Kata ya Kunduchi Ulinzi Shirikishi mchango ni Tsh 15,000 kwa mwezi kwa Nyumba, Wajumbe wapewe EFD

Juzujuzi nilimsikia Makamu wa raisi anaongelea Wenyeviti wa Mitaa kutafuta/kusimamia mapato...nikajiuliza mtaani kuna vyanzo gani vya mapato...sasa nilipoona wanakuja na ishu ya ulinzi shirikishi nikajua ndicho walichomaanisha.

Hivi ni lazima kulindwa?.
 
Nimepata barua ya mchango wa Ulinzi Shirikishi tsh 15000 bila kujali nyumbani kwako una Mlinzi ama la

Ni vema basi Wajumbe wavawiwe EFD kwa ajili ya kumbukumbu nzuri ya Mapato na Matumizi maana hii nchi Wajanja Wajanja ni Wengi
Kwa siku Sh 500/= Sasa unalalamika hela kidogo hivyo unalindwa uhai wako na mali zako kwa hela kidogo hivyo? Watanzania nani katutupia pepo wa kulalamilikia kila kitu? Sh.500 hata soda haiwezi kununua lakini unabugia mabia mangapi kwa siku? Nakubaliana na wewe kuhusu monitoring ya hayo makusanyo iwe kwa matumizi ya EFD au njia nyingine mwafaka
 
Hii ndiyo maana halisi ya kula kwa urefu wa kamba.

Vyombo vya ulinzi kazi yake nini? Polisi wanalipwa mishahara kwa kazi ipi!

Tozo lukuki bado ulizi liwe jukumu la raia? Kweli Nchi sasa haitawaliki kwani hii tabia ya ulinzi wa mchongo itaenea Nchi nzima.
We ndiyo huna akili kabisa tafuta hata za kuazima. Unajua idadi ya polisi nchi nzima? Kawaambie viongozi wako mimi polisi watanilinda usichangie. Tumia vizuri akili. Ila ukivamiwa na panya road pambana nao usimlalamikie mtu
 
Nimepata barua ya mchango wa Ulinzi Shirikishi tsh 15000 bila kujali nyumbani kwako una Mlinzi ama la

Ni vema basi Wajumbe wavawiwe EFD kwa ajili ya kumbukumbu nzuri ya Mapato na Matumizi maana hii nchi Wajanja Wajanja ni Wengi
Kama hamtaki acheni, unadhani kuna Polisi wakuwepo kila mahala?

By the way uwiano wa watu na Polisi ni mdogo..
Acheni msitoe mtaona moto wa panyaroad.
 
Kwa siku Sh 500/= Sasa unalalamika hela kidogo hivyo unalindwa uhai wako na mali zako kwa hela kidogo hivyo? Watanzania nani katutupia pepo wa kulalamilikia kila kitu? Sh.500 hata soda haiwezi kununua lakini unabugia mabia mangapi kwa siku? Nakubaliana na wewe kuhusu monitoring ya hayo makusanyo iwe kwa matumizi ya EFD au njia nyingine mwafaka
Wapi nilipolalamika manka?

Nimeshauri Wajumbe wapewe EFD machines kwa ajili ya risiti
 
Nimepata barua ya mchango wa Ulinzi Shirikishi tsh 15000 bila kujali nyumbani kwako una Mlinzi ama la

Ni vema basi Wajumbe wavawiwe EFD kwa ajili ya kumbukumbu nzuri ya Mapato na Matumizi maana hii nchi Wajanja Wajanja ni Wengi
Acha uongo, kila kaya ni tsh elfu mbili, na wenye maduka elfu tano kwa mwezi nnavyojua ,kwa maeneo mengi
 
Usalama upo au?
Je kuna uwizi wowote unaotokea
Alafu ungetuambia kata hiyo kunduchi
Ipi hiyo kama kunduchi ushuwani bei
Hiyo sawa tu,kama kunduchi uswaz lazima bei iwe chini

Ova
Kata ya Kunduchi ni kubwa sana mkuu imeanzia Tegeta kuja mashimoni wanapolipua mawe kushuka hadi baharini yote ni Kunduchi hiyo.
 
Back
Top Bottom