Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Eleven pages of stuff in less than......hours. 104 contributions and still counting. 1,261 observations so far!

This surely must be the most pressing issue of our times so far.

Msinitupie madongo, please!!!!!!!! It's just that I too needed to add my busaras on this issue.
 
jamboonormal_Chifupa_Skendozzz.jpg


Amina Chifupa wa Mpakanjia
 
Moto huu hakuna anayeweza kuuzima..ni mabadiliko ya wakati na kizazi. Nasema siasa ya bongo imeingiwa na vijana...tena sasa hivi bado huu uchafu haujakolea maana bado wakina JM, Kingunge, Kawawa n.k wako hai na wananguvu za kama zile za Yesu aliponyoosha mkono mawimbi ya bahari yakapoa...hawa kwa siasa za bongo ndani na nje ya CCM wana nguvu hizo. Wanauwezo wa kupoza mawimbi ya siasa bongo; yeyote ndani ya Chama akiambiwa ujumbe kutoka kwa JM unasema usifanye hiki au kile basi hakuna kusema LAKINI..!! Unatiii

Siku ikifika Mungu akawachukua hawa Wazee ndio itakuwa mwisho wa CCM maana MOTO unakaowaka utavunja Chama....hebu fikiria Nchimbi atake kugombea Umakamu M/kiti wa CCM halafu aje na Kampeni Chafu kiasi hiki.

HATARI?


Aisee,umeongea kitu kizito sana na nadhani ni matokeo ya uchambuzi yakinifu wa hali ya juu sana.Kama ulivyosema,skandali hii ni ishara ya nyakati na kizazi.Cant agree more with you on that.Umehit point haswa.

Kwa upande mmoja sakata hili linaweza kutoa taswira ya namna ukosefu wa maadili ulivyo tatizo sugu katika medani za uongozi huko nyumbani.Sio siri kuwa viongozi wetu wengi sio wasafi kimaadili.Na hilo linaanzia ngazi za juu kabisa.Recently,nimeskia wajuzi wa mambo wakidai PM kazidisha uswahiba wake na wabunge wa kike...wasio na uoga wakaenda mbali zaidi kudai kuwa "anawabadili" kama nguo.Guess what,AC alikuwa miongoni mwa hao suspects.JK mwenyewe ni usual suspect,na ilishanong'onwa huko nyuma kuwa "alimsaidia sana" AC ktk harakati za kupata ubunge.

On a street level,Mpakanjia alimuoa AC katika muendelezo uleule wa Ng'wizukulu Jilala kumuoa Nora,Fikiri Madinda kumuona Aisha,Mwisho Mwampamba kumuoa Ray-C,etc etc....nyingi ya hizi ni ndoa za umaarufu.Hakuna mapenzi ya dhati bali ni muendelezo wa jitihada za kutafuta ujiko.Yaani ukiwa staa (in TZ sense) basi lazima uoe staa.Well,sio dhambi kufanya hivyo coz hata huko Hollywood ni kama hivyo,lakini kwa sie wenye maadili ya kiafrika tunaamini kuwa ndoa sio suala la headings kwenye vyombo vya habari.Ndoa ni takatifu na kabla pande mbili hazijaamua kuwa ziko compatible kuna mambo kadha wa kadha yanayopaswa kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kuangalia background info.Kwa yeyote anayemjua Medi na AC atakubaliana nami kuwa ndoa hiyo ilikuwa bomu la wakati linalosubiri kulipuka muda wowote.Bila kuingilia utashi wao,yayumkinika kusema kuwa kama Medi angekuwa anatafuta mke wa dhati asingemuoa AC,na hivyohivyo kama kweli AC alikuwa anatafuta mume wa dhati basi she it wrong alipoamua kuolewa na Medi.CVs zao zilikuwa zinaihukumu ndoa yao.

When AC became an MP Medi alidhani kuwa huo ulikuwa wakati mwafaka wa kutumia nafasi ya mkewe kisiasa kufanikisha madili yake (mume).Wanaomjua AC walijua dhahiri huko bungeni ataenda kuwa mlo wa vigogo walafi.

Ndoa za kisanii hudumu au kuvunjika kisanii pia.
 
Aaaah mwanangu Zitto, hata hatushtuani bob!... sasa itakuwaje?

Mali hizo mjomba sii rahisi, waache wao (CCM) wachukue nchi lakini malipo yake makubwa zaidi - twala nao sahani moja.

