Kashfa ya Richmond bado mbichi…

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
001edward lowassa 1.jpg

Elias Msuya
MKANGANYIKO wa kauli za viongozi wa serikali kuhusu ugonjwa unaomsumbua Naibu waziri wa ujenzi Dk Harrison Mwakyembe unahusishwa na fukuto la kashfa ya Richmond aliloliibua na kusababisha baadhi ya vigogo wa serikali kujiuzulu.

Mengi yamesemwa na watu mbalimbali kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa kashfa ya Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond.

Ripoti ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Dk Mwakyembe, iliyohitimisha safari za mawaziri wawili, wa Nishati na Madini kwa vipindi tofauti, Naziri Karamagi na Dk Ibrahim Msabah, sambamba na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa.

Kutotekelezeka kwa maazimio 23 ya Richmond
Kamati ya Dk Mwakyembe ilitoa maazimio 23 ambayo Bunge liliitaka serikali iyatekeleze.

Hadi sasa ni maazimio 10 tu yameshafanyiwa kazi huku mengine 13 yakiwa bado hewani na yasiyozungumziwa.

Waziri Mkuu aliyemrithi Lowassa, Mizengo Pinda, amewahi kutoa taarifa Bungeni Agosti 28, 2008 na Februari 11, 2009 ambapo mojawapo ya taarifa yake ilijadiliwa na kamati, ambazo nazo zililitaarifu Bunge kuwa utekelezaji wa Maazimio 10 kati ya 23 yaliyotolewa na Bunge, yalifanyiwa kazi hadi mwezi Februari, 2009 na Maazimio 13 bado yalikuwa hayajakamilika.

Maazimio hayo 13 ni nambari 1, 2, 3, 5, 7, 8, 9, 10, 11, 13, 14,15 na 18 ambayo Bunge lilitaarifiwa tarehe Februari 10, 2010 kuwa yako katika hatua mbalimbali ya utekelezaji.

Hivi karibuni Mbunge wa Ubungo John Mnyika amepeleka hoja binafsi Bungeni akilitaka Bunge liazimie uamuzi wa Bunge uliofanyika katika Bunge la Tisa Mkutano wa 18 wa Februari 10, 2010 kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya mkataba baina ya Tanesco na kampuni ya Richmond Development Company LLC; ubadilishwe.

Katika maazimio hayo, Mnyika anataja azimio namba tatu, ambalo liliagiza Mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa na Dowans Holdings S.A.) na ile kati ya Tanesco na IPTL, Songas, Aggreko na Alstom Power Rentals, ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo Mikataba ya Madini ilivyopitiwa upya na Serikali, akisema iwapo Azimio hili lingetekelezwa kwa ukamilifu wake, gharama za uzalishaji Tanesco na serikali kwa ujumla zinazotokana na matatizo katika mikataba zingepungua.

Kuhusu kurekebishwa kwa Sheria ya Maadili ya viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code of Ethics Act), ili kuondoa mgongano wa kimslahi kwa viongozi wa serikali kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, Mnyika ameitaka Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hilo ndani na nje ya Bunge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.

Mnyika anasema kuwa maazimio namba nane na 14, yana maudhui yanayofanana kwa sababu yanaitaka Serikali iwawajibishe Viongozi wenye dhamana ya kisiasa waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini ambao wakati ule alikuwa ni Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

Hata hivyo anasema kuwa licha ya uchunguzi wa ndani na nje ya nchi wa Vyombo vya Dola vya Kimataifa ndani ya miaka miwili, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa wahusika katika kashfa ambayo maazimio ya bunge yalipitishwa zaidi ya miaka minne iliyopita hali ambayo inaweza kusababisha hata mashahidi na ushahidi kupotea.
Kuhusu Maazimio namba tano, saba na 14, anasema hayajatelezwa mpaka sasa na mamlaka ya juu ya serikali.

Kashfa ya Richmond bado mbichi
Tangu Lowassa amejiuzulu, amekuwa akitumia muda mwingi kujisafisha na kashfa hiyo kwa udi na uvumba. Kana kwamba kashfa hiyo haikuwa na mtuhumiwa, Rais Kikwete ameonyesha kumtetea Lowassa akisema kuwa hiyo ni ajali ya kisiasa.

Katika kuonyesha kukerwa na kashfa hiyo, mwishoni mwa mwaka jana katika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM (NEC) Lowassa alimtaja Rais Kikwete kuhusika na kashfa hiyo.

“Mwenyekiti (Rais Kikwete) utakumbuka kwamba, mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu, ukasema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo nahukumiwa kwa kuitwa fisadi, kwa nini?” anasema Lowassa na kuongeza,
“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kulinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba eti mimi ni fisadi?”.

Ugonjwa wa Dk Mwakyembe
Ugonjwa wa ajabu wa ngozi unaomsumbua Dk Mwakyembe, unahusishwa na sakata la Richmond hasa kutokana na kauli tata za viongozi waandamizi wa serikali na wale wa jeshi la polisi na kwa upande mwingine na Mwakyembe mwenyewe.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashakriki Samuel Sitta amekuwa akizungumza bila kutafuna maneno kuwa Dk Mwakyembe amelishwa sumu, lakini Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha anapinga huku akimtaka apeleke ushahidi polisi.

