Kanisa uchaguzi umeisha tuukomboe wakati

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Wapenda wana JF wenzangu. Nimeona niandike makala hii baada ya kuona kuyumba kusikokuwa kwa kawaida kwa kanisa kabla na mara baada ya UCHAGUZI wa mwaka huu (2015) ambao umemuibua Dr. John Magufuli kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchaguzi huu umeshuhudia jinsi ambavyo wanaoitwa watumishi wa Mungu hasa wapentekostel kusimama madhabahuni na kuhubiri siasa. Pia viongozi hao wamediriki kuwaambia waumini wao wamchague Mhe. Lowassa kwa kuwa ndie chaguo la Mungu.

Wapo manabii na mitume, wachungaji nk ambao walidiriki kusema wakatwe kichwa Mhe. Lowassa asipoingia Ikulu. Hii inaashiria imani kuu pasipo Shaka na usikivu mkuu wa mungu waliyemsikia. Watumishi hawa wamewafungishaa watu wengine siku 21, wengine siku 40 nk ili Mhe. Lowasa awe Rais na sio kuomba Mungu awape Rais aliyeupendeza moyo wake.

Tumeshuhudia mgombea mmoja akitinga Kanisani na kuomba huruma za kanisa na waumini wa dhehebu fulani. Yako mengi naomba niishie hapa kwa eneo hili na nianze kutoa hoja.

1. JE WALIISIKIA SAUTI YA MUNGU?
Baada ya matokeo kutoka ninao ujasiri wa kusema hawa ndugu hawakuisikia sauti ya Mungu bali walikuwa wanatembea kwenye kivuli cha MAHABA kilichojaa ubatili wa nafsi zao.

Yeremia 23:16
"Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha Bwana"

2. JE WALIENDA MBELE ZA MUNGU WAKIWA NA VINYAGO?
Inawezekana kabisa hawa watumishi wa Mungu walisimama madhabahuni wakiwa na vinyago katika mioyo yao. Mungu alipotazama maombi yao alibaini ni ubatili mtupu. Walikuwa wakifanya kwa haja ya mioyo yao na sio mapenzi ya Mungu.

Ezekiel 14:3-5
"Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote? Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;"

3. JE MUNGU AMESHINDWA?
Jambo moja linanitatiza na kuusumbua moyo wangu ni imani za watumishi hawa na watu wao. Kama ni kuomba wameomba sanaaaaaa!!! Kama ni Kufunga wamefunga sanaaaa na kuomba. Swali linakuja; Je waliomba sawa na mapenzi ya Mungu au haja za mioyo yao??? Je Mungu huwa anashindwa?

Wanaenda mbali zaidi katika kunishangaza ukomavu wao wa kiroho pale wanaposema waliibiwa kura.. Je huyo Mungu wanayemuamini alishindwa kuzuia huo uovu? Kweli mwanadamu kupitia TUME na CCM anaweza kuzuia kusudi la Mungu? Ina maana Mungu wa CCM ni mkuu kuliko Mungu wa UKAWA? Mkono wa Mungu ulishindwa kuwafikia waovu wote waliokuwa wamejipanga kuiba kura na kuwazuia? (kama kweli waliiba)
Kweli wajameni Mungu ashindwe na mwanadamu ( WATU WA TUME NA CCM?) kama ni kweli basi something is wrong somewhere!

Isaya 59:1
"Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;"

Mungu ninayemjua Mimi ni Mungu mwenye enzi, muumba mbingu na nchi na hajawahi kushindwa. Mapenzi Yake hutimia sawa na sala ya Baba yetu uliye mbinguni.

Mathayo 6:9-10
"Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni"

Mungu ANAJIBU maombi yetu SAWASAWA na mapenzi Yake makamilifu kwetu.

4. MUNGU HUMUINUA YULE AMTAKAYE.
Madaraka yanatoka kwa Mungu. Mungu HUMUINUA yule amtakaye.

1 Samwel 2:8
"Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake"

Daniel 4:17 (b)
"....kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge."

5. JE HESHIMA YAO KWA WAUMINI SASA KWA JAMII IKOJE?
Nabii anapotabiri na unabii wake usipotimia neno la Mungu linasema apogwe mawe. Mungu sio kigeugeu.

Kumbukumbu la Torati 13:5 (b)
"Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu.."

Kumbukumbu la Torati 13:20
"Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa."

6. JE MWILI WA KRISTO UMEUMIA AU UMEUMIA WEWE BINAFSI?
Mwili wa Kristo hauwezi kuumia kwa maunabii ya uongo!! Zaidi ni kuumiza mwili wa Kristo na kumsulubisha mara ya pili. Wewe unayejiita mtu wa Mungu, Je unaujenga mwili wa Kristo au unauhuzunisha kwa kupingana na kweli ya Kristo. Hebu kaa chini upya ondoa vinyago moyoni utafute upya uso wa Mungu na ndipo utaisikia tena sauti yake.

Mungu anaenda kuijenga upya Tanzania yetu kupitia sisi wenyewe wa Tanzania wala sio kupitia mtu wa nchi nyingine. Acheni uvivu wa kuomba na kusoma neno la Mungu ili kuzijua ahadi za Mungu. Tembeeni mkiwa mmembeba Kristo badala ya kubeba watu na majina ya watu. baba jina la Jehovah.

Tanzania itajengwa na Mimi na wewe tuliofinyangwa na Bwana kwa udongo wa Tanzania. Baraka zetu Ziko Tanzania. Ni wakati wa kumlingana Mungu ili kile tulichokipoteza muda mrefu kirejeshwe kwa kupitia uongozi Mungu aliyotupa na sio kwenda kinyume nao.

1 Timotheo 2:1-2
"Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu."

Warumi 13:1
"Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu"

MWISHO
Naomba uelewe nilichoandika na hakuna haja ya kubishana ki ushabiki. Tupo hapa kuijenga nchi yetu. Jiulize umejiandaa kufanya nini katika awamu ya tano.

Je unataka Mungu akutumie katika eneo gani kimwili na kiroho. Je mzigo wako unataka uongozi wa awamu ya tano ufanye nini kwa Taifa hili. Haya huwezi kuyaona na kuyaombea Kama bado uko kwenye malumbano. Hebu na tuukomboe wakati. Achana na mafundisho potofu uliyopokea yenye kuharibu akili. Roho Mtakatifu ni Mwalimu wa kweli, ni mfariji wa kweli. Mruhusu akuongoze tena, rudi tena msalabani ambako baraka zako zipo.

Wale mnaopenda kupingana na neno la Mungu; ni maombi yangu neno la Mungu lijitetee lenyewe, maana Mungu hujipigania mwenyewe. NENO LA MUNGU NI MOTO NA UPANGA UKATAO KUWILI.

Tanzania ni yetu tusimame pamoja bila kujali dini zetu, itikadi za vyama au makabila.

Mungu awabariki sana na ninawapenda.

Queen Esther
 
Nimetafuta neno FAFADHALI kwenye kamusi nimelikosa. Ngoja niendelee na kulisaka maana yake
 
Njia za MUNGU sio kama za wanadamu. Ukombozi wa wana Israel ulianzia pale MUSA alipookotwa na binti Farao. Ukombozi huwa ni process na wala siyo kitu cha siku moja. Kumbuka mbele za MUNGU siku moja ni kama miaka elfu. Ukombozi wa mwanadamu ulianzia bustani ya edeni, pale MUNGU aliposema uzao wa mwanamke utamponda ibilisi kichwa Mwanzo 3:15, na ulitimia YESU alipokwenda calvary. Ukombozi is a process. In the spiritual realms,the battle is already won. Remember we walk by faith and not by sight.

Kumbuka haikuwa rahisi farao kuwaachia wana wa Israel kuondoka ili kwenda kwenye ya ahadi kufanya ibada, baada ya mapigo kumi ndio farao aliwaruhusu wana wa Israel kuondoka. It didn't happen in one day. Pia baada ya kufika nchi ya ahadi MUNGU hayakuondoa yale mataifa yote kwenye nchi ya ile kwa wakati mmoja, na alikuwa na sababu nyingi sana na za msingi Kutoka 23:29.

Kumbuka pia haki huinua taifa methali 14:34, na misingi ya kiti cha enzi cha MUNGU Baba ni haki(rigtheous and justice are the foundations of GOD's throne) zaburi 89:14. MUNGU kamwe si dhalimu, hawezi kutimia njia zisizo za haki kutimiza makusudi yake. He is a great GOD, na YEYE siyo kiziwi hujibu kwa wakati. HE is also full of suprises. Huwa wakati mwingine anajibu tusivyo tegemea. Kumbuka baada ya Daudi kupakwa mafuta kama mfalme aliendelea kuchunga ngombe ingawa MUNGU alikuwa ameshaundoa utawala wa Sauli wa kumkabidhi Daudi mwana wa YESE siku ile alipoasi 1 samuel 28:17.
 
Siyo nafasi yako kukosoa waliyosema au waliofanya hao watumishi wa Mungu. Hiyo ni kazi ya Mungu sio yako. Usijitafutie dhambi kusema watumishi wake, kaa kimya simama na Mungu wako.
 
Back
Top Bottom