Elections 2010 Katiba inasema kiti cha Rais kipo wazi

Kabengwe

JF-Expert Member
Oct 20, 2009
240
47
Wadau nilikuwa napitia katiba katika tovuti ya taifa (www.tanzania.go.tz) nimekutana na hiki kipengele ambacho nimekuwa interested kujua zaidi:

38
.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka
masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kufuata masharti ya Katiba hii.
Sheria ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria ya 1994
Na.34 ib.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri
itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;
(b) baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bunge
kwanza:
(c) baada ya Rais kupoteza sifa za kushika nafasi
madaraka ya kuchaguliwa;
(d) baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa
Katiba hii, na kuondolewa katika madaraka;
(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37 ya Katiba hii kwamba Rais hawezi
kumudu kazi na shughuli zake;
(f) baada ya Rais kufariki.
(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tu
ya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu.


Kwa sasa bunge lilishavunjwa, Kwanini JK bado anaitwa Rais wa JMT?!
Au kuna kipengele kingine kinachosema otherwise?!
 
Mhhh! Hii inanifanya nirudi katika pingamizi la Chadema dhidi ya JK. Itamsaidia iwapo Tendwa atasema JK hakuwa 'Rais' wakati anatoa zile ahadi katika hotuba zake kwa hiyo hizo ahadi zichukuliwe kama ahadi tu za mgombea yoyote anazotoa na siyo hongo.

Lakini kama hii ni hivyo, basi JK anaweza kuwa accused na mambo mengi mengine ya kutumia urais wake pamoja na huduma apewazwo Rais kufanya kampeni zake.
 
Mhhh! Hii inanifanya nirudi katika pingamizi la Chadema dhidi ya JK. Itamsaidia iwapo Tendwa atasema JK hakuwa 'Rais' wakati anatoa zile ahadi katika hotuba zake kwa hiyo hizo ahadi zichukuliwe kama ahadi tu za mgombea yoyote anazotoa na siyo hongo.

Lakini kama hii ni hivyo, basi JK anaweza kuwa accused na mambo mengi mengine ya kutumia urais wake pamoja na huduma apewazwo Rais kufanya kampeni zake.

Zile wala si ahadi tupu, ni amri ambazo zinafanyiwakazi tayari na mamlaka husika, eg kupandisha mishahara ya watumishi!
 
Ni kweli kabisa...Chief Justice anapaswa kuendesha nchi pamoja na makatibu wakuu....akina masha sio mawaziri tena kwa vile hawana ubunge.....
 
Ndo kusema hii ni loophole ya CCM kutokea katika pingamizi eeh!!!
 
Zile wala si ahadi tupu, ni amri ambazo zinafanyiwakazi tayari na mamlaka husika, eg kupandisha mishahara ya watumishi!
Alikuwa wapi siku zote hizo i.e. from Dec 2005 asitekeleze ahadi?By the way,maagizo yake si yalikuwa bayana kuwa wafanyakazi hata wakigoma miaka minane hawataongezewa mishahara?
 
Sheria za bongo ziko kama sheria za quantum physics, vitu viwili vyenye mutual exclusivity vinaweza kutokea pamoja. Kiti cha rais kikawa wazi, halafu ukaambiwa Kikwete ni rais. Unarusha sarafu halafu unapata heads and tails simultaneously.
 
Zile wala si ahadi tupu, ni amri ambazo zinafanyiwakazi tayari na mamlaka husika, eg kupandisha mishahara ya watumishi!

Kama ulikuwepo mkulu,

Katika kampeni anazo zitoa JK nia mambo tiali yanafanyiwa kazi ni kuwa tayari yameisha kuwa set up kwa hiyo ni kuzunguka na kusema ila cha ajabu kwanini yawe yanachukua kila baada ya miongo 5?? kunanini hapo? why cant they be done within a short of period?

Na kuinadi ilani ya chama ni kuwa uwe na malengo ya miaka ijayo with marvelous plan ambayo itatekelezeka kwa muda maaaluumu na sio kungojea wakati wa kampeni.

Na hapo sishindwi kuacha kusema kuwa viongozi wetu wengi ni wanyanga'nyi,walaghai wanapola mali za wananchi kwa manufaa yao wanashindwa kuimarisha maendeleo kwa kile tukipatacho kwa maisha ya watanzania na tugawane hicho kilichopo kipatikanacho lakini wananchi hawapati chochote sasa hapo ni uongozi kweli au ni muda wa kuumpa mtu kura na anatunyang'anya haki zetu zote za kimsingi kwa miongo 5.

Mambo yako mengi ni kama CDA na Halmashauli ya Dodoma kushindwa elewana na kuendeleza terrific plan ya mji wa Dodoma kazi kuwachonganisha wananchi na kuingiza siasa katika kuujenga mji wa Dodoma yaaani ni kero tuuupu hapo CCM wanashindwa kuwa wazi kwa wananchi wa Dodoma na wakikaaa hivyo hao ndugu zangu wagogo watabakia kuwa nyuma siku zote kwa kuendekeza siasa za makundi na kujijali wao kwa kizazi hiki badala ya kijacho

 
ERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
RAIS​
Rais wa
Jamhuri
ya Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9​
33​
.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.

Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano na
mamlaka yake
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9​
34​
.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano
katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote
yahusuyo Tanzania Bara.
(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu
utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote
ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
28​
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya
mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia
juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,
yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa
ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu
madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayatahesabiwa kwamba-
(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria
yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au
mamlaka yoyote ambayo si Rais; au
(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya
kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka
yoyote ambayo si Rais.​
Utekelezaji wa
shughuli za
Serikali
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9​
35​
.-(1) Shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri ya
Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya
Rais.
(2) Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni
ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika
kanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katiba
hii.

Mamlaka ya
kuanzisha na
kuwateua watu
wa kushika
nafasi za
madaraka
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 2000
Na.3 ib.6​
36​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na
mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna
mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika
nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za
idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika
kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo
zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali
zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuzi
unaofanywa na Rais.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), masharti
mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria yoyote
inayohusika, mamlaka ya kuwateua watu wengine wote
wasiokuwa viongozi wala watendaji wakuu, kushika nafasi za

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
29​
madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
na pia mamalaka ya kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoa
katika madaraka, kuwafukuza kazi na mamlaka ya kudhibiti
nidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi
mwa Tume za Utumishi na mamlaka mengineyo yaliyotajwa na
kupewa madaraka kuhusu nafasi za madaraka kwa mujibu wa
Katiba hii au kwa mujibu wa sheria yoyote inayohusika.
(4) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayatahesabiwa
kuwa yanamzuia Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya
watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.​
Utekelezaji wa
kazi na shughuli
za
Rais, n.k Sheria
ya 1984 Na.15
ib.9
Sheria ya 1992
Na.4 ib …
Na.20
ib.12,
Sheria yua
1994 Na.34 ib.6​
37​
.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.
(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi
kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili,
laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili
au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio
kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa
mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania,
na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu
kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais
kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba
kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi
itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na
masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha
Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na
shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa
kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama
naye hayupo au ni mgonjwa; basi

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
30​
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya
Muungano.
(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b)
na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Rais
kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia
katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza
kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingine
anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kuteleza
kazi na shughuli za Rais.
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote.
(6) Ifahamike kwamba kiti cha Rais hakitakuwa kiwazi na
Rais hatahesabiwa kwamba hayuko katika Jamhuri ya Muungano
endapo-
(a) atakuwa hayupo katika mji ambao ndio makao makuu
ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano kwa
kipindi cha muda wa saa ishirini na nne; au
(c) atakuwa ni mgonjwa lakini anatumaini kuwa atapata
nafuu baada ya muda si mrefu.
(7) Iwapo kutatokea lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika
ibara ndogo ya (6) na Rais akiona kuwa inafaa kuwakilisha
madaraka yake kwa muda wa jambo hilo, basi aweza kutoa
maagizo kwa maandishi ya kumteua yeyote kati ya watu
waliotajwa katika aya ya (a) au ya (b) za ibara ndogo ya (3) ya
ibara hii kwa ajili ya kutekeleza madaraka ya Rais wakati yeye
hayupo au ni mgonjwa, na mtu huyo atakayeteuliwa atatekeleza
madaraka hayo ya Rais kwa kufuata masharti yoyote
yatakayowekwa na Rais; isipokuwa kwamba masharti yaliyomo
katika ibara hii ndogo yafahamike kuwa hayapunguzi wala
kuathiri uwezo wa Rais alionao kwa mujibu wa sheria nyingine
yoyote wa kuwakilisha madaraka yake kwa mtu mwingine yeyote.
(8) Rais aweza, akiona inafaa kufanya hivyo, kumwagiza kwa
maandishi Waziri yeyote kutekeleza kazi na shughuli zozote za
Rais ambazo Rais atazitaja katika maagizo yake na Waziri
aliyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo,​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
31​
aliyeagizwa hivyo kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo,
atakuwa na mamlaka ya kutekeleza kazi na shughuli hizo kwa
kufuata masharti yoyote yaliyowekwa na Rais, lakini bila ya kujali
masharti ya sheria nyingine yoyote; isipokuwa kwamba-
(a) Rais hatakuwa na mamlaka ya kuwakilisha kwa
Waziri kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo
kazi yoyote ya Rais aliyokabidhiwa na sheria yoyote
inayotokana na masharti ya mkataba wowote uliotiwa
sahihi na Jamhuri ya Muungano iwapo kisheria Rais
haruhusiwi kuwakilisha kazi hiyo kwa mtu mwingine
yoyote;
(b) ifahamike kwamba maagizo yanayotolewa na Rais
kwa mujibu wa masharti ya ibara hii ndogo, ya
kumwagiza Waziri yeyote kutekeleza kazi yoyote ya
Rais, hayatahesabiwa kwamba yanamzuia Rais
kutekeleza kazi hiyo yeye mwenyewe.
(9) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii-
(a) Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanywa kwa ajili
ya kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio kuhusu hali ya
afya ya Rais utahesabiwa kuwa ni mkutano halali
hata kama mjumbe yeyote wa Baraza hilo hayupo au
kiti chake ki wazi, na itahesabiwa kuwa Baraza
limepitisha azimio hilo ikiwa litaungwa mkono kwa
kauli ya wajumbe walio wengi waliohudhuria mkutano
na kupiga kura.
(b) Rais hatahesabiwa kuwa hayupo katika Jamhuri ya
Muungano kwa sababu tu ya kupitia nje ya Tanzania
wakati yuko safarini kutoka sehemu moja ya
Tanzania kwenda sehemu nyingine, au kwa sababu
kwamba ametoa maagizo kwa mujibu wa masharti ya
ibara ndogo ya (7) na maagizo hayo bado
hayajabatilishwa.
(10) Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katika
ibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais, kwa
mujibu wa ibara hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge,
kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake au
kufuta uteuzi wowote uliofanywa na Rais.
(11) Mtu yeyote atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais
kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kama ni Mbunge hatapoteza
kiti chake katika Bunge wala hatapoteza sifa zake za
kuchaguliwa kuwa Mbunge kwa sababu tu ya kutekeleza kazi na
shughuli za Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.​
Uchaguzi wa
Rais Sheria ya
1984 Na.15 ib.9​
38​
.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka
masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
32​
kwa kufuata masharti ya Katiba hii.​
Sheria ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria ya 1994
Na.34 ib.​
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri
itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;
(b) baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bunge
kwanza:
(c) baada ya Rais kupoteza sifa za kushika nafasi
madaraka ya kuchaguliwa;
(d) baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa
Katiba hii, na kuondolewa katika madaraka;
(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37 ya Katiba hii kwamba Rais hawezi
kumudu kazi na shughuli zake;
(f) baada ya Rais kufariki.
(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tu
ya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu.​
Sifa za mtu
kuchaguliwa wa
kuwa Rais
Sheria ya 1992
Na.4
Sheria ya 1994
Na.13 ib…
Sheria ya 1994
Na.34 ib….
Sheria ya 2000
Na.3 ib.7​
39​
.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa

kodi yoyote ya Serikali.
(2) Bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni
yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushiriki
shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote
hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano kama si mwananchama na mgombea
aliyependekezwa na chama cha siasa.​
Haki ya
kuchaguliwa
tena
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria Na.34 ya
1994 ib.9​
40​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena
kushika kiti hicho.
(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika
kiti cha Rais.
(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za
kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Za nzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au
zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.

Utaratibu wa
uchaguzi wa
Rais Sheria
Na.20 ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria Na.34
ya 1994
Na.34 ib.10​
41​
.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine
lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na
inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha
kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea
katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la
mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
ya Makamu wa Rais.
(2) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi
wa Rais yatawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi katika siku na
saa itakayotajwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na
mtu hatakuwa amependekezwa kwa halali isipokuwa tu kama
kupendekezwa kwake kunaungwa mkono na wananchi wapiga
kura kwa idadi na kwa namna itakayotajwa na sheria iliyotungwa
na Bunge.
(3) Endapo inapofika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea
mmoja tu ambaye anapendekezwa kwa halali, Tume itawasilisha
jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au
kumkataa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii na ya sheria

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
34​
iliyotungwa na Bunge.
(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanywa
siku itakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria
iliyotungwa na Bunge.
(5) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa
Rais yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.​
Wakati na muda
wa kushika
madaraka ya
Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9​
42​
.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema
iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa
kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla
ya kupita siku saba.
(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika

ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka
mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.
(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti
hicho atakula kiapo cha Rais; au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;
au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii.
(4) Iwapo Jamhuri ya Muungano inapigana vita dhidi ya adui
na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bunge
laweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wa
miaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii
isipokuwa kwamba muda wowote utakaoongezwa kila mara
hautazidi miezi sita.​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
35​
(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais,
kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine
chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.​
Masharti ya kazi
ya Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9​
43​
.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, na
atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au
posho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo
hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho,
vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii.
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais
havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Madaraka ya
kutangaza vita
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.4 ib.14​
44​
.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa
na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza kuwapo kwa hali
ya vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi yoyote.
(2) Baada ya kutoa tangazo, Rais atapeleka nakala ya
tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya
kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ndani
ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha
mkutano wa Bunge ili kutafakari hali ya mambo na kufikiria
kupitisha au kutopitisha azimio la kuunga mkono tangazo la vita
lililotolewa na Rais.

Uwezo wa
kutoa msamaha
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9​
45​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na
hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza
kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa
masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu
yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa
lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au
asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote
kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
36​
aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au
kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza,
au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia
ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka
utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka
yake kwa mujibu wa ibara hii.
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa
na kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa
Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge
inayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo
yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania
Bara kwa mujibu wa sheria.​
Kinga dhidi ya
mashataka ya
na madai
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
Sheria ya 1992
Na.20 ib…​
46​
.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku
kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake
mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka
yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua
mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa
kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au
baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku
thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais
atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi
kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria
iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo
kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina
lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa
analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais

kwa mujibu wa Katiba hii.
Bunge laweza
kumshtaki Rais
Sheria ya 1992
Na.20 ib.8
Sheria ya 1995
Na.12 ib.4​
46A​
.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-

Sheria ya ….​
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili
yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais
wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja
kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu
kama-
(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku
thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo
inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa
aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati
Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze
mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa
iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa
masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja
kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka
Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya
hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na
kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua
theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara
hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani-
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye
atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
38​
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa
Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa
vinavyowakilishwa Bungeni.
(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum
ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi
na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais
juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa
dhidi yake.
(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi
kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya
Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda
usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa
yake kwa Spika.
(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya
Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata
utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili
taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura
za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote,
Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha
Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.
(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya
Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti
cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika
kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge
lilipopitisha azimio hilo.
(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na
mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata
malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo​
alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na
Bunge.​
39​
Wajibu wa
viongozi wakuu
wa vyombo vya
mamlaka ya
utendaji
kudumisha
Muungano
Sheria ya 1995
Na.12 ib.5​
46B​
.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katika
ibara ya 28 ya Katiba hii, viongozi wakuu wa vyombo vyenye
mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano vilivyotajwa
katika, ibara ya 4 ya Katiba hii, watawajibika, kila mmoja wao
katika kutekeleza madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii
au Katiba ya Zanzibar, 1984, kuhakikisha kuwa analinda
kuimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kila
mmojwawapo wa viongozi wakuu wa vyombo vyenye mamlaka
ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano kabla ya kushika
madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii ataapa kuitetea na
kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya ibara hii:-
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Zanzibar, na

(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
 


Kama ulikuwepo mkulu,

Katika kampeni anazo zitoa JK nia mambo tiali yanafanyiwa kazi ni kuwa tayari yameisha kuwa set up kwa hiyo ni kuzunguka na kusema ila cha ajabu kwanini yawe yanachukua kila baada ya miongo 5?? kunanini hapo? why cant they be done within a short of period?


Naamini Jethro hapo unamaanisha miaka mitano.
 
Ninaomba mdau yeyote anijuze kuhusu:
- lini kikwete alitoa ahadi ya mishahara kwa wafanyakazi na
-nyongeza ya mshahara aliotaja ni kiasi gani

nitashukuru kwa data hizo, sorry kwa kuwa out of topic
 
Wadau nilikuwa napitia katiba katika tovuti ya taifa (www.tanzania.go.tz) nimekutana na hiki kipengele ambacho nimekuwa interested kujua zaidi:

38
.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka
masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kufuata masharti ya Katiba hii.
Sheria ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria ya 1994
Na.34 ib.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri
itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;
(b) baada ya Rais kujiuzulu bila ya kulivunja Bunge
kwanza:
(c) baada ya Rais kupoteza sifa za kushika nafasi
madaraka ya kuchaguliwa;
(d) baada ya Rais kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa
Katiba hii, na kuondolewa katika madaraka;
(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 37 ya Katiba hii kwamba Rais hawezi
kumudu kazi na shughuli zake;
(f) baada ya Rais kufariki.
(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa kiwazi kwa sababu tu
ya Bunge kupitisha hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu.


Kwa sasa bunge lilishavunjwa, Kwanini JK bado anaitwa Rais wa JMT?!
Au kuna kipengele kingine kinachosema otherwise?!
Duh
sasa hapo ndo kasheshe lenyewe
 
Hii katiba yetu imechakachuliwa sana.

Naamini kuna kipengele kinacho kinzana na hiki kwenye hii hii katiba yetu.

Hili ntalifanyia utafiti mpaka nione mwisho wake!
 
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;

"Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii" those are the operating words, ina maana kunaweza kuwepo exception huko zinazosema kiti cha rais hakiwi wazi -kama rais hajafariki- mpaka rais mpya aapishwe.

Unajua hayo masharti mengine yanayoongelewa hapo ni yapi ?
 
Yaani hili likatiba limekaa kishaghalabaghala kweli. Halieleweki hata kwenye mambo yaliyo mepesi. I'm just shaking my head. Hivi kuna ugumu gani kuandika katiba inayoeleweka bila utata wowote?

Mbona Marekani katiba yao inaeleweka bila ubishi wowote kuhusu muda wa raisi wa kukaa madarakani? Sisi kinachotushinda ni nini?

Duli bhalemelwa gete aise!!! (Samahanini imebidi tu niandike kwa Kisukuma hapo)
 
Jana niliona tunakosea hata Kiingereza kwenye katiba, leo tumefikia hatua nyingine kukosea mpaka Kiswahili !

http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977

(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000.)




42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba.

(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais

(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais; au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(4) Iwapo Jamhuri ya Muungano inapigana vita dhidi ya adui na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bunge laweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wa miaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii isipokuwa kwamba muda wowote utakaoongezwa kila mara hautazidi miezi sita.

(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais,kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
 
Back
Top Bottom