheria) ingeweza kuongeza efficiency and effectiveness ya judiciary system kwa ujumla wake. True autonomy ya tawi hili la utawala ndio njia pekee ya kutatua changamoto hizi pamoja nyingine kama ulivyojadili.

Naelewa hoja yako juu ya ugumu wa kujibu maswali yangu namba 4 & 5 katika bandiko namba moja kwa maelezo uliyotoa, na kimsingi nakubaliana na wewe; Lakini pia maswali yale yanaweza bakia kama angalizo tu;

Mwisho ningependa kunukuu hoja yako ifuatavo:

Kwa bahati mbaya sana tupo katika trap! Rais akaamua kujifungia mahali na kuandika mawazo yake na washirika wake, yakapelekwa bungeni ambako ulikuwa ni mhuri wa Rais yule yule aliyefanya madudu hayo, ikaundwa tume ya katiba tukaambiwa tutoe maoni tena tukizuiwa tusijadili mengine bila kujua tunataka kwenda wapi, kwa njia gani na kwa nini.

Kwa hoja hii, executive powers za rais as ahead of state and government zinahitaji kurekebishwa au kudhibitiwa lakini nukuu yako nyingine inapingana na hili, pale uliposema kwamba:

Nguvu gani abaki nazo Rais:

Mkuu wa state na government.

Matatizo uliyojadili kuhusiana na mchakato wa kupata katiba mpya yanatokana na nguvu ya Rais as head of state and government kama ilivyo chini ya Katiba ya sasa, nguvu ambazo unashauri ziachwe bila kuguswa i.e. head of state and head of government; Naona mgongano wa hoja zako mbili hapa, unless ni mimi ndio sijakuelewa vizuri. Vinginevyo nimejadili kidogo hoja hii kule juu nilipkuwa najadili sehemu “A”, hasa kwenye mjadala unaohusu nguvu za rais as a head of state and government per article 37 na article 54 (4) kwa mujibu wa Katiba ya 1977.
 
Niseme nimedandia hoja; hata hivyo nitajituma kujibu kwa undani nitakapopata nafasi

Nionavyo mimi na pengine wewe utakumbuka usemi ulioelezea utawala wa Mkapa kuwa ni wa kibabe. Kila mtu alikuwa na maana yake ndani ya kauli ya ubabe wa Mkapa.

Maoni yangu ni kuwa

1. Mkapa aliingia madarakani kwa nguvu ya Mwl. Nyerere. Seriously sioni kama alikuwa chagua la wananchi; kwa sababu nguvu ya chama dola ilikuwa bado imeshamiri na upinzani ulielezwa au ulipewa sura ya watu wanaopinga mema ya nchi ni wakuogopwa.

2. State Vs Government Ni bahati mbaya hakuna defined line katika katiba na katika utawala wa siku hadi siku. Mkapa alitumia hilo akajikwaa sana kwenye suala la uchaguzi wa 2000 kwa kuawa wan CUF 79. Akajikwaa vibaya zaidi kwenye ubinafsishaji kwa sababu ya kushindwa kwa kusudio na kukosekana kwa waathirika kudai fidia kwa maumivu hayo. Mfano wafanyakazi wa General Tyre Arusha na wengine

Kifupi mimi silaumu nipo pamoja na wengine tunaojaribu kutoa maoni yetu. La msingi Katiba yetu hususan kwa upande wa "content" za urais zina mapungufu sana. Ndiyo maana(sababu) awamu zote nne za urais zinajitofautisha sana kulingana na wajihi na nafsi zao, utadhani hawa marais wametoka kwenye sayari tofauti. In a nutshell pamoja na aina ya utawala na uongozi wa kiurais wenye utata; cha msingi tumewapata marais ambao kila moja kaja na lake, Nyerere na Azimio la Arusha, Mwinyi na Azimio la Zanzibar, Mkapa na ubinfsishaji JK dhaifu na FastJet. Inaonekana Katiba yetu kwenye urais ina matatizo.

Nakubaliana na hoja zako kimsingi; na kuhusiana na eneo la kijani hapo juu - tatizo lipo hapo kwani inayonyesha kwamba tatizo sio katiba yetu bali watu, ingawa haina maana kwamba tusibadili katiba iliyopo; Mwanafalsafa mmoja kutoka India (Dr. Ambedkar) alipata kunena yafuatayo:

"However good or bad a Constitution may be, it is sure to turn out BAD because those who are called to work it happen to be a bad lot; however Bad a Constitution may be, it may turon out to be good if those who are called to work on it happen to be a good lot; The working of the Constitution does not wholly depend on the nature of the Constituion; The Constitutions can provide only the organ of the STATE such as the Legislature, the Executive and the Judiciary; The factors on which the working of these organs of the State dpend are the people and the political parties..."

Dr. Ambedkar pia anasema hivi:

"The Constitution is after all, some kind of a legal body given to the ways of Governments and the life of a people. A Constitution if it is out of touch with the people's life, aims, and aspirations, becomes rather empty, if it falls behind those aims, it drags the people down. It should be something ahead to keep people's eyes and minds up to a certain high mark";

Pia President of India's Constituent Assembly alipata kunena kwamba:

"After all, the Constitution like a machine is a lifeless thing. It acquires life because of the man who control and operate it; And India needs today nothing more than a set of honest men who will have the interest of the country before them."

Hizi ni nukuu muhimu sana za kujifunza kutoka kwa wenzetu ambazo sio Tume ya Katiba, Jukwaa na Katiba au mtanzania yoyote mwenye influence katika mchakato husika amepata kufanyia utafiti na kuelimisha watanzania; Pengine baada ya kuziweka humu, kama wahusika watapita pita humu na kusoma michango yetu ya vijiweni, pengine wataweza kuzisoma na kupata msukumo wa kufanya utafiti zaidi au kuchukau maneno haya kwa copy and paste fashion na kwenda kutamba nazo kwenye vyombo vya habari kama vile wao ndio watunzi; Lakini muhimu kwetu ni kwamba ujumbe wa namna hii ufikie watanzania walio wengi;


cc:
EMT, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Zakumi, Bongolander, AshaDii, Kichuguu, jouneGwalu, Jasusi, JokaKuu, MTAZAMO, Mwita Maranya, Dingswayo, Mkiliman, tubadilike-sasa, Bobuk, muchetz, Getstart, Ivonya-Ngia, Mgaya Kimweri, CHIGANGA, JingalaFalsafa Rutashubanyuma, Ogah, Mag3, Raia Fulani, Mkandara;
 
Mkuu Mchambuzi.....
Prof Shivji ameuliza swali moja muhimu sana ambalo hatuhitaji kulikwepa. Amesema, tunaandika katiba, je, ni lini tulikaa tukamua aina ya taifa tunalopaswa kuwa?[/CENTER]
[/LIST]
​​

Asante Mkuu Nguruvi3. Tena limetumika neno sahihi kabisa, yaani je, ni aina gani ya Taifa TUNALOPASWA kuwa, na sio TUNALOTAKA! Kwa maana tunaweza kutaka kuwa wafugaji, wakati nyenzo/facilities zetu zote kwa ujumla ni za uvuvi. KUTAKA kunaweza kusukumwa na HULKA ZETU, lakini KUPASWA halihusishi maamuzi bila MANTIKI. Yaani hata kama mwanadada anapenda kuvaa nguo nyepesi za wazi na anataka aonekane hivyo kila wakati, lakini kwa USALAMA WAKE ANAPASWA KUVAA KOTI NA NGUO NZITO AKIWA MAKAMBAKO. Tena wakati mwingine KUPASWA hakuamuliwi, ila kutafakariwa na kufuatwa tu. MANTIKI ipo siku zote, ni kuitafakari na kuiweka wazi na watu watapaswa kuifuata kwa ustawi wao!
Binafsi ninaamini wazi kuwa "HAKUNA DIRA YA TAIFA, BASI HAKUNA HATUA YOYOTE MBELE" na kila matatizo yanayotukabiri leo hii misingi yake imo humo kwenye swala la DIRA YA TAIFA/IMANI KUU YA WATANZANIA, ni wazi kabisa hata suluhisho lake lipo humo. "UNYONGE WETU UPO 'COZ WE HAVE NO OUR OWN BELIEF TO PROUD OF" "mtoto akivaa shati jipya, kama hajiamini akichekwa na wenzake atabadilishana na kuukuu lililotoboka, na hatoacha kupigwa na baridi"
Tunaandika katiba. Je, ni lini tulikaa chini na kutafakari na kugundua ni taifa la aina gani TUNALOPASWA KUWA? Kadri tunavyolikwepa swali hili, ndivyo tunavyozidi kuwaongezea maumivu watoto wetu!
DIRA YA TAIFA ni IMANI KUU YA TAIFA juu ya kila kitu chao. Tukumbuke pia kuwa, DIRA NDIYO INAYOUNDA KATIBA, KATIBA IPO KURASIMISHA DIRA, DIRA HUZAA MIFUMO, MIFUMO HUZA SERA, SERA ZINAPORASIMISHWA HUITWA SHERIA/KATIBA.
Mkuu Mchambuzi, kamwe mzoga uliooza hauwezi kutoa kimfaacho mtu kula! MATUMAINI YA MMEA HUJENGWA KWANZA NA SEHEMU ULIKOTOKEA, je ni mwambani ama udongoni.
Mungu wetu anaita sasa.
 