Kuna msemo usemao kuwa mme mdhinifu hafai ila kwa mke mdhinifu!...na leo kweli bibie kakutana vingongo vya Kibembe!......maneno hayo!

On the other side mjomba mke wa mtu hapo kidogo kuna mushkeri lakini!... sijui kama ningekuwa nafasi yako ningeishika dini!... Picha inajieleza mengi.
 
Mnashangaa nini amina chifupa "kusingiziwa" ( i cant proove it even though different sources have ) kwamba katembea na fulani, je na hao viongozi wakubwa kabisa serikalini ambao wapo responsible na nchi yenyewe achilia mbali na chifupa ambae ni mbunge tu ?

Hapa kweli kuna ishu, nadhani na hii ni kutokana na hao/huyo mtu aliyefanya hivyo atakuwa katika sort ya mtandao fulani !! anyway chifupa wewe kaza moyo, kama kweli ulifanya wanachosema umefanya then u deserve it na kama hukufanya basi mungu akupe hekima kuondokana na kuepuka masuala kama haya baadae !!

Sasa chifupa, hiyo vacancy unaonaje mimi nikiijaza ??

tuwasiliane mheshimiwa chifupa: nitumie pm
 
Mpaka sasa hivi ni bila bila

huyo binti hajaonekana wala kusikika na kwa kweli hali inasikitisha.

Kama nilivyosema hapo awali lolote likimtokea huyu binti Nchimbi ajue kuwa DUNIA NI NDOGO

natumai busara za MZEE WA PAMBA zitaingia lakini NCHMBI kama ataendelea na kuleta za kuleta then hakuna means itabidi awe NEUTRALISED after al maslahi ya Chama na Taifa ni muhimu zaidi ya Persoalities kama yeye
 
Mheshimiwa Samvulachole,jukumu la kumlinda AC ni la polisi.Usalama wa taifa kazi yao ni exact that,polisi ni usalama wa raia,ila usalama wa taifa wana kitengo kinachoitwa PSU,(Presidential Security Unit),ndio ma-body guard wa rais,makamu pm na nk.
Hali ilivyo sasa hao PSU(Presidential Security Unit) watalinda hata wanamtandao,maana NDIO wanaendesha nchi.Huoni jinsi kauli za kujichanganya zilivyo nyingi siku hizi? serikali moja,jambo moja lakini kauli mia moja.
 
Gazeti.jpg

UDAKU BONGO NAKO UKO BIZE..wanaume wote CCM akaenda kumungunyuliwa na CHADEMA?

Kaka samvu sasa napata jibu kwa nini kijana zitto alikuwa anaongea kwa uhakika kwamba ,kichwa kimoja chadema ni hamsini ccm...sasa inaonekana binti alikuwa akimuona handsome boy ,portable mmoja zitto anaona kama vile wako hamsini...alafu siunajua upande wa pili BP, Tele...kwani mada kesi haogopi!!![kiddin]
 
Kama humu JF kunakuwa na topic nyingine za maana zaidi na zinafutwa bila ya sababu, wala taarifa basi ningewaomba wahusika wafute topic hii na isichangiwe kabisa, na pia uongozi wa JF uwaandikie barua waandishi wa habari wa tanzania, wasipende kuandika au kuzusha Kashfa ambazo hazina ushahidi wala ukweli wowote.
Hamuoni kama kashfa za aina hii zinadhalilisha sana BUNGE!!! hivi Bunge la Jamhuri Yetu ya Tanzania ni sehemu ya kupeleka malalamiko ya kijinga na ya kinyumbani kabisa na yakarushwa hewani? Hivi hamuoni kwamba kuchangia au kushabikia topic za aina hii ni kushiriki kikamilifu katika kudhalilisha chombo cha uma yani BUNGE!!
sasa haya ni mambo ya nyumbani na sioni haja kwanza ya kumuandikia barua Spika!! nadhani ni busara zaidi kwa Mpakanjia kuandika barua ya malalamiko kwa mjumbe wa nyumba 10 kwani ndio wanaoamua kesi za ugoni.
Bw. Mpakanjia huna haja ya kulalamikia bunge kwa sababu umeshamhukumu mkeo kwa kumpa talaka, sasa bunge likusaidie nini? usichanganye Mapenzi yenu ya nyumbani na maswala ya siasa.
FUTENI TOPIC HIIII HAINA MAANA YOYOTE ZAIDI YAKUDHALILISHA CHOMBO CHA UMA; BUNGE SIO SEHEMU YA KULETA MAPENZI:

MFANO: MIMI NIKITEMBEA NA MWANAMKE ANAYEITWA HADIJA NA AKIWA ANAFANYA KAZI YA POLISI, NITASEMA NATEMBEA NA HADIJA NA SIO POLISI
kwa hiyo kwa kesi hii ni hayo hayo tu AMINA NI MHE MBUNGE na AKIWA NYUMBANI ATAKUWA NI AMINA CHIFUPA KAMA MDANGANYIKA WA KAWAIDA TU:
UBUNGE NI TITEL TU WANDUGU CHIFUPA AKIWA NYUMBANI NI CHIFUPA TU.
 
