Mama Tibaijuka kwanza karibu sana hapa JF.Tunakuahidi ushirikiano kwa mambo ya msingi.
Hata hivyo, pamoja na kukukaribisha, napenda kukuomba umshauri na Rais Kikwete naye ajiunge hapa JF ili aweze kujibu na kufafanua mambo mbali mbali yanayomhusu yeye kama yeye na yale yanayohusu taasisi ya uraisi. Kuna mambo mengine yanahitaji kauli yake mwenyewe na wala si kauli ya wasaidizi wake.
Kama mh. Rais ni member facebook, kwanini asiwe member JF?
Kama mawaziri wake na wasaidi wake wengine wa chama na serikali ni members wa JF kwanini nae asiwe member?
Ni ushauri tu.
Mkuu wa kaya yupo sana umu ndani sema nae kajivalisha jina feki.
Sasa mbona mnaanza kumtisha prof wa watu jamani?Karibu sana Professor,
Wasia wangu kwako hapa ni jamvini la kina watu na wenye tabia mbali mbali hivyo nakuusia kuwa mvumilivu na fikiri kwanza kabla hujajibu kwani unaweza kuta unalumbana na mpinzani wako wa kisiasa hapa jamvini. Halafu ukiteleza ikawa vantage point ya kukumaliza kisiasa kwani siasa za bongo ni za majitaka.
Otherwise, karibu sana kijiweni nitarudi kwenye mada ya mipango miji hasa kwa jiji la Dar kwani tunaumia sana kiafya na kifedha na huu mlundikano uliopo jijini Dar kiasi saa nyingine unaona bora tu tusitembelee hilo jiji au tusije kabisa Tanzania.
nakupongeza kwa kukumbuka lucnde aje
Nimefurahi sana kuingia kwako Profesa Tibaijuka. Ukumbi huu unaogopwa sana na watu wenye makando kando mengi, lakini natambua kuwa wewe si miongoni mwao, ndio maana ukajitokeza wazi kwa ID yako inayotambulika. Karibu sana.