Mkuu Mchambuzi, ahsante sana kwa jinsi unavyo ''attack'' hoja kwa mantiki. Nitarejea kujadili yale ya bandiko #83
 
Nakubaliana na wewe.Sio kila uwakilishi unatakiwa bungeni.Hii inafanya vyama vingi vya kijamii kuendeshwa kisiasa kwakuwa vinakuwa dominated na the so called wawakilishi wao bungeni.Lakini pia wabunge ni wawakilishi wa watu wote(sio wasio na ulemavu pekee).Kwahiyo kama mbunge hawakilishi maslahi ya matabaka mbalimbali ya jamii yote hilo ni tatizo binafsi la mbunge.

Kuweka uwakilishi maalum bungeni ni kuridhika na kukubaliana kuwa mbunge anawakilisha wasio maalum pekee!Kitu ambacho sio kweli,kama mbunge hawakilishi jamii yote hafai kuwa bungeni.
Ntakubaliana nawe ikiwa huko kwenye asasi za jamii nako watachaguana na sio kuteua. Nasisitiza hapa pasiwe na mbunge wa KUTEULIWA bali ACHAGULIWE kwa kura.
 
Mchambuzi;5606396]Nguruvi3, Na katika hili, nimekuwa nahoji je, katiba iseme nini kuhusiana na mfumo wetu wa kiuchumi na kijamii ili Rais wa nchi aweze kuendesha nchi kwa dira inayoeleweka na kukubalika na walio wengi as head of state and government? Je, iwe ni Ujamaa? Ubepari? Kwa sababu nizizojua, sijapata maoni kutoka kwa mchangiaji yoyote juu ya hili. Pia kwa mtazamo wako nguruvi3, unadhani hatuwezi ku deal na hoja ya Shivji kuhusiana na umuhimu wa watanzania kuamua wanataka taifa la namna gani kupitia mchakato wa Katiba mpya?
Makosa yalifanyika tangu mwanzo na ni makosa yale yale yaliyoplekea Kenya kuwa katika mzozo wa kuandika katiba mpya kwa muda mrefu.Tofauti na sisi wenzetu walikomaa ili wapate kitu
wanachokitaka.

Mchambuzi, ni kweli rais ana madaraka ya executive lakini madaraka hayo anapaswa ayatumie kwa njia zinazokubalika na jamii.
Jamii iliamua kuwa ni wakati sasa tuwe na katiba mpya. Rais alipaswa kusimamia mchakato wa katiba kwa kuhakikisha kuwa utulivu na fursa zinapatikana kwa kila mmoja.

Alipaswa akutane kwanza na wasomi, wataalamu na wawakilishi wa makundi ya jamii kupata maoni ni vipi tuandike katiba, thamani zipi za taifa ziangaliwe na tunataka kuwa taifa la namna gani.

Baada ya hapo ndipo tulitakiwa tuwe na majadiliano ya kitaifa kwanza kwa mambo muhimu. Hapa ndipo katiba yetu ingeweza kutamka sisi tunataka kujenga taifa la namna gani, mfano ubepari, ujamaa n.k.
Kisha mchakato uanze kulingana na yale wananchi waliyojadili.

Kinyume chake rais akajifungia Ikulu na watu wachache wakaanda mswada na kwa bahati mbaya ukaplekwa kwa ''wendawazimu Dodoma'' nao kwa sababu ya dhiki na njaa zao wakaupitisha.

Kwamba tunawezaje kutumia fursa ili kuingiza hoja ya Shivji, kwakweli ni too late.
Tumeshaweka mkokoteni mbele ya farasi na tunakwenda vivyo hivyo.

