Kanisa lanusurika kuteketea kwa moto Zanzibar asubuhi ya leo...

Status
Not open for further replies.
Kuna uwezekano mkubwa haya mambo yanafanyika kwa agenda ya siri ya kutaka kuvuruga amani yetu huku wakijificha kwenye uislamu ( ilhali waislamu ni watu wenye upendo)......tuwe makini na kuwatupia waislamu lawama ama kuhusika na kila kinachotokea.....
 
breaking news ya asubuhi ya leo kanisa la shalom ministry mkoa wa kusini unguja limechomwa moto na watu wasiojulikana.Hakuna majeruhi wala vifo,hakuna aliyekwisha kamatwa upelelezi unaendelea.

source:ITV breaking news/radio one and capital tv,imedhibitishwa na kamanda wa polisi zanzibar,Augustino Ulomi.

Mungu mkuu tuokoe na waovu hawa. Hivi makanisa na viongozi wake wamefanya uovu gani mpaka wakastahiri haya yanayowapata?
Wapi viongoz wetu wa nchi ambao waliapa kwa misaafu kuwalinda watz na mali zao?
 
Nami nimesikia breaking news hizo kupitia ITV. Ngoja tusubiri wenye details zaidi watujuze.
 
Wana-JF, kwa mujibu wa Radio Wapo, ni kwamba kuna Kanisa limechomwa huko Zanzibar alfajiri ya leo.

Moto ulizimwa, na hakuna majeruhi,ila eneo la Madhabahu liliungua

#
Ni vibya kutumia neno la uwongo lakini hapa nalazimika kumwita mtoa habari ni muongo na yaelekea hana nia njema na zanzibar na huenda antaka kugombanisha watu wa dini tofauti badala ya kusuluhisha.naomba anambie pahala gani sasa hivi mimi niko unguja takwenda kuchukua Picha.
 
Kuna kitu kinapikwa, harufu inasikika kwa uhodari wa wapishi!...Intelligensia ya nchi hii iko wapi? vyombo ya usalama zindukeni, acheni kulala usingizi fofo; haya yanayotokea ni muondelezo wa kukolezea mpasuko baina yetu kwa manufaa yao...
 
ZANZIBAR TENA
Kanisa lanusurika kuteketea
kwa moto Zanzibar asubuhi ya
leo... - Lilirushiwa kitu kama
bomu
kilicholipuka moto japo majirani waliamka na kuuzima
moto huo kabla kuleta madhara
makubwa.
- Tukio hilo limejitokeza
asubuhi ya leo kwenye mida ya
saa kumi. - Hakuna chombo cha dola
kilichofika eneo hilo hadi mida
ya saa 1 asubuhi
 
Kuna mtu alichangia kwa kusema tusiwahusishe Waislamu na tukio la kifo cha Paroko, na hapa anatuambiaje? kama kweli taarifa hizi zitakuwa za kweli basi tunafungua ukurasa mpya wa ugaidi Zanzibar!

Hatujawahi kusikia misikiti imechomwa moto,au shehe/kiongozi wa kiislam ameuliwa,viongozi wa nchi ambao 90% ni waislam wamekaa kimya.Kwa nini Wakristo wasiamini kuwa waratibu wakubwa wa mpango huu wa kuchoma moto makanisa,kuwaua wachunga na mapadri ni viongozi tokea Rais na wasaidizi wake ila wanawatumia vikundi vidogo ambavyo serikali haivichukulii hatua zozote.Huu ni mpango wa kuifanya nchi iwe ya kiislam kama ilvyo Nigeria.KIKWETE UNAIPELEKA NCHI KUBAYA SANA.
 
naomba watanzania tutulie,japo yule muovu anajaribu kuwajaribu tutoke kwenye imani ya umoja ya ngao ya upendo.tuombe uvumilivu wa miyoyo na kutafuta kina cha matukio haya,ndio tusiende na kuhisi japo hupelekea kwenye tafiti za kina na kuweza kupata ukweli,tusihisi kuhukumu.kwani kuna michezo mingi huchezwa kupelekea jambo fulani kutekeleza azma fulani.tuiombe busara kuwa nasi tukishughulikia haya maasi yalengayo kutujengea hisia nchi inatumbukia kwenye vita udini.
 
Kweli Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.

Naona aibu kuendelea kujisifu kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani maana majanga yamezidi, Elimu Janga la kitafa, Vitu feki Tanzania ni janga la Kitaifa, Wanasiasa ni porojo na kutoka mapovu tu hawana solution ya matatizo zaidi ya kuongozwa na matukio na kujali masllahi yao nao wamekuwa ni majanga ya kitaifa, Huduma za kijamii ni janga la kitaifa watu wanajipandishia bei za vitu watakavyo, hakuna wa kukemea yote ni majanga ya kitaifa. Udini nao siusemei maana tuendako wale waliooana waksto na waislamu sijui nani atamkataa mwenzie maana hakuna famili ambayo haijachanganyika! Adui yetu ni nani hatumjui?:help:

Kilimo kwanza nalo ni janga la kitaifa mikoa mbalimbali inazidi kukumbwa na njaa, migogoro ya wakulima na wafugaji linazidi kuwa janga la kitaifa kila kukicha, Imani za kishirikina nalo ni janga la kitaifa, Sasa tena janga la kuchinja (inachekesha sio kwa furaha bali huzuni), Uhalifu ndo usiseme. Kila nikitazama naona Mambo yote ni ubatili mtupu. Kweli siku za mwisho upendo wa wengi utapoa.

TANZANIA INA MAJANGA MENGI YA KITAIFA MATHALANI
1.WABUNGE WENGI BUNGENI KWA SASA NI JANGA LA KITAIFA
2. ELIMU YETU SI JANGA TU BALI KIFO KWA TAIFA
3. UTAWALA BORA JANGA LA KITAIFA
4.UWAJIBIKAJI OFISI ZA SERIKALI JANGA LA KITAIFA
5. RUSHWA KUONGEZEKA SANA JANGA LA KITAIFA
6. TATIZO LA MAJI KWA WANANCHI JANGA LA KITAIFA
7. RESOURCES ZETU KUCHUKULIWA NA WAGENI..JANGA LA KITAIFA
8. SUPIKA WA BUNYE JANGA LA KITAIFA
9. SIASA ZETU JANGA LA KITAIFA
10. UDINI JANGA LA KITAIFA
11. n.K JANGA LA KITAIFA

IMEBAKI KUMUOMBA MUNGU TU ILI MAJANGA HAYA YASITULETEE MATATIZO!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom