Kasumba hii tutaiacha lini?

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Kwa muda sasa tumekuwa na kasumba ya kujiona kila mmoja wetu ni wa maana kuliko mwingine.
Kasumba hii imepelekea wengine kujiita Waheshimiwa.
Wengine wasomi,Maofisa usafirishaji n.k.
Kwa kweli mimi binafsi sipendezwi na Kasumba hii kwani haitujengei umoja kama Taifa bali unatugawa katika Matabaka.
Nakumbuka kuna kipindi enzi za Mwalimu watu tulikuwa tunaitana Ndugu bila kujali nafasi,cheo au elumu ya mtu aliyokuwa nayo.
Nachelea kusema kwamba,hii ilisaidia sana kuleta usawa miongoni mwetu,na hivyo kujenga umoja na Mshikamano ambao tumekuwa tukijivumia kama Taifa.
Nadhani ifike mahala sasa turudi kwenye utamaduni huo wa kujiona watu wote tuko sawa.
Kasumba ya kila mmoja kutaka kujitofautisha na mwingine eti kwa sababu tu ya Cheo su elimu na taaluma yake sasa inatakiwa ife ili turudi kwenye kujiona kwamba wote ni sawa na tuitane tu Ndugu.
Hii itaimarisha zaidi upendo miongoni mwetu na kujenga umoja wenye usawa na mshikamano imara zaidi.
Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kasumba hii imepelekea wengine kujiita Waheshimiwa.
Wengine wasomi,Maofisa usafirishaji n.k.
Kasumba haiwezi kuisha, ikiwa hata wewe umbae unajaribu kuihabarisha jamii hujui nini unaongelea.

Ofisa usafirishaji hicho ni cheo, watu wanakausha darasani kusomea. Wanapohitimi, jamii inawatambua kwa cheo Chao. Sina haja ya kuelezea maana ya msomi au muheshimiwa pia.

Ulichotakiwa wewe ni kusema watu hawatakiwi kudharau wengine hata kama kuna tofauti kubwa ya kipato kati yao.

Alafu kuhusu issue ya kuitana ndugu, zama zimechange. Siku hizi tunaitana "Kaka" hata kama hatufahamiani. Au "Mkuu", "Boss" nk
 
Back
Top Bottom