Nilimsikia Rais alipokuwa Ethiopia kuhudhuria mkutano wa utawala bora, nilishtushwa sana na kauli yake kuhusu Tanganyika imara na Zanzibar kupatikana baada ya mchakato. Yaani rais wa JMT tayari amesha rule out kuhusu Utanganyika na Uzanzibar na siyo Tanzania.

Leo wametoa vitambulisho vya taifa. Nimeona hata wale wasiopenda muungano nao wamechukua tena wakiuutukana muungano huo. Hii maana yake ni kuwa tayari rais anajua nini matokeo ya mchakato.

Hapo ndipo nasema kuingiza hoja ya Shivji ni jambo lisilowezekana na likiwezekana ni kiini macho unless uniambie mtazamo mwingienjuu ya hilo.
Pia kimsingi nakubaliana na wewe kwamba kuwamchia Rais kuhodhi masuala haya kwa pamoja ni hatari kwa taifa, hasa itakapotokea nchi inapata rais mwehu au anayepandikizwa na wenye fedha au majajusi kutoka nje ili awatumikie wao badala ya wananchi, kwani you never know, especially given the fact kwamba a new type of Cold War is on the Rise; Lakini nilikuwa naomba kusikia mawazo yako katika hili: Je, Katiba iweke devices gani ambazo zitazuia uasi au mazingira ambayo wenye fedha au external agents za kijasusi zinaweza kuteka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa matakwa yao? Hakika uwepo wa sheria peke yake ndani ya katiba haitoshi;
Kwa hili nadhani njia mojawapo ni kuhakikisha kuwa madaraka yanayohusu usalama na ulinzi wa nchi yasilundukwe kwa mtu mmoja. Sheria ni sehemu tu ya suluhu lakini si suluhu kama ulivyosema.

Kuwepo na mgawanyo kuhusu hilo hata kama rais atapewa ''shea kubwa kidogo''. Wakuu wa vyombo vya usalama wawajibike kwingine na si kwa mtu mmoja. Matahalan, mkuu wa usalama aweze kuhojiwa na bunge na hata kufikishwa mbele ya sheria ikithibitika vinginevyo kama itakavyokuwa kwa viongozi wengine.

Hii itasaidia sana kutokuwa na ''syndicate''. Kwa sasa hivi ni rahisi sana kwasababu kila mmoja anawajibika kwa mtu mmoja na asipokubaliana naye anaweza kujikuta katika matatizo. Bado hatujaweza kutengua kitendawili cha Imran Kombe kwa uchache wa kusema na mfano wa hili kama utanielewa.

Leo kamati ya bunge la Marekani imepewa classified document za drone iliyoangushwa Iran na iliwahi kuomba document za Benghaz kutoka vyombo vya usalama kuangalia nani amebofoa na kwanini. Kwa msingi huo ni ngumu sana kiongozi kutenda nje ya wigo wake. Nadhani we can borrow a leaf
Lakini nina tatizwa kidogo na suala la bunge kupewa madaraka makubwa sana huku katiba ikiwa haijengi mazingira ya kuwa na bunge lenye uzalendo, integrity and competency, among other things, kama nilivyojadili hapo awali; Nini mtazamo wako katika suala hili? Na je, unadhani kuna umuhimu wa kuwa na two houses in the parliament kama house of commons and house of lords in the west minster system? Kwani kama sijakosea, (per mjadala wa balozi Sefue), wewe pia unapendelea tuwe na mfumo wa presidential, na sio parliamentary; Actually hata humu, kwa hoja yako juu ya umuhimu wa kumwacha Rais kuwa head of state and government bila ya udhibiti wowote, it means unaegemea kwenye presidential form of governance than parliamentary; Swali linalofuatia ni je - tukiwa na mfumo presidential, yet tukalipa bunge nguvu kama hizi as a substitute kwa mamlaka ya Rais maana yake tunaingia katika mfumo ambao ni semi – presidential; Sina tatizo na hili per se lakini we have to choose what we really want – Presidential au hybrid between the two, huku tukielewa faida na hasara zake;
Nadhani tuwe na hybrid kwasababu accountability inazaa stability na vyote tuavihitaji.

Kuhusu bunge kuna changamoto sana. Ninachokiona si tatizo la bunge as bunge, tatizo ni lawatu wanaotengeneza bunge.
Hili linaanzia katika vyama na tunapaswa kuliangalia kwa umakini.

Nadhani katiba iwe na kipengele kuwa mbunge hatapoteza ubunge hata kama atafukuzwa na chama, na pia anaweza ku-switch akabaki na ubunge wake.

Mbunge ni mwajiriwa wa wananchi na wao ndio wawe na uwezo wa kumuondoa kwa petition au taratibu nyingine. Maana kubwa hapa ni kuzuia ''woga, hypocrisy na stupid loyality''

I can't agree more with you katika suala la kuwa na two house, upper and lower.
House moja iwe ya makabwela na nyingine iwe ya prominent and respected figures katika society.
Hili litasaidia sana kuwa na bunge lenye maana na kuzuia ujinga wa kuendesha bunge kama kijiwe cha kahawa.

Spika asiwe mbunge au mwanachama wa chama chochote cha kisiasa.
Akitaka kugombea ni lazima kwanza 'denounce'' loyality yake yeyote kwa chama cha kisiasa.
Spika achaguliwe na wabunge na iwe nafasi huru kwa kila mtu.
Hili litatusaidia kuzuia kubambikiziwa''wehu'' kwasababu tu ya majority in the house.

Ruzuku ziondolewe katika vyama ili kuzuia massive corruption.
Kutokana na kuzagaa kwa pesa za ruzuku ubunge umekuwa kama lawalawa unayoweza kununua popote.
Wabunge wajihudumie katika chaguzi na kama vyama vitawasaidia basi ni vyama a si pesa ya kodi ya kila mwananchi.

Sheria ya matumizi wakati wa uchaguzi ukaziwe na ipewe meno. Anayeikiuka ikbainika iwe mwisho wa career katika siasa.
Na pia masurufu ya bunge yaondolewe ili bunge liwe sehemu ya kazi na si sehemu ya kusaka utajiri.

Rekodi za ushiriki ikiwa ni pamoja na upigaji kura ndani ya bunge ziwe kwa kila mbunge mmoja mmoja na si suala la ndiyo au hapana. Hili litatusaidia kupata viongozi kama nilivyoeleza mwisho.

Wabunge wasijihusishe na shughuli za mashirika kama wajumbe wa bodi na wala wasijihusishe na NGOs.
Nikirudi kwenye hoja yangu kuhusu two houses within the parliament, nia hapa ni kuhakikisha kwamba parliamentary form of governance ambayo inherently leads to instability in governments (mfano Japan) lakini more government accountability, basi angalau tuhakikishe kwamba tunapata angalau reasonable stability katika mazingira yenye bunge lenye meno makali; Njia moja wapo kwa mtazamo wangu ni kuweka kikatiba kanuni ya special majority au absolute majority badala ya simple majority katika ku approve mapendekezo ya Rais, kuyatengua au kuiadhibu serikali isiyowajibika; Hii itasaidia serikali kuwa accountable, yet kuwa stable kwani ili suala lipite katika bunge, litahitaji nguvu kubwa ya hoja kushawishi wengi; ni mtazamo wangu tu lakini, I might be wrong on this one;
Nakubalina nawe kanisa. Na ikiwezekana yaanishwe maeneo yanayoweza kuwekewa special majority au hiyo absolute kutoka na umuhimu wake.
Madhara yake ni pamoja na ukosefu wa haki kwa wananchi kwani moja ya sababu zinazofanya kesi nyingi zichelewe kutolewa maamuzi ni ukosefu wa fedha na vifaa, pia hakuna morale na motivation miongoni mwa watumishi wa mahakama, tofauti na reforms ambazo zimegeuza bunge kutoka hali yake ya zamani; Watumishi wa mahakama wanaishia kuwa corrupt, na wanakosa hamasa ya kuwa wabunifu hasa in terms of application of Information and Communication Technologies kuhusiana na masuala ya court registry na e-justice kwa ujumla wake kwani modernization ya aina yoyote inahitaji resources; Modernization hii per mtazamo wa mahakama (sio wizara ya sheria) ingeweza kuongeza efficiency and effectiveness ya judiciary system kwa ujumla wake. True autonomy ya tawi hili la utawala ndio njia pekee ya kutatua changamoto hizi pamoja nyingine kama ulivyojadili.
Mahakama iwe independent kabisa na kuwa na bajeti yake inayotawaliwa na mahakama yenyewe. Nakubaliana sana

Tatizo la viongozi wetu ni kuweka masilahi yao mbele zaidi ya vizazi vijavyo. Sijui ni viongozi wangapi wa nchi hii wanaweza kueleza kama ''state'' wapi tulipo na wapi tunaelekea.