Hayo yakiendelea, Mkurugenzi wa Idara ya Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba naye anaibuka na kudai kuwa Dk Mwakyembe hakulishwa sumu ila anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi.

Hali hiyo inasababisha, Dk Mwakyembe kuvunja ukimya na kutoa taarifa ya masikitiko yake dhidi ya jeshi la polisi huku akisema kuwa halimtendei haki hasa kwa kuaua kutoa taarifa yenye kupotosha.

Lakini hapo hapo, Waziri wa Afya Dk Haji Mponda aliibuka na kuikana taarifa ya Manumba kwamba haikutoka katika Wizara ya Afya.
Mfululizo wa matukio hayo unaonyesha utata mkubwa na mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bashiru Ally, chanzo cha viongozi wa serikali moja kutoa kauli zinazopingana kuhusu chanzo cha ugonjwa wa Dk Mwakyembe ni serikali kushindwa kuukabili ufisadi.

“Ukiweka kando suala la viongozi kutoa kauli za kujikanganya kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe kwamba amelishwa sumu au la, lakini ukiliangalia jambo hili utabaini kuwa chanzo chake ni ufisadi, na niseme kwamba hatua hii, mafisadi wameteka dola na hii ni hatari sana kwa taifa,” anasema.

Anasema ni makosa makubwa kuwaacha watu waliotuhumiwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi kama vile wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na nyinginezo wakiendelea kuranda mitaani pamoja na wale walioibua ufisadi huo.

Anainyooshea kidole Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa kutotekeleza maazimio ya kamati ya Dk Mwakyembe kuhusu sakata la Richmond.

“Kama Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ingetekeleza maazimio ya kamati ya Dk Mwakyembe, leo hii hofu kwamba kalishwa sumu, isingekuwepo na ugonjwa wake ungeonekana wa kawaida” anasema.

Kosa la Sitta
Licha ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta kuwa mwanzilishi wa uchunguzi sakata la Richmond Bungeni hadi kupata ukweli wake, bado analaumiwa kwa kutolisimamia kikamilifu kuhakikisha kwamba serikali inabanwa na Bunge hadi inatekeleza maamuzi yote.

“Sitta alifanya makosa makubwa kulegeza kamba alipokuwa Spika. Halafu leo anaibuka na kulia kwamba Dk Mwakyembe amelishwa sumu, ameshachelewa. Alitakiwa kukaza uzi wakati uleule ili serikali itekeleze maazimio yote kikamilifu” anasema Bashiru.

Historia ya Sakata la Richmond
Mwaka 2006 baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani kulitokea tatizo kubwa la uhaba wa umeme. Hapo ndipo Serikali ilipoanza kufanya mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za dharura za kutatua tatizo hilo.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa alikuwa mstari wa mbele katika mikakati hiyo. Matokeo ya kampuni ya Richmond Development (LLC) ni miongoni mwa mambo yaliyofanyika katika utawala wake.

Mengi yamejitokeza baada ya kampuni hiyo kuanza kazi zake. Mojawapo ni pale ilipobainika kuwa kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kama ilivyodhaniwa, badala yake kulikuwa na michezo michafu iliyofanyika kwa maslahi ya wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wa serikali.

Mwaka 2007, sakata hilo lilifika Bungeni ambapo aliyekuwa Spika wakati huo, Samuel Sitta aliunda kamati iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe ili kuchunguza upya suala hilo.

Kamati hiyo ilichunguza sakata hilo na kutoa taarifa ilionyesha kuhusika kwa viongozi wa juu wa serikali akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa

Chanzo.
Kashfa ya Richmond bado mbichi
 
Heading Vs Content??????

The heading reflects what is in the content, that the sickness that Mwakyembe is suffering from cannot be seperated from the Richmond scandal. In other words those investigating the source of his illness cannot succeed without delving into the Richmond saga; maybe Mwakyembe, had he not been the chairman of the committee that investigated the said company, would be in perfect health condition today!!
 
Mi naona kuna lengo limejificha kuchelewesha utekelezaji wa maazimio 13 ya bunge, moja kubwa likiwa ni kupoteza ushahidi kwa gharama yoyote ile kama inavyoonekana sasa kwa Mwakyembe, Sitta kupoteza nafasi ya uspika na wanakamati wengine kupoteza nafasi ya ubunge ktk majimbo yao kama ilivyotokea Nzega na mbinu zingine zaidi zinaendelea kuandaliwa kuzima suala hili. Pili likikaa muda mrefu na wahusika wengine wanaweza wakawa wameiaga dunia kwa sababu mbalimbali na watanzania pia ni wepesi kusahau.
 
Ndio maana wanataka kumpoteza mwenyekiti wa kamati iliyochunguza hiyo kashfa!! Akipotea huyo basi kila kitu kitakuwa kwishney!!!
 
Back
Top Bottom