Kanuni na Sheria za Uchaguzi wa kumpata Rais wa Tanzania zibadilishwe

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,786
15,732
Wanabodi habari za siku

Nimekaa nikaangalia namna nchi yetu tunavyoendesha Chaguzi zetu hasa huu Uchaguzi mkuu, na zaidi hapo kwenye Urais.

Urais ni level kubwa sana ya Kiutawala na Uongozi nchi hii na karibu nchi zote Duniani. Rais hatakiwi kupatikana kirahisi rahisi tu.

Mchakato wa kumpata Rais lazima uwe mchakato mgumu wenye lengo la kumpata Rais halisi na anayekubalika na Wananchi wake.

Nchi yetu hii, ina taratibu moja mbovu sana kwenye kumpata Rais.

Sheria yetu ya uchaguzi inatamka kuwa MSHINDI WA KITI CHA URAIS NI YULE ALIYEPATA KURA NYINGI KATIKA UCHAGUZI MKUU.

Sheria hii ni mbovu na imepitwa na wakati. Kwenye nchi yenye Mikoa 31 na Makabila 120+ Rais apatikane kwa wingi wa kura tu?

Ikitokea mimi nimegombea Urais na nikaamua sasa nipige kampeni mikoa 10 tu yenye wapiga kura wengi, na nikapata kura za kuwazidi wengine itakuwa haki? Yaani Rais awe amepata kura kutoka zone fulani tu na bado awe Rais wa Tanzania nzima kisa amepata kura nyingi?

Kwa Dunia ya leo, nashauri Sheria hii ifutwe na uwekwe utaratibu mpya sasa, utaratibu huu uwe kama ifuatavyo.

1. RAIS ANATAKIWA KUPATA 50%+ 1 YA KURA HALALI ZOTE.

2. RAIS ANATAKIWA KUPATA ANGALAU 40% YA KURA KATIKA KILA MKOA KWA MIKOA 20 KATI YA 26 YA TANZANIA BARA + 25% YA KURA ZOTE ZA ZANZIBAR.

IKITOKEA HAKUNA MGOMBEA ALIYEFIKISHA VIGEZO HIVYO, UCHAGUZI URUDIWE KWA DURU YA PILI KWA WALE WAWILI WA JUU.

Utaratibu huu utatupatia Rais anayekubalika katika Eneo kubwa la nchi yetu. Hivyo kuondoa uwezekano wowote wa kupata Urais Kupitia, Ukanda, Ukabila, Dini au hata Matumizi makubwa ya Fedha.

Urais uwe mgumu mtu kupata, ili kuleta ufanisi, kwa sasa ni rahisi mjinga mmoja kushinda uchaguzi kwa kutumia Ukanda au Dini.

Nawasilisha wadau.
Pascal Mayalla
Mohamed Said
 
Sanduku la kura limeibwa na washukiwa wakuu ni CCCCCM.

Kura ya WAZI pekee ukijumlisha na Utaratibu uliopendekeza wa 50+1% ni njia nzuri ya Kupata DIWANI, MBUNGE na RAIS.

Pia utambue kuwa Katiba ya 1977 iliyopo imezeeka kiasi Cha kushindwa kupokea viraka vipya.

Tunataka KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Amen.
 
Sanduku la kura limeibwa na washukiwa wakuu ni CCCCCM.

Kura ya WAZI pekee ukijumlisha na Utaratibu uliopendekeza wa 50+1% ni njia nzuri ya Kupata DIWANI, MBUNGE na RAIS.
Ili kubalance kuwepo % za kukubalika kwa kila mkoa, hii itaondoa ukanda, na mgombea atalazimika kuwa na mikakati halisi ya kupata kura. Kwa maana next Election ni rahisi kupigwa chini.
 
Wazo zuri,

Bt kutekelezeka kwake ni muhimu kuandika KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA kabla haijaitwa KATIBA pendekezwa.

KATIBA iliyopo ya 1977, imezeeka kiasi kwamba ukiweka kiraka kipya, inatatuka.
 
Wanabodi habari za siku

1. RAIS ANATAKIWA KUPATA 50%+ 1 YA KURA HALALI ZOTE.
Naunga mkono hoja
2. RAIS ANATAKIWA KUPATA ANGALAU 40% YA KURA KATIKA KILA MKOA KWA MIKOA 20 KATI YA 26 YA TANZANIA BARA + 25% YA KURA ZOTE ZA ZANZIBAR.
Naunga mkono hoja ila iwe theluthi moja
IKITOKEA HAKUNA MGOMBEA ALIYEFIKISHA VIGEZO HIVYO, UCHAGUZI URUDIWE KWA DURU YA PILI KWA WALE WAWILI WA JUU.

Nawasilisha wadau.
Naunga mkono hoja ila sio lazima uchaguzi urudiwe, afanye coalition kutimiza akidi.
P
 
Wanabodi habari za siku

Nimekaa nikaangalia namna nchi yetu tunavyoendesha Chaguzi zetu hasa huu Uchaguzi mkuu, na zaidi hapo kwenye Urais.

Urais ni level kubwa sana ya Kiutawala na Uongozi nchi hii na karibu nchi zote Duniani. Rais hatakiwi kupatikana kirahisi rahisi tu.

Mchakato wa kumpata Rais lazima uwe mchakato mgumu wenye lengo la kumpata Rais halisi na anayekubalika na Wananchi wake.

Nchi yetu hii, ina taratibu moja mbovu sana kwenye kumpata Rais.

Sheria yetu ya uchaguzi inatamka kuwa MSHINDI WA KITI CHA URAIS NI YULE ALIYEPATA KURA NYINGI KATIKA UCHAGUZI MKUU.

Sheria hii ni mbovu na imepitwa na wakati. Kwenye nchi yenye Mikoa 31 na Makabila 120+ Rais apatikane kwa wingi wa kura tu?

Ikitokea mimi nimegombea Urais na nikaamua sasa nipige kampeni mikoa 10 tu yenye wapiga kura wengi, na nikapata kura za kuwazidi wengine itakuwa haki? Yaani Rais awe amepata kura kutoka zone fulani tu na bado awe Rais wa Tanzania nzima kisa amepata kura nyingi?

Kwa Dunia ya leo, nashauri Sheria hii ifutwe na uwekwe utaratibu mpya sasa, utaratibu huu uwe kama ifuatavyo.

1. RAIS ANATAKIWA KUPATA 50%+ 1 YA KURA HALALI ZOTE.

2. RAIS ANATAKIWA KUPATA ANGALAU 40% YA KURA KATIKA KILA MKOA KWA MIKOA 20 KATI YA 26 YA TANZANIA BARA + 25% YA KURA ZOTE ZA ZANZIBAR.

IKITOKEA HAKUNA MGOMBEA ALIYEFIKISHA VIGEZO HIVYO, UCHAGUZI URUDIWE KWA DURU YA PILI KWA WALE WAWILI WA JUU.

Utaratibu huu utatupatia Rais anayekubalika katika Eneo kubwa la nchi yetu. Hivyo kuondoa uwezekano wowote wa kupata Urais Kupitia, Ukanda, Ukabila, Dini au hata Matumizi makubwa ya Fedha.

Urais uwe mgumu mtu kupata, ili kuleta ufanisi, kwa sasa ni rahisi mjinga mmoja kushinda uchaguzi kwa kutumia Ukanda au Dini.

Nawasilisha wadau.
Pascal Mayalla
Mohamed Said

Wanabodi habari za siku

Nimekaa nikaangalia namna nchi yetu tunavyoendesha Chaguzi zetu hasa huu Uchaguzi mkuu, na zaidi hapo kwenye Urais.

Urais ni level kubwa sana ya Kiutawala na Uongozi nchi hii na karibu nchi zote Duniani. Rais hatakiwi kupatikana kirahisi rahisi tu.

Mchakato wa kumpata Rais lazima uwe mchakato mgumu wenye lengo la kumpata Rais halisi na anayekubalika na Wananchi wake.

Nchi yetu hii, ina taratibu moja mbovu sana kwenye kumpata Rais.

Sheria yetu ya uchaguzi inatamka kuwa MSHINDI WA KITI CHA URAIS NI YULE ALIYEPATA KURA NYINGI KATIKA UCHAGUZI MKUU.

Sheria hii ni mbovu na imepitwa na wakati. Kwenye nchi yenye Mikoa 31 na Makabila 120+ Rais apatikane kwa wingi wa kura tu?

Ikitokea mimi nimegombea Urais na nikaamua sasa nipige kampeni mikoa 10 tu yenye wapiga kura wengi, na nikapata kura za kuwazidi wengine itakuwa haki? Yaani Rais awe amepata kura kutoka zone fulani tu na bado awe Rais wa Tanzania nzima kisa amepata kura nyingi?

Kwa Dunia ya leo, nashauri Sheria hii ifutwe na uwekwe utaratibu mpya sasa, utaratibu huu uwe kama ifuatavyo.

1. RAIS ANATAKIWA KUPATA 50%+ 1 YA KURA HALALI ZOTE.

2. RAIS ANATAKIWA KUPATA ANGALAU 40% YA KURA KATIKA KILA MKOA KWA MIKOA 20 KATI YA 26 YA TANZANIA BARA + 25% YA KURA ZOTE ZA ZANZIBAR.

IKITOKEA HAKUNA MGOMBEA ALIYEFIKISHA VIGEZO HIVYO, UCHAGUZI URUDIWE KWA DURU YA PILI KWA WALE WAWILI WA JUU.

Utaratibu huu utatupatia Rais anayekubalika katika Eneo kubwa la nchi yetu. Hivyo kuondoa uwezekano wowote wa kupata Urais Kupitia, Ukanda, Ukabila, Dini au hata Matumizi makubwa ya Fedha.

Urais uwe mgumu mtu kupata, ili kuleta ufanisi, kwa sasa ni rahisi mjinga mmoja kushinda uchaguzi kwa kutumia Ukanda au Dini.

Nawasilisha wadau.
Pascal Mayalla
Mohamed Said
Haya maoni ni vyema kama yangepelekwa Bungeni maana wao ndo watunga sheria hizi
 
Back
Top Bottom