Hakuna cha kufuta wala nini

wenzio ndio tunapenda topiki kama hizi naona unataka kuleta yale yale ya mainstream media kujidai wana standards ili hali wanakuja humu ndani Kunyonya vitu

kwa taarifa yako Mods walifuta THREADS 4 zinazohusiana na hii kashfa lakini matokeo yake wali GIVE IN for simple reason:

WE DARE TALK OPENLY

je unajua kuna BLOG NGAPI zingeanzishwa leo kama utawakataza watu wasiongee? watu uzuri sasa wanajua wanazo alternatives



Gazeti.jpg
 
nani anasema kawawa et al wanaweza kumfunga paka kengele..mmesahau ugomvi wa miaka ya 70 mwisho mwisho wa pius na rashid kumgombea anna ....hadi mwisho ikabidi pius aonewe tu huruma aachiwe mtoto since alikuwa mpweke mkewe akiwa mgonjwa...kawawa alikuwa jogoo yule mfanon wake ni john...na huu ndio muendelezo wa kina emmenuel,hapa tatizo kilichowauma ni kuwa kwa nini ampe zitto??

huyu mtu aliyeishia la pili mpakanjia ana tabu sana,yeye ndio kicheche namba moja ,sasa kama huduma yake inapungua ....spika anahusika vipi? kama ni spika naye ana mke wake lakini wakiwa bungeni wanachapa kazi kama wabunge mambo ya usiku kando ,sasa sembuse kujadili talaka ya mbunge !!!

mimi naamini mambo ya chumbani ni binafsi ....nilikuwa nasoma tabloid moja la nje juu ya condy kudaiwa kula vitu na foreign secretary wa uk,italia na canada ...wamarekani hawaaangalii sana hilo wanaangalia kazi yake;but je wanawake wa kiswahili wanaweza kumegwa na mtu pasi kuanza kutoa siri za ofisini,mme ets...maana kwa mzungu mkiwa kwenye business ya sex hakuna kuleta kuulizana mambo ya kazi au lakini wenzangu na mimi ukimchukua atakuambia kila kitu kuhusu babake,dadake,kaka ets within a short period....
 
Naona hapa hatuna budi kuwekana sawa na kuwa wa kweli kwa nafsi zetu. Naombe nijieleze vizuri na kueleweka. Sithubutu hata kidogo kutetea, kuhalalisha, au kuendeleza kitendo ambacho wanatuhumiwa vijana wetu. Nitakuwa wa kwanza kabisa kulaani kitendo na kukilaani. Nitafanya hivyo si kwa sababu ya uanasiasa wa wanaodaiwa kuhusika bali kwa sababu ya suala zima la maadili ya mtu wa ndoa (Bi. Chifupa) na kijana mchumba wa mtu (Zitto). Kwa maneno hayo ningelikabili suala hilo kama ambavyo kaka yangu au rafiki yangu angehusishwa nalo. Nisingefikiri hata kidogo kuwa tatizo kubwa kabisa la maadili, lililowahi kutokea limetokea na linatishia kuvunja vunja jumuya au chama! Ningeliweka jambo hili katika maudhui yake sawia. Msimamo wangu uko hivi:

a. Kama ni kweli kuwa ndugu zetu (siyo maadui kwa namna yoyote ile) wamehusishwa na kitendo hiki, basi ni kosa, kukengeuka kimaadili ya kijinsia, na ni jambo la aibu. Kwa mtu wa ndoa kwenda nje ya ndoa yake kwa sababu yoyote ile ni kinyume na kiapo cha ndoa yake na kwa hilo jamii yaweza kuoneshwa kutokufurahishwa na kitendo hicho. Kwa mtu ambaye anajua mwenzie anayemtongoza ni mtu wa ndoa basi kwake huyo naye ni kosa na ni aibu kwake na hasa kama na yeye ana mtu ambaye amemuahidi penzi lake.

