Karibu upate ushauri mbalimbali kuhusiana na changamoto za maisha bila malipo

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,047
Heshima kwenu Wakuu.

Naam, hii ni fursa ya kubadilishana mawazo hasa kwa wale wenye changamoto za maisha ili ku-share experiences na skills za hapa na pale. Kwahiyo karibu sana na ujisikie huru. Itapendeza iwapo utaelezea kwa undani kidogo changamoto uliyonayo ili iwe rahisi kusaidiwa.

Je, hakuna harufu ya upigwaji (utapeli) hapa?
Hapana kabisa, sihitaji mtu anifuate inbox wala kubadilishana contact. Tunamalizana hapahapa.

Je, mimi ni mwanasaikolojia au nafahamu kila kitu?
Hapana kwakweli. Mie si mwanasaikolojia wala sifahamu kila kitu. Isipokuwa, nimewekeza kwa muda mrefu kujifunza skills za maisha. Nadhani ni vizuri ku-share maarifa niliyonayo na kwa wengine zaidi.

Je, mimi mwenyewe nimefanikiwa kutatua changamoto zangu?
Kwa kiasi kikubwa ndiyo. Ninayo mapungufu mengi tu kwakuwa sifahamu kila kitu na ninaendelea kujifunza. Ila kwa kiasi chake niwefanikiwa kukabiliana na changamoto nyingi za maisha. Kuishi kwangu vijijini na mijini, ndani na nje ya nchi kumenifanya kukumbana na changamoto nyingi na nimejifunza vitu vingi sana. Mambo mengi mengine nayofahamu yametokana na research zangu binafsi ambazo huwa nazifanya kwa siri. Nikikutana na watu huwa ni msikilizaji zaidi kuliko kuwa muongeaji na huwa natumia skills za research nazojifunza darasani katika kujifunza na kuwauliza watu maswali. Wao huwa hawajui kama nawadodosa ili kupata taarifa flani kuhusiana na mitizamo yao juu ya kile nilichokusudia ila kumbe ndio hivyo huwa natumia fursa hiyo kupata taarifa.

Lengo langu hasa ni nini?
Mie naamini watu wengi wanahitaji maarifa ya namna ya kukabiliana na maisha. Kwahiyo kila mtu mwenye nafasi anatakiwa kuchangia kadri awezavyo kuhakikisha jamii kubwa inapata maarifa sahihi ili tufikie jamii ya watu wenyer impact. Jamii iliyostaarabika na kuheshimu misingi ya sheria na kuwaheshimu watu wengine.

Kwa sasa nipo naandaa kitabu nitakachokipa jina ( Ijue misingi ya maisha). Sasa kabla sijakamilisha kuandika kitabu huwa napenda kupata feedback kwa watu wengine ili nione haya maarifa niliyojifunza yanapokelewa kwa mtizamo upi katika jamii na kipi niboreshe zaidi. Kwahiyo hii ni sehemu ya kufanyia majaribio nilichojifunza kwa muda mrefu kama ni relevant kwenye jamii yetu. Nikipata ukosoaji mkubwa sana nitajifunza jambo, na nikipata compliment napo nitakuwa nimejifunza jambo.

Nadhani nimejieleza vya kutosha, kwahiyo karibuni sana. Karibuni sana tuweze kubadilishana mawazo.
 
Nipo hapa kupokea maswali ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Karibuni. Nitaelezea kulingana na maarifa niliyojifunza kwa muda mrefu kidogo.
 
Back
Top Bottom