Kati ya Mama na Mke Nani anapaswa kukaa Siti ya mbele wakati unaendesha Gari?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
KATI YA MAMA NA MKE NANI ANAPASWA KUKAA SITI YA MBELE WAKATI UNAENDESHA GARI?

Anaandika, Robert Heriel

Rafiki yangu Hosea amenipigia simu akaniuliza hivi; Kati ya Mama yake na MKE wake Nani anastahili kukaa SITI ya MBELE ya GARI wakati yeye(Hosea) anaendesha Gari? Nikaona niilete mada Hii kwenu. Ili tujifunze wote.

Imekuwa ni kawaida ya Watu kutaka kuwalinganisha MAMA na MKE kuwa Nani zaidi ya mwenzake.
Nataka kusema kuwa ni makosa makubwa kulinganisha vitu au Watu wasiolingana. Mke ni daraja jingine na Mama ni Daraja jingine.

Pili, Kati ya MKE na Mama hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake isipokuwa ubora wao utapimwa Kwa namna watakavyo au walivyotekeleza majukumu yao Kwa nafasi zao. Mama kuzaa pekee yake haimfanyi kuwa Bora isipokuwa yapo majukumu mengine kama malezi. Halikadhalika MKE kukuzalia Watoto pekeake haitoshi kumfanya awe Bora kwako isipokuwa majukumu yake Kwa Watoto pamoja na wewe kama mumewe.

Kama utapima uzito wa majukumu ya MKE na Mama bila kujali madaraja Yao basi utagundua MKE ni zaidi ya Mama, na hapo nazungumzia kimajukumu na kiwajibu. Hata hivyo hiyo haimfanyi MKE kuwa Bora zaidi ya Mama.

Asubuhi nilitoka kuelezea mada isemayo Watu Maskini na wajinga hupenda kuongozwa na Mitazamo na Maoni ya Watu zaidi kuliko Kanuni na sheria. Kama tungefuata Kanuni na sheria Hilo swali lisingekuwepo na haya mambo ya kulinganisha MKE na Mama yasingekuwepo. Kwa sababu Kanuni na sheria zipo wazi kabisa.

Rafiki yangu Hosea aliponiuliza swali hilo nilimjibu Kwa kumuuliza maswali yafuatayo;

1. Nikamuuliza; Kitandani mwako unalala na Nani?
Mbona haukuniuliza Kati ya MKE na Mama yako Nani ambaye utalala naye kitanda kimoja?
Akaguna, akasema hayo mambo ni tofauti na mambo ya SITI za magari.

2. Nikamuuliza, Kati ya Mama na MKE wako Nani anaitwa Mrs. Hosea? Akajibu MKE wangu.

3. Nikamuuliza, Wakati Mama yako anakaa SITI ya MBELE na wewe, je Mkeo atakaa nyuma na Baba yako(mkwewe)? Yaani Wakati Mama yako anang'ang'ania kukaa SITI ya mbele, Baba yako anakuwa yupo wapi au mumewe anakuwa yupo wapi?

4. Nikamuuliza, Watoto wako watakubali Mama Yao(Mkeo) umuweke Nyuma ilhali wewe ndiye mume wake(Baba Yao)? Huoni utajenga kitu kwa Watoto kuwa humpendi Mama Yao na umemuweka katika nafasi ya pili?
Huoni hiyo itakuathiri Huko baadaye Watoto wakikua?

Hata hivyo mtu yeyote anaweza kukaa SITI ya MBELE iwe Mama au MKE au mtoto itategemea Kwa maana hayo ni mambo madpfp ila kama kuna mazingira ya kuonyesha Nani anastahili kukaa MBELE basi MKE ndiye anayestahili. Maana kuna Wamama wengine wanachokochoko Sana. Kumzaa MTU hakukupi Haki ya kuvunja itifaki ya nature na kumfanya MTu uliyemzaa kuwa mtumwa. Nafasi lazima ziheshimiwe.

Kisheria na kikanuni, kwenye familia mama na Baba anashika nafasi ya tatu Huko kama sio ya nne. Kwa mtiririko huu.

1. Mume na MKE.
Hawa ndio nafasi ya Kwanza. Yaani MKE lazima Ampe mumewe nafasi ya Kwanza halikadhalika na Mwanaume/mume lazima Ampe Mkewe nafasi ya Kwanza katika familia.

2. Watoto
Hawa ndio wanashika nafasi ya Pili. mume na MKE huhangaika Kwa Ajili ya Watoto wao kuwalea mpaka wakikua.

3. Wazazi
Baba na Mama. Hawa ndio hushika nafasi ya tatu katika mahusiano ya familia. Baba na Mama yako ni familia nyingine yenye uhusiano wa karibu wa kidamu na ninyi. Ila haina maana wao ndio wawe namba moja.

4. Ndugu
Hawa ni wale mliozaliwa pamoja iwe Baba mmoja, Mama mmoja, mtoto wa Mama mkubwa au mdogo, wajomba, mashangazi n.k.

5. Jamaa
Hawa ni wale wenye undugu wa mbali, undugu wa Tochi.

6. Marafiki.
Hawa ni wale ambao hamna undugu lakini mnaukaribu na mahusiano mazuri.

Zingatia Watoto utakaowazaa wewe kwako ni namba mbili lakini wakishakua na kuanzisha familia wao watakuweka namba tatu. Na wajukuu watakuwa nafasi ya nne Huko, hivyo unakosa mamlaka ya kuingilia familia zao labda wakuombe ushauri.

Jukumu kubwa la mzazi ni kuwalea Watoto wake katika miaka yote ya uhai wake. Lakini sio kudai nafasi zisizo zako. Jukumu la mtoto ni kuwaheshimu wazazi wake, kwa kusikiliza mashauri Mema.

Kama Mama yako anakupenda Sana basi atapaswa aonyeshe upendo huo Kwa Baba yako mzazi. Yaani abaki kwenye nafasi yake. Nafasi ya mume wake asikupe wewe. Wala wewe usimpoke Baba yako nafasi yake Kwa Mama yako. Kila mmoja abaki kwenye nafasi yake.

Baba yako ndio anapaswa kumfanya Mama yako namba moja na sio wewe. Kumfanya Mama yako namba moja ni kutomheshimu Baba yako na kutokumpa heshima Mkeo.

Ni Sawa na Mkeo asikupe nafasi ya Kwanza kama mumewe, lazima ujihisi kudharaulika.
Hujawahi sikia Watu wakilalamika Wake zao hawawasikilizi ila wanasikiliza Wazazi wao.

Ukiona Mkeo hakusikilizi na hakupi nafasi ya Kwanza, fukuza mapema, Huko mbeleni sio salama. Ukiona Mumeo anajifanya anawapenda Ndugu au wazazi wake kuliko wewe kimbia, Achana naye huyo Hana Akili na hajitambui. Mwambie akalale na hao Ndugu zake. Wala usimuonee aibu wala usimfiche, mpe makavu.

Ni hatari kuoa au kuolewa na MTU asiyejua kutenganisha mipaka na makundi ya Watu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwani hiyo inabadilisha muda wa kufika mapema safarini, wote si mtashuka pamoja.Hata hivyo mke anastahili.

😂😂😂

Utaziweza Akili za Wanawake.
Wanawake wanapenda kupendwa.
Si unaona swali halijaulizwa Kwa upande wetu kina Baba.

Kwa Wanawake inamaana kubwa, Wanawake ni Watu wa kugombea nafasi za kupendwa😀😀
 
Hili ni swali pana sana na halina jibu la moja kwa moja. Inategemea mama yupo na baba au yupo peke yake, kama yupo peke yake kiheshima mnapaswa kumpa offer ya kukaa mbele coz kiafrica kiti cha mbele ni cha heshima yeye mwenyewe ndio akatae aseme atakaa nyuma.

Pia inategemea na mchango wa mama mwenyewe jamani kuna watu bila mama usingekuwa wewe na hata huyo mke asingekutazama mara mbili so kama mama yupo peke yake bila baba apewe nafasi ya kuchagua kama Baba yupo baba anakaa mbele mama na mke nyuma
 
Kamwe usiwaweke wanawake pamoja, watagombana tu.


Kila mtu akae na mmewe

😀
Umesema vyema,

Lakini Sisi Kama wanaume tunafanyaga kwaajili ya kuwafurahisha Mama zetu waone kuwa tunawapenda zaidi kuliko chochote. Tunawapa Moto.

Hivyo kumuweka SITI ya MBELE sio kosa ikiwa Mkeo ni muelewa.

Lakini kama Mama yako alishaanza kumchokoa Mkeo lazima Mkeo naye aone nafasi yake ipo hatarini, na hapendwi
 
Hili ni swali pana sana na halina jibu la moja kwa moja. Inategemea mama yupo na baba au yupo peke yake, kama yupo peke yake kiheshima mnapaswa kumpa offer ya kukaa mbele ...

Wakati unamuweka MBELE Kwa kisingizio hicho Mkeo awe muelewa na uwe umeshamseti hivyo.
Vinginevyo Jambo dogo kama hilo sio ajabu ukashangaa linazua yakuzua.

Hata hivyo wapo Wamama wenye chokochoko na kuwatishia Wakwe zao Maisha kuwa wao ndio top Kwa kijana.
Tena wengine wanasema na kuonyesha waziwazi. Hapo ndipo utata unapozuka.

Kama ulivyosema Mama anaweza kupewa Offer mara moja moja kukaa MBELE, ila anayestahili ni MKE.
Mama ni Wakati uliopita
MKE ni Wakati uliopo
Watoto ni Wakati ujao.
Lazima ujue kucheza navyo vyote
 
Back
Top Bottom