Mchambuzi mi nadhani kuna haja ya kuwa na vetting nzuri ya viongozi.
Tunahitaji kupata kiongozi si kwa kupenedekezwa tu bali kumfahamu kuhusu ushiriki, misimamo, maono na mitazamo yake kisiasa kuanzia miaka mingi.Hili litatuepusha kupata kiongozi kwa ''kuuziwa mbuzi katika gunia''
 
Ili kufanya mjadala wetu uwe na manufaa zaidi kutakuwa na tija zaidi iwapo tutajadili content juu ya nguvu za Rais kwa mujibu wa Katiba kwa kuelekeza focus ya mjadala katika masuala yafuatayo:


  1. Katika Katiba Mpya, Ni Mamlaka/Nguvu zipi za Rais ziachwe kama zilivyo ndani ya Katiba ya sasa (1977) na bila ya kudhibitiwa? Kwa hoja gani?
  2. Katika Katiba Mpya, Mamlaka/Nguvu zipi za Rais ziachwe kama zilivyo ndani ya Katiba ya sasa (1977) lakini zisiachwe bila ya Kudhibitiwa? Zidhibitiwe na taasisi (chombo/vyombo) gani? Kwa hoja gani?
  3. Katika Katiba Mpya, Mamlaka/Nguvu zipi za Rais ndani ya Katiba ya sasa (1977) ziondolewe kabisa kutoka kwa Rais? Zipelekwe kwenye taasisi gani? Kwa hoja gani?
  4. Kwa muda mrefu sasa, nchi inayumba kutokana na ukosefu wa Dira inayotambulika rasmi kwa mujibu wa Katiba ya nchi (both in Precept/Principle and Practice), kwani on the one hand, by precept, Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa Kijamaa, lakini on the other hand, in practice Tanzania ni nchi inayo practice ubepari na soko huria kwa muda mrefu zaidi kuliko Mfumo wa Ujamaa. Je, Katiba Mpya itamke Taifa la Tanzania linafuata mfumo gani wa Kiuchumi na Kijamii ili Rais wa nchi aweze kuongoza kwa mujibu wa Dira na Mfumo unaotambulika rasmi kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi?
  5. Mwisho, ili Taifa liweze ku-balance baina ya uwepo wa government stability na government accountability, ambapo government stability ni zao la Presidential form of government huku government accountability ikiwa ni zao la Parliamentary form of government, Je – Katiba Mpya itamke Tanzania inafuata what form of governance between the two? Kwa hoja gani?

Sijui kama nitakuwa nje ya madhumuni ya huu mjadala, lakini nadhani suala kubwa siyo Rais kuwa na madaraka makubwa au madogo.

Kwa maoni yangu, suala kubwa ni checks and balances. Kama kuna checks and balances suala la Rais kuwa na madaraka makubwa linakuwa irrelevant.

Kuhusu suala la kuwa na parlimentary au presidential system, sidhani kama litakuwa na manufaa hasa ukiangalia jinsi bunge la sasa linavyofanywa kuwa rubber stamp ya maamuzi mengi ya serikali.

Yanayondelea bungeni hivi sasa ni kielelezo tosha kabisa kuwa hatuna bunge ambalo ni supreme katika kufanya shughuli zake.
 
[/LIST]

Sijui kama nitakuwa nje ya madhumuni ya huu mjadala, lakini nadhani suala kubwa siyo Rais kuwa na madaraka makubwa au madogo.

Kwa maoni yangu, suala kubwa ni checks and balances. Kama kuna checks and balances suala la Rais kuwa na madaraka makubwa linakuwa irrelevant.

Kuhusu suala la kuwa na parlimentary au presidential system, sidhani kama litakuwa na manufaa hasa ukiangalia jinsi bunge la sasa linavyofanywa kuwa rubber stamp ya maamuzi mengi ya serikali.

Yanayondelea bungeni hivi sasa ni kielelezo tosha kabisa kuwa hatuna bunge ambalo ni supreme katika kufanya shughuli zake.

Ndio maana hata mimi nimekuwa na wasiwasi wangu kuhusu quality ya vyombo ambavyo tutavitumia for checks and balance kwani again, sioni mahakama na bunge vikiwa na watumishi ambao ni competent, patriotic na wenye integrity, if we are not careful hali itakuwa ni ya vurugu zaidi kuliko sasa kwani nguvu itakuwa kama imesambazwa kwa wenda wazimu wengi zaidi;
 
Kwa ujinga wa utovu wa ukomavu wa kisiasa Tanzania yetu hatuja komaa kumpa raisi mamlaka kubwa bali mamlaka hii inatakiwa kugawanywa kwa miimili stahiki kuileta haki.
topcombofr.jpg

Madhumini ya uzi huu ni kuendeleza mjadala wa awali uliotokana na hoja ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue kwamba kupunguza madaraka ya Rais ni hatari kwa amani, utulivu, na mshikamano wetu kama Taifa. Mjadala huo unapatikana katika uzi ufuatao: Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Kwa bahati mbaya (au pengine nzuri), katika mjadala juu ya hoja ya Balozi Sefue, hatukupata nafasi ya kujadili kwa kina kuhusu Yaliyomo katika madaraka Ya Rais (CONTENT) kwa mujibu wa Katiba ya sasa, badala yake tulitumia muda mwingi sana kujadili Mazingira/Muktadha Wa Matumizi Ya Madaraka Ya Rais (CONTEXT), mjadala ambao bado unaendelea kule hivi sasa kupitia uzi huo hapo juu. Kutokana na umuhimu wa Content ambayo hatukuipa uzito unaostahili, nimeonelea kwamba itakuwa ni busara zaidi iwapo tutaanzisha mjadala tofauti unaolenga zaidi CONTENT kwenye uzi mpya ili tupate nafasi to exhaust Content Related Issues kama tulivyofanikiwa to exhaust Context Related Issues, katika mjadala kuhusiana na hoja ya Balozi Sefue.

Nimefanikiwa kuja na CONTENT Juu ya Madaraka ya Rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya JMT (1977) katika maendeo KUMI kama ifuatavyo:

KWANZA, Rais ni head of &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];STATE' and Head of &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];GOVERNMENT'. Kwenye Mjadala wa awali tuliona jinsi gani dhana ya STATE na GOVERNMENT zilivyokuwa tofauti.

PILI, Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.

TATU, Rais ni Sehemu ya Mhimili wa Bunge la JMT:

  • Lakini hapo hapo, ana mamlaka ya kuteua wabunge kumi kwa jinsi anavyopenda.
  • Under certain circumstances, anaweza kulivunja Bunge kabla halijamaliza muda wake.
  • Muhimu pia ni kwamba, hakuna muswada wowote ambao unaweza kupitishwa na Bunge na kuwa Sheria ya Nchi bila ya maamuzi ya Rais.
NNE, Rais ana full authority to declare wars and make peace.

TANO, Rais ana nguvu/mamlaka ya kumweka mtu yeyote kizuizini bila ya kumfikisha kwanza mahakamani iwapo kwa hisia zake, kufanya hivyo kutakuwa ni kwa manufaa ya kulinda Amani na Utulivu nchini. Hii ni kwa mujibu wa Preventive Detention Act (1962) na Deportation Ordinance (1921).

SITA, under the Society Ordinance (1954), Rais is empowered in his/her absolute discretion, kupiga marufuku au kufunga shughuli za NGOs au Voluntary Societies zozote ambazo anahisi zipo incompatible na utunzaji wa Amani na Utulivu nchini.

SABA, Rais ana mamlaka ya kutaifisha mali yoyote and vest it in the government.

NANE, chini ya Sheria ya Magazeti (1976), Waziri wa Habari ambae anawajibika moja kwa moja kwa Rais, ana mamlaka ya kufungia au kuzuia uchapishaji wa Gazeti lolote nchini iwapo atahisi kwamba kufanya hivyo ni kwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];faida ya umma' au ni kwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];faida ya amani na utulivu' nchini.

TISA, Rais anateua jina la Waziri Mkuu; anateua Mawaziri, Naibu Mawaziri; Mabalozi; Makatibu Wakuu; Manaibu Makatibu Wakuu; Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Majaji (including Jaji Mkuu); Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama (Polisi, JWTZ, JKT, Magereza, Usalama wa Taifa); Watendaji Wakuu Wa Taasisi zote nyeti za umma (kama vile Benki Kuu, NEC, Msajili wa Vyama Vya Siasa, CAG, Takukuru, DCI, DPP..); Watendaji wakuu wa Mashirika na Taasisi Zote Za Umma pamoja na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi; Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya; Na

KUMI, Rais is the Ultimate Owner of Land/Ardhi yote ya Tanzania ipo chini ya mamlaka ya Rais, wengine wote ni wapangaji na Rais ana uwezo wa kubadilisha umiliki au matumizi ya eneo lolote la ardhi Tanzania.

