Mtu wa Mungu
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 444
- 19
Kwa Watanzani wenye mapenzi mema na nchi hii, habari kwamba rais Kikwete amekubali kuandikwa katiba mpya, hizi ni habari njema!!!
Ila, kama ana utashi wa kweli wa kisiasa juu ya jambo hili muhimu sana, na la kihistoria kwa yeye binafsi na taifa hili, asiachie mchakato kusimamiwa na serikali yake; mashaka yangu, na huenda ya wengi ni kwamba:-
1) Katika miaka yake mitano ya kwanza imedhihirika kwamba si yeye anayeongoza serikali yake bali kundi la wachache-mafisadi, ambao hawana utaifa ndani yao hata kidogo;
2)Mafisadi hawa, kupitia kwa mmoja wao aliye na nguvu kubwa ya fedha na mtandao mkubwa wa sheria kimataifa hivi majuzi tu amesema kwenye vyombo vya habari kwamba kuandikwa katiba mpya ni kupindua serikali; ni dhahiri kwamba mafisadi hawa watateka mchakato na kuupeleka kwenye mgogoro badala ya kusudio la taifa hili;
3) Chombo pekee chenye uwakilishi wa wananchi wote ni bunge; Katiba ni sheria mama; kama Kikwte ana utashi wa kisiasa juu ya hoja hii, basi kwenye kikao cha bunge cha Februari 8, 2011, waziri wake wa sheria awasilishe msuada wa kuandikwa katiba mpya, na bunge liridhie na kutunga sheria ya kuongoza mchakto wote ikiwa ni pamoja na hadidu za rejea-pamoja na time frame-ndipo sasa kila sekta na jamii nzima iweze kuelewa na kushiriki ipasavyo;
4) Msimamo wa waziri wa sheria Kombani na na mwanasheria mkuu Mrema unapinga dhana nzima ya kuandikwa katiba mpya; kuwakabidhi watu hawa hawa kusimamia mchakato ni kuwadanganya watanzania; kama si kuwahadaa;
5) Katiba Mpya ni Tanzania Mpya!! Katiba ya sasa ya mwaka 1977 (wakati CCM imezaliwa) ni ya chama kimoja cha CCM; kimantiki, CCM hiyo hiyo ambayo tayari imeonesha kuingiwa na tabia ya Taliban ya Afganistan, haiwezi hata kidogo kuongoza mchakato wa kuunda na kupatikana katiba ya kweli-CCM sasa hivi si ile ya 1977 hata kidogo!!!!!!!!!!!!!!!(hata ingekuwa mimi ndiye CCM na serikali yake!!!!!!,yaani watengeneze kisu kikali cha kukata vichwa vyao??????!!!!!!)