b. Kama (a) ni kweli basi jukumu la kwanza na kuwajibika kwa kwanza kabisa siyo kwa JF, Chadema, CCM au nchi nzima! Jukumu la hawa vijana kujieleza ni kwa wale wawapendao na familia zao. Kama AC ameshindwa kumshawishi mumewe kuwa maneno hayo ni majungu, au kama Medi ana ushahidi usiopingika kuwa kweli mkewe alikuwa na mahusiano na Zitto hilo ni suala la nyumba yao! Kama Medi ameamua kumhusisha Spika (kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe) na hivyo kulifanya jambo hilo kuwa la hadhara, hayo ni maamuzi yake! Kwa kijana Zitto, jukumu lake la kwanza ni kwa mchumba wake, na familia yake! Kwa watu hao wa karibu ndio anatakiwa kwenda kutoa maelezo kwanza kabla ya sisi watu wa JF (au watu wa kwenye vyama vya siasa) kurukia na kutoka tuombwe radhi!!

c. Kama (a) na (b) ni vya kweli, basi AC na KZ kwa kuangalia nafasi zao katika jamii wanajukumu jingine nalo ni dogo kuliko hilo la pili. Kwa vile hawa ni viongozi itakuwa ni kosa kubwa sana kuwaangalia wao kama "mifano" ya jamii! Mtindo wa kuwaona wanasiasa kama role model ni sawa na mtindo wa kuwaona wasanii kuwa ni role model na wanapoharibu basi hisia ya kusalitiwa, kukatishiwa tamaa, na kuachwa kwenye mataa hujiri! Kwa vile vijana hawa ni wabunge wa Bunge letu na wameonesha umahiri bungeni n.k basi wengi wanawatarajia kuwa basi vijana hawa wanapaswa kuwa na maadili yaliyotukuka! Kutarajia hivyo hata kwa nia nzuri kiasi gani au kwa ajili ya chama kwa kiasi gani ni kuwa na matarajio yasiyo na msingi!!

Ni kweli tunaweza kuweka maadili kwenye ngazi ya juu lakini kutarajia kuwa watu hawatakengeuka na wakingeuka basi tuwateremshie nyundo za laana ni kutarajia maji jangwani! Tuwe wa kweli. Kitendo cha ngono na hisia ambazo huambatana nazo hakitokani na mantiki, usomi, ujuzi, umahiri wa uongozi n.k! Ni kitendo ambacho kinapita maelezo ya kitaaluma! Ni kitendo cha kinyama na kibailojia! Wengi wetu tunaweza kutawala hisia zetu na vionjo vyetu kwa muda fulani, lakini ni wachache wetu ambao wanaweza kutawala vitu hivyo wakati wote, dhidi ya watu wote, na mahali popote!! Ni kwa sababu hiyo basi, licha ya kukubali kuwa kitendo hicho kimepotoka, hata hivyo tusitoe hukumu ambayo yaweza kutumuka dhidi yetu pia! Kipimo kile kile tupimiacho ndicho kitakachotumiwa kutupimia na sisi!!

d. Nakubaliana na maoni ya baadhi ya watu kuwa maadili ni kitu muhimu sana kwa kiongozi. Katika hili nitumie maneno mawili ambayo yote kwa lugha yetu yanatafsiriwa kama "Maadili"; Morality na Ethics. Ingawa yote yanahusiana, maana yake kwa ujumla ina mstari mwembamba. Kuna maadili yanayoongoza jamii nzima katika kuamua matendo fulani ni mema au maovu, mazuri au mabaya. Kila jamii ina mambo ambayo yanakubalika kuwa ni mema na mengine ambayo yanakatazwa. Matendo haya mara nyingi hutegemea mafunzo ya dini, na tamaduni yanapotendwa. Wakati Tanzania kuoa mke zaidi ya mmoja inakubalika na kutambulika kisheria na swali la umaadili halipo, nchi kama Marekani jambo hilo ni marufuku na linaonekana ni kinyume na maadili mema (immoral). Hata hivyo kuna matendo ambayo watu fulani hutarajiwa kutenda na hukatazwa kutenda kutokana na ajira zao au nafasi zao. Mara nyingi matendo haya hayajali hasa dini au tamaduni bali yanajali zaidi athari zake katika jamii na wahusika (ethics).

Ndugu zetu wanatuhumiwa kuvunja yote mawili: Hilo la pili la (ethics) tunaweza kujadiliana uzito wake kwa wadaiwa, hilo la kwanza kwa wengi halina ubishi.

