Kati ya Mama na Mke nani anastahili zaidi ya 50% ya mapenzi

Ma



Umetembelewa na mamako anakaa siku kadhaa hivi kwako. Anataka kodi ya meza aachiwe yeye apange cha kumunua...ni sawa su si sawa?

Kwa sasa siwezi kujua...
Ila mama yangu hatoweza kuja kufanya hayo...
Sana sana huyo mke mtarajiwa ndiyo atakua anapewa pesa na mama yangu...



Cc: mahondaw
 
Kuna mapenz na upendo
Jukumu la mama ni kukuzaa,kukulea na kukupa malezi bora ili uwe baba bora baadae
Upendo wa mama kwa mtoto mara nying haupungui ila upendo wa mwanaune kwa mkewe unaweza kupungua ila mapenz yakaendelea kuwepo..
Huwez mpenda mama yako kuliko mke wako
Utajidanganya nafsi tu bure na utakua unajilisha upepo..
Mume bora anatengenezwa na mama na baba,na hvyo hvyo mke bora anatengenezwa na familia yake
Mke wako ni namba moja wako,
Msaidizi wako
Mshauri wako
Msiri wako
Mzaz mwenzako
Mla vingi vyako
Mtesi wako
Mfurahia vyako
Mfurahiwa wako

Unataka kujua unampenda nani?
Mwanaume mwngine akitembea na mama yako itakuuma kdgo
Mwanaume mwingine akimtongoza tu mke wako naimani jibu unalo moyoni mwako.

ThtsY,mke ndio anashikilia uhusiano wote wa maisha halisi ya mwanaume...na sio mama.
 
Unajaribu kugawa upendo kama pesa/chungwa! Akili nyingine huwa sizielewi. Kwa nini usiwapende wote 100%?
 
Binadamu ana makundi mhm kadhaa na kimsingi hayo makundi hayatakiwi ku-compete maana itakuwa ni unfair competition

1.wazazi
2.ndugu
3.mke au wake
4.Marafiki na watu unaoshirikiana nao
Kwenye Mambo ya msingi

Sasa ni mpuuzi pekee ndo atawaza Kuweka competition Kati ya

1.Mama aliyemzaa na mke
2.Dada ake tumbo moja na mke
3.Rafiki na mama
4.Mama ake na ndugu

Yaani kifupi hayo makundi Kila kundi hapo linaumuhimu wake kivyake na kwa mda wake..

Huwezi ukaanza kushindanisha parachichi na maharage hata kama unapenda maharage sana inabidi ujue good fats utazipata kwenye parachichi.

Mpuuzi atadhani mama ni muhimu kuliko mke au mke ni muhimu kuliko marafiki au marafiki ni muhimu kuliko ndugu.ila mwerevu anajua baraka nitakazozipata kwa mama siwezi kupata kwa mke na care nitakayopata kwa mke siwezi kupata kwa mama,msaada nitakaopewa na rafiki siwezi kupata kwa mke na changamoto hizi mtu peke wa kuzibeba ni ndugu pekee.

Mjinga akioa anaachana na marafiki wote hata kupokea simu ya ndugu hataki, ana dharau mama ake lakini akipoteza tu kazi ndo anaelewa nina rafiki yangu Sehmu flani,nina ndugu yangu Sehmu flan na kumbe baraka za mama ni mhm...

Mjinga mwingine akioa anadhan Bado yupo single basi anaishi km hana mke, anajali ndugu na kumdharau mkewe,mama kwanza mke ni mtu wa kupita tu hlf akishikwa na stroke hawezi kufanya kazi, marafiki wamekata,ndugu wamechoka kuhudumia ndo anageuka pembeni nakujikuta yupo yeye na mke tu na mke yupo busy kumfulia nguo zake zenye mikojo.

Usiwe mjinga
 
Kuna mapenz na upendo
Jukumu la mama ni kukuzaa,kukulea na kukupa malezi bora ili uwe baba bora baadae
Upendo wa mama kwa mtoto mara nying haupungui ila upendo wa mwanaune kwa mkewe unaweza kupungua ila mapenz yakaendelea kuwepo..
Huwez mpenda mama yako kuliko mke wako
Utajidanganya nafsi tu bure na utakua unajilisha upepo..
Mume bora anatengenezwa na mama na baba,na hvyo hvyo mke bora anatengenezwa na familia yake
Mke wako ni namba moja wako,
Msaidizi wako
Mshauri wako
Msiri wako
Mzaz mwenzako
Mla vingi vyako
Mtesi wako
Mfurahia vyako
Mfurahiwa wako

Unataka kujua unampenda nani?
Mwanaume mwngine akitembea na mama yako itakuuma kdgo
Mwanaume mwingine akimtongoza tu mke wako naimani jibu unalo moyoni mwako.

ThtsY,mke ndio anashikilia uhusiano wote wa maisha halisi ya mwanaume...na sio mama.
umemaliza kila kitu. mada ifungwe
 
mapenzi gani unayo yaongelea?

mke unaweza kuachana nae mkaanza kuitana ex. vp kuhusu mama yako mnaweza kuachana
mama 30%
baba 30%
mimi 40%
marafiki 0%
mke 0%


pia umeuliza swali la ajabu
 
Kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako
Waefeso 5:25 Enyi waume wapendeni wake zenu
Mwisho wa kunukuu in Mwanri's voice
 
Ingawa ni Mapenzi tofauti ila bado jibu la swali hili ni rahisi.Mama ni mmoja tu,unaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja.Mama ni mama yangu kwa umri wangu wote,mke atakuwa mke wangu mpaka pale tutakapoachana ama kifo.Kwangu time inajalisha,Ina nafasi yake kwenye uhusiano.Daima ni Mama baada ya Mungu.
 
nafasi ya mama haina mbadala, haizibiki, wala haina sub.
Mama 70% wife 30%.
Ye mwenyewe kamkuta na nimeishi nae miaka mingi kuliko yeye wife, yani hadi niishi na wife muda nilioishi na mama atakua keshatangulia msbele za haki.
Wife anaweza kukusaliti, kukuchukia, kukuua, hata kukufanyia ubaya wowote lakini mama kama ni yeye alikuweka tumboni miezi tisa yeye ndio final kwenye maisha yako. TAMBUA HILO
 
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
 
Mama ni Mke wa Baba

Mke wako ni Mama wa watoto wako.


Mama atabaki Mama.


Mke atabaki Mke.


Ukiegemea upande mmoja utakua na maisha magumu.


Yapasa wote uwakumbatie kwa usawa.

Mimi kwangu Mke na watoto kwanza halafu labda Mama au mwingine atafwatia labda Baba, mdogo wangu, Dada, au hata Babu /Bibi hao wote wanaweza kubanana hapo kwenye nafasi ya pili, lkn nafasi ya kwanza haina mjadala, ...
 
Kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako
Waefeso 5:25 Enyi waume wapendeni wake zenu
Mwisho wa kunukuu in Mwanri's voice

Umenukuu vema, kwa tafsiri isiyo rasmi ni hivi:

Heshima kwa MAMA, mapenzi ni kwa MKE.
 
Hatuchagui MAMA wa kuzaliwa naye, ila tunachagua MKE tumpendaye.

Tafakari!
 
Back
Top Bottom