Katiba mpya na malipo ya uzeeni - TUCTA mpo

Wa Mjengoni

JF-Expert Member
May 4, 2010
480
128
TUCTA tusaidieni hili liwekwe wazi kwenye katiba mpya kwa faida ya sasa na hata miaka hamsini ijayo.
Jambo lenyewe linahusu kwamba fedha tunazochangia kwenye mifuko mbalimbali ya akiba kwa kuwa haziwekewi riba (na kama ipo ni ndogo sana) basi michango hii iwe inapokelewa na mifuko hiyo ikiwa tayari converted in USD na mara utakapoacha kazi au kustaafu na wewe ulipwe in USD. Nasema hivi kwa sababu shilingi yetu inaporomoka kila mwaka katika kasi ya ajabu, sasa hii inakula kwa mfanyakazi, malipo say yanayoweza kununua gari la biashara mwaka huu ningestaafu au kuacha kazi, unastukia baada ya miaka kadhaa ya kuendelea kazini yanarudi na kutosha kuanzisha genge la nyanya yaani unaenda mbele kwa kurudi kinyumenyume!
Mzee Nico Mgaya tunakuaminia kupigania maslahi yetu. TUCTA juu!
icon6.png
 
Back
Top Bottom