Kasi ya ukamataji wa meno ya tembo

mtupori2010

Member
Sep 13, 2010
22
8
Naomba kuuliza, mwenye taarifa anijuze. Kuna wakati fulani tanzania ilitaka kuuza meno ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye maghala yake. Ilkaleta mzozo kimataifa na hazikuuzwa. Kenya wao wakachoma moto pembe walizokuwa nazo!!! Kwa idadi ya tembo wanaodaiwa kuuawa ukihesabu meno yaliyokamatwa si wangekuwa wamekwisha? Inanitia shaka kuwa zile pembe zilizokuwa zimehifadhiwa ndizo wajanja wanazichukua na kusafirisha hasa ukizingatia picha tunazoonyeshwa ni za meno ya zamani. Je serikali imekagua maghala yake kuona kama bado zipo? Nakumbuka ilikuwa enzi ya Mh Maige.Tusije tukawa tunauwa wawinda swala tu kumbe meno yanatoka kwenye stoo za serikali.
 
Nakubaliana na wew meno yaliokamatwa kwa wachina na kule Unguja ni tembo wa zamani kwa muonekano wake na size maana ni makubwa kuna uwezekano mkubwa yametoka kwenye maghala ya maliasili pale Chang'ombe(Ivory) hasa ukizingatia Waziri anavyofika fasta maana vijana wanawajua waliowauzia so wanamwezesha Kagasheki ale maujiko na watu wasahau madudu yake.Ingefaa kama kweli serikali ina nia ya dhati kupambana na ujangili huu kutangaza idadi ya meno yaliokuwepo kwenye maghala na kuyateketeza.Vinginevyo tunachezeana picha tu kuwa tunapinga hii biashara kumbe tunaunga mkono kwa kuuza meno yaliyopo kwenye maghala.
 
Back
Top Bottom