Katiba Mpya au Utawala Bora?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Yafuatayo ni maoni yangu yasiyoegemea upande wowote wa kisiasa.

Sura ya Kwanza, Sehemu ya Tatu ya Katiba inahusu Haki na Wajibu Muhimu (Haki ya Usawa, Kuishi, Uhuru wa Mawazo, Kufanya kazi, na Wajibu wa Jamii).

Hivyo ndivyo misingi mikuu ya demokrasia. Isitoshe wananchi huwakilishwa na viongozi waliowachagua kwenye mihimili mikuu ya maamuzi (Bunge na Serikali). Na iwapo Haki na Uhuru utakuwa umeingiliwa, basi Mahakama (Sura ya Tano ya Katiba) ipo kuchukua hatua stahiki.

Kwa nukuu hiyo naamini lengo kuu la wadai Katiba mpya ni kuweka misingi ya kutoa nafasi sawa za kushinda uchaguzi na wala si kudumisha au kupanua wigo wa demokrasia nchini.

Je, Katiba iliyopo (1977) ina mapungufu gani kati suala la demkrasia?
 
Vijana wa siku hizi mpo tayari kugezwa geuzwa kama chapati hamjui kitu.
 
Back
Top Bottom