Vigezo hivi kumi vinamfanya Rais wa Tanzania kuwa ni: The Giver and Taker of LIFE, LIBERTY and LIVELIHOOD in Tanzania. Pia Katiba ya sasa inamlinda Rais mstaafu dhidi ya mashtaka na madai ya aina yote ambayo yanahusiana na shughuli zake wakati alipokuwa Rais wa nchi. Hali hii inamfanya Rais wa Tanzania kuwa ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Imperial President, na ilipelekea hata Mwalimu Nyerere kutamka wakati fulani huko nyuma katika mahojiano na BBC kwamba:

"I have sufficient powers under the constitution to be a Dictator."

Lakini ni dhahiri kwamba Mwalimu hakuwa Dictator Per Se kwani ingawa not always, Nyerere alitumia zaidi His Popularity kuliko Constitutional Powers to get things done, and there is no doubt kwamba Nyerere was a popular leader ambae hajapata kutokea tena Tanzania.

Ili kufanya mjadala wetu uwe na manufaa zaidi kutakuwa na tija zaidi iwapo tutajadili content juu ya nguvu za Rais kwa mujibu wa Katiba kwa kuelekeza focus ya mjadala katika masuala yafuatayo:


  1. Katika Katiba Mpya, Ni Mamlaka/Nguvu zipi za Rais ziachwe kama zilivyo ndani ya Katiba ya sasa (1977) na bila ya kudhibitiwa? Kwa hoja gani?
  2. Katika Katiba Mpya, Mamlaka/Nguvu zipi za Rais ziachwe kama zilivyo ndani ya Katiba ya sasa (1977) lakini zisiachwe bila ya Kudhibitiwa? Zidhibitiwe na taasisi (chombo/vyombo) gani? Kwa hoja gani?
  3. Katika Katiba Mpya, Mamlaka/Nguvu zipi za Rais ndani ya Katiba ya sasa (1977) ziondolewe kabisa kutoka kwa Rais? Zipelekwe kwenye taasisi gani? Kwa hoja gani?
  4. Kwa muda mrefu sasa, nchi inayumba kutokana na ukosefu wa Dira inayotambulika rasmi kwa mujibu wa Katiba ya nchi (both in Precept/Principle and Practice), kwani on the one hand, by precept, Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa Kijamaa, lakini on the other hand, in practice Tanzania ni nchi inayo practice ubepari na soko huria kwa muda mrefu zaidi kuliko Mfumo wa Ujamaa. Je, Katiba Mpya itamke Taifa la Tanzania linafuata mfumo gani wa Kiuchumi na Kijamii ili Rais wa nchi aweze kuongoza kwa mujibu wa Dira na Mfumo unaotambulika rasmi kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi?
  5. Mwisho, ili Taifa liweze ku-balance baina ya uwepo wa government stability na government accountability, ambapo government stability ni zao la Presidential form of government huku government accountability ikiwa ni zao la Parliamentary form of government, Je &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Katiba Mpya itamke Tanzania inafuata what form of governance between the two? Kwa hoja gani?

Karibuni katika mjadala, pamoja tujenge Taifa letu.

----------------------------------------------------------------------------------

cc: EMT, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Zakumi, Bongolander, AshaDii, Kichuguu, jouneGwalu, Jasusi, JokaKuu, MTAZAMO, Mwita Maranya, Dingswayo, Mkiliman, tubadilike-sasa, Bobuk, muchetz, Getstart, Nguruvi3, Ivonya-Ngia, Mgaya Kimweri, CHIGANGA, JingalaFalsafa Rutashubanyuma, Ogah, Mag3, Raia Fulani, Mkandara;
 
Mijadala ya namna hii ilikuwepo kabla JF haijavamiwa na wachangiaji wa kulipwa ambao hawaandiki kwa kutumia akili zao bali mapenzi ya mioyo yao. Wako radhi kuita nyeusi kuwa nyeupe.
 
Back
Top Bottom