Kitu ninachokataa ni kujaribu kufanya makosa yao kuwa ni kuvunja ethics za kazi na za uongozi wa Taifa. Hivi ni wapi Chadema iliposema kuwa kitendo cha zinaa nje/kabla ya ndoa ni kosa linalohitaji kuombewa radhi? Nimeangalia kwenye Kanuni za Maadili ya CCM hakuna kosa hilo!! Haijatokea kiongozi kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa vile amelala na fulani!! Je hilo linahalalisha vitendo hivyo? La hasha! Ila jambo moja linatuambia ni kuwa vitendo hivyo havilingani na rushwa, wizi, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa siri za chama n.k!! Ni kweli AC na KZ watakuwa wameghafilika kwa kujihusisha na vitendo wanavyodaiwa kufanya, lakini kulinganisha matendo hayo na uhalifu na matendo yanakatazwa kisheria siyo kitendo cha haki hata kidogo!!

Nimalizie kwa pointi hizi mbili:

1: Hapa niseme hivi: Msingi wa kufukuzwa AC kutoka CCM itakuwa ni madai ya kuwa kutokana na mahusiano yake (ya mapenzi au vinginevyo) na Zitto basi alikuwa anapenyeza siri za CCM kwa mbunge huyo wa upinzani. Kaeni chonjo, kwani kikao cha Kamati Kuu kinafanyika mwishoni mwa juma hili!

2: Kwa wale ambao tunamuita Zitto ni rafiki, tusimshawishi hata chembe kulizungumzia jambo hili hadharani sasa ila alishughulikie na watu wake wa karibu. Zitto ASILIZUNGUMZIE jambo hili hadi itakapojulikana Amina atasema nini na CCM itachukua hatua gani. DON'T let him play his cards, hadi atakapoona kadi za CCM zimechezwa, why you may ask;


IT IS POLITICS after all!!!
 
Mpakanjia anatwanga maji ndani ya kinu maana nina sikia kwamba hata Spika anaye pelekewa mashitaka huenda kisha lamba dume .Sasa badala ya mashitaka kwake unaweza kuwa unampa matatizo Mzee wa watu bure na matatizo ya mabarua ya ngono zao mitaani .
 
Hii ni lesson kwa JK na timu yake!
mchezo mchafu wanaoucheza utawagharimu sana!
Ni time ya Nchimbi na wenzake kupigwa chini kwa maslahi ya chama!
This is shame, BUL@#$%HIT and ujinga kabisa!
Maskini Tanzania .. dah!!!!!!!!!!!!
 
Mpakanjia anatwanga maji ndani ya kinu maana nina sikia kwamba hata Spika anaye pelekewa mashitaka huenda kisha lamba dume .Sasa badala ya mashitaka kwake unaweza kuwa unampa matatizo Mzee wa watu bure na matatizo ya mabarua ya ngono zao mitaani .
Kama mambo ni haya basi kuna siku bendera ya nchi itapepea nusu mlingoti mwaka mzima maana itakuwa vifo mfululizo.
 
brutus hawa wote wanafuata nyayo za kampeni chafu alizotumia muungwana kupata ukuu wa kaya ,dhidi ya SAS na ZERO....so haitakuwa halali wala sidhani kama atakuwa na sababu ya kuwakemea wakati mtandao kampeni chafu NDIO ZAO...ndio maana sioni haja ya kuharakisha kumlaumu zitto wakati inajulikana kuwa kampeni ccm ndio zimeanza ...ZITTO TULIA TULI...na hizi kampeni watachafuana sana ,huu ni uwenyekiti wa UV bado umakamu mwenyekiti taifa[bara]....tutasikia mengi!!!
 
Gazeti.jpg

UDAKU BONGO NAKO UKO BIZE..wanaume wote CCM akaenda kumungunyuliwa na CHADEMA?

Kama mambo ni haya basi kuna siku bendera ya nchi itapepea nusu mlingoti mwaka mzima maana itakuwa vifo mfululizo.

true millionaire ..watapeana sana wazee na vijana kinamama na SERENGETI BOYS....HUWA wakianza kuondoka wanafulululizaga sana tena sanasana wanapokaribia kumaliza miaka mitano...sasa sijui inakuwaga pressure au maneno...lakini kuna haja ya kuonyesha njia kwenye mapambano ya UKIMWI,kwa kuacha tabia endelezi...sasa kama ukiangalia mtu mmoja link inaanzia juu kabisa ....si ajabu mamemo ya millionaire yakatokea!!!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom