Kanisa Katoliki kujadili ombi msamaha wa Sitta

nimesikia na kusoma katika vyombo vya habari edward lowassa akihutubia katika maadhimisho ya miaka 50 ya jimbo katoliki la morogoro akiliomba kanisa katoliki radhi kutokana na matusi yaliyoelekezwa kwa maaskofu wa cct wakiwemo wa kanisa hilo na mwenyekiti wa lililokuwa bunge maaalumu la katiba aliyewaita maaskfu hao mashetani. ninavyojua mimi mtu akikosa ni lazima kwanza aone uchungu na chukizo kwa kosa lakie kisha yeye mwenyewe aamue kuomba radhi/msamaha ili asamehewe. sijaelewa ni nini hasa kimemsukuma lowassa kujitwika zigo la kutubia na kuomba msamaha kwa ajili ya dha,bi na udhalilishaji mkubwa aliofanya samwel sita(hasimu wake wa kisiasa) ilihali sitta mwenyewe ameridhika kwa kile alichowatamkia maskofu.hivi kama lowassa aliguswa na matusi yale kwanini hakuyakemea kipindi kilekile kama alivyokemea tatizo la ajira kwa vijana?
nawasilisha.
Kila jambo na nyakati zake, huuitaji kuwa professor kulijua hili by the way kwa nini jana mlimpiga Warioba baada ya kupewa ela na Membe na Sita
 
Busara ya upendo

Hakuna kuitwa mjinga na mpuuzi mara 2 hiyo hiyo mara mja tayari ameshawaita na wakiristo watabaki kuwa wapuuzi tu. sasa kama ni msamaha dawa yake katiba aliyoipitisha Sitta kwa ubabe ipigiwe kura ya HAPANA vyenginevyo ni kukubali wakiristo kuwa wapuuzi zaidi na zaidi.
 
Hakika dada. Hawa Nipashe, ITV na Radio One ni vyombo vya habari ambavi vipo kimipasho kwa lengo la kumjenga mtu fulani na kumbomoa mwingine

Laana ya kuwashambilia wazee wako itakuandama kwa utovu wako wa nidhamu pimbi wewe.... Unampiga Jaji Warioba kwa lipi? Hoja si hujibiwa kwa hoja? Mpuuzi kabisa wewe!
 
1:Lowassa angekua na Busara angepinga waziwazi kitendo hicho bungeni na pia angepinga maoni ya wananchi kupuuzwa

2:Angekua na nia njema basi angepinga kuondolewa kipengele cha Tunu za Taifa.Maadili ya viongozi yameporomoka kutokana na kukosekana kwa kipengele hiki ambacho viongozi wa Dini walikua wakipigia kelele

3:Sitta alipaswa aombe radhi yeye kama yeye na sio Lowassa kuleta unafiki wa kujijenga kisiasa na kujisafisha kwa tuhuma alizo nazo ambazo pia ni zao la ukosefu wa tunu za taifa

4:Mimi kama Mkristu tena Mkatoliki mwenye msimamo wa kiimani sitapenda kuona Maaskofu wakilidhalilisha kanisa kwa kuwaendekeza wanasiasa aina ya Lowassa na Sitta na siasa zao za majitaka

5:Kanisa lionyeshe msimamo kuhusu waraka wao
 
Maaskofu japo imeandikwa samehe lakini jueni nasi wafuasi wenu tuliumia sana. Aende kanisani mbele ya Maaskofu wote aombr mwenyewe nasi tukishuhudia. Utaombaje msamaha kishenzi shenzi vile halafu ukubaliwe?
 
kaka. that smartness you have doesn't match the cerebral capacity of most of members here.
ulichokisema ndicho kilicho sahihi 100% tatizo ni kwamba, huu msusruru wa wajinga humu wana uwezo wa kujua hilo!!!
Smartness?my ass!Mtawapata wajinga wachache lakini siyo mimi,Mimi kama Mkatoliki msimamo wangu upo pale pale,Lowassa hapaswi kumwombea msamaha Sitta,Wajua kwanini Lowassa amelazimika kumwombea msamaha Sitta?Ni kwasababu anataka kutuliza hasara za Wakatoliki ili wasije wakaikwamisha katiba pendekezwa ambayo Lowassa ni miongoni mwa beneficiaries wakubwa.Usitaka kutupupambaza,We are smarter than you could ever imagine!
 
Lowassa--Novermber3-2014.jpg

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana,Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.

Kanisa Katoliki Tanzania, limesema uamuzi wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kuliomba radhi Kanisa hilo kufuatia migongano iliyojitokeza kati ya viongozi wa serikali na wa Bunge Maalum la Katiba (BMK), ni jambo linalojadilika.
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, alisema pamoja na uamuzi huo wa busara aliouchukua Lowassa, jambo hilo ni la hekima na kama litajitokeza katika mkutano ujao wa Baraza hilo utakaofanyika kesho litajadiliwa na kutolewa maoni ya pamoja ya Baraza.
¡°Ninakaa na wenzangu wa Baraza la Maaskofu, Novemba 4,mwaka huu (kesho), nalisubiri kama suala hilo la msamaha kama litakuja kwenye sura kama hiyo, tutalijadili na tutatoa maoni ya pamoja ya Baraza,¡± alisema Askofu
Ngalalekumtwa na kuongeza: Alisema kama huyo aliyeambiwa (Askofu wa Mahenge) atalileta kama ajenda tutalijadili.¡±
Askofu Ngalalekumtwa alisema mtu mmoja hawezi kutoa tamko hadi wakae kama Baraza kutoa maoni ya pamoja.
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli, aliomba msamaha huo wakati akitoa salamu zake katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge, mkoani Morogoro wiki iliyopita. Alisema Kanisa Katoliki lina mchango mkubwa katika kudumisha amani na mshikamano nchini, hivyo mambo yaliyojitokeza yanapaswa kusamehewa.
¡°Najua hivi karibuni tumewaudhi, lakini mimi naomba mtusamehe bure tu, kama vile mzazi anavyomsamehe mtoto wake anapokosea,¡± alisema Lowassa na kuongeza kuwa Kanisa Katoliki ni muhimu katika maendeleo ya nchi.
Ingawa Lowassa hakueleza kwa undani tofauti zilizojitokeza kati ya Kanisa hilo na baadhi ya viongozi wa serikali, lakini wakati BMK likiendelea, taasisi za dini zilisambaza waraka uliosainiwa na viongozi wake ukilikosoa Bunge hilo kwa mambo mbalimbali ikiwamo kuendelea kujadili rasimu bila maridhiano kutokana na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia.
Kadhalika, viongozi wa madhahebu hayo ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT) na Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walilikosoa BMK kwa kupuuza maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Waraka huo ulisababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kujiweka katika wakati mgumu kwa kuzua mgogoro dhidi ya viongozi wa dini ya Kikristo, baada ya kuita waraka huo kuwa ni wa kipuuzi na wa ovyo ovyo.
Sitta ambaye alitoa kauli hiyo Oktoba Mosi mwaka huu, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa waraka wa maaskofu una lugha ya Ukawa, ingawa maaskofu kwa upande wao waliueleza kuwa ni waraka wa kinabii, kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.
Sitta alitoa kauli ya kuuponda waraka huo bungeni alipokuwa akielezea mwenendo wa upigaji kura za kupitisha ibara na sura za rasimu ya katiba iliyopendekezwa kabla ya upigaji wa kura na wakati wa kutangaza matokeo, akisema watu wa Mungu kama maaskofu hawawezi kutoa waraka kama huo na kudai kuwa amekuwa akituhumiwa kwenye mitandao kwamba anadharau maaskofu.
¡°Nimalizie na viongozi wangu wa kiroho¡-mababa zangu maaskofu, natuhumiwa sana kwenye mablog kwamba nadharau maaskofu. Wakiwa na matendo kama hayo hao baadhi ya maaskofu itabidi tuendelee kuwadharau,¡± alisema na kuongeza: ¡°Ninao waraka huu ambao umelazimishwa kutumwa katika makanisa. Sioni utukufu wa Ukristo katika waraka huo. Huu waraka unamwamuru Rais airudishe Tume ya Mabadiliko ya Katiba.¡±
Kuna Ukristo hapa?¡± Alihoji na kuendelea: ¡°Waraka huu unamlazimisha Rais asitishe mchakato wa Bunge Maalum¡-tangu lini watu wa kiroho wanatoa maagizo ya kisiasa? Hii siyo haki hata kidogo¡-kuna Ukristo hapa? Waraka una lugha za wale Ukawa tuliowazoea.¡±
¡°Hivi kweli maaskofu wa Kikristo wanaweza kusema kwamba Wizara ya Katiba na Sheria irudishe tovuti ya Tume ya Jaji Warioba na kuirejeshea nyaraka zake zote ili wananchi wasome na kujifunza?¡± alihoji Sitta.
¡°Kwamba maoni ya wananchi hayawezi kufutwa na kudharauriwa na chama tawala, hivyo basi Bunge la Katiba lijadili na kuboresha tu rasimu ya katiba na si kubadilisha,¡± alisema Sitta.
¡°Waraka huu kwa shinikizo la maaskofu umesambazwa kwenye makanisa na kusomwa. Mimi nasema kama Mkristo, tukianza kuruhusu nchi yetu kutoa nyaraka hizi za kisiasa zisomwe makanisani kwa kudai huo ni msimamo wa maaskofu, basi nchi hii tutaipeleka kubaya. ¡°Na mini kama mtu mzima lazima nionye kuhusu tabia hii, ukizingatia nchi hii haina dini, hawa baadhi ya maaskofu ambao walikusanywa Dar es Salaam na makundi yale yale yanayohusishwa na Ukawa, kama wao ni wanachama wa siri wa vyama vya siasa vinavyochukia CCM wajitokeze waziwazi,¡± alisema Sitta.
Sitta aliendelea kunukuu waraka huo kwamba kuna askofu mmoja ameapa kwamba atawaelimisha waumini wake ili siku za usoni wawashughulikie viongozi kama mimi (Sitta). Nasema aendelee, lakini Mungu anaona yote yaliyo moyoni mwetu.¡± Baada ya Sitta kutoa kauli hiyo, Askofu wa Jimbo la Katoliki la Bunda, Mhashamu Renatus Nkwande, alisema matamshi ya Sitta yanaonyesha anavyohangaika kualalisha kilicho haramu.
Alisema kitendo cha Sitta kuendesha BMK kwa kukejeli wajumbe wenzake walioondoka bungeni (Ukawa) na wajumbe walioandaa rasimu ya pili kwenye Tume ya Katiba Mpya chini ya Jaji Joseph Warioba, ni jambo la aibu ambalo halivumiliki, na ndiyo maana walitoa waraka wa kutokubaliana nacho. ¡°Kwa kweli Sitta ametutukana, ametafuta ubaya kwa viongozi wa dini, kwa kuwa tumesema ukweli ? Sisi tulikuwa tunatimiza wajibu wetu kwa Wakristo ¡-tulizungumza kutokana na hitaji la wakati, na ulikuwa waraka wa unabii,¡± alisema.
Viongozi wengine wa kanisa Katoliki waliojibu kauli za Sitta ni Makamu Mwenyekiti wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini, ambaye alinukuliwa akisema kuwa Sitta amelewa madaraka.
Wakati hayo yakiendelea, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Anthony Komu, amesema viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Sitta ndio waliopaswa kuliomba msamaha Kanisa.
Akizungumza katika mikutano iliyofanyika Kata za Mabogini, Kibosho Magharibi na Kibosho Kirima, Jimbo la Moshi Vijijini kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali za serikali za mitaa, Komu alisema:
¡°Unawezaje kuwaombea msamaha watu ambao hawajui kama wamefanya kosa.
¡°Angeishauri CCM na serikali yake imwambie Sitta ajutie kosa lake kwa kuwakebehi viongozi wa dini waliotoa mawazo yao kuhusu kupuuzwa kwa maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.¡±

CHANZO: NIPASHE
 
Kumbe hata sakramenti ya upatanisho au kitubio sasa tutatuma mawakala kutufanyia maungamo. Hakuna umuhimu wa mtenda dhambi kwenda mwenyewe na kwa kinywa chake mwenyewe kumuungamia padri dhambi zake na kuomba msamaha.

CHANZO: NIPASHE[/QUOTE]
 
Sitta anautaka urais alidhani watanzania watamshangilia kwa kuwapa katba lakn ndo amejitengenezea jeneza na kabur lake ataliona kwny kura ya maon na mwkn ndo utakua mwk wake wa mwsho kuliona bunge kwa sababu ya ubnafsi
 
Pamoja na msamaha huo hata kama utatolewa kama ilivyo kawaida ya Wakristo, ninaomba wawasamehe ccm lakini katiba wasiikubali kwa sababu msamaha usiokuwa na marekebisho ni unafiki.

Yule mtoza ushuru Zakayo alipoenda kutubia makosa yake kwa Bwana Yesu alisema "...na ikiwa kuna mtu nimemdhurumu, nitamrudishia mara nne..."

Lowasa anaomba msamaha kama BMK, Ccm, Mbunge, raisi mgombea, ama Serikali?

Katika kuomba msamaha huko anarudishaje mali zetu alizotufisidi? Mbona haziongelei kama ni toba ya kweli?

Tatizo kubwa si matusi ya Sita, sita alikuwa anatekeleza ilani ya ccm. Ccm imekubali kurekebisha makosa? Ni kweli lowasa katumwa na ccm? Makosa ya ccm ya kubinafisisha katiba yatarekebishwaje?

Ikumbukwe kuwa tamko la Ma askofu halikutolewa kwa ajili ya PRIDE za hao wajumbe ama kanisa. Mzizi wa matamko na muafaka ule ilikuwa ni uchakachuaji wa katiba, ubinafsi wa ccm kuweka mbele maslahi yao katika katiba huku wakitupilia mbali maoni ya watanzania. Na uchakachuaji huo umeendelea hadi kwenye ngazi za kura yakupitisha hilo rasimu.
SASA HIII TOBA YA LOWASA ITAREKEBISHAJE MATATIZO WALIYOYOFANYA KATIKA MCHAKATO NA MUUNDO MZIMA WA KATIBA WALIYOIPENDEKEZA?

My take:- Lowasa kama anatubu:-

1. Arudishi mali alizofisidi taifa.
2. Ccm wa withdraw likatiba lao wanaloendelea kulishinikiza kwa wananchi huku wakizuia kila uwezekano wa kuilewa.
3. Wakiri kwa taifa kwamba pamoja na uchakachuaji wa kibinafsi walioufanya, lakini pia wamegushi kura za kuipitisha na hivvyo kila kitu pale ni fake.
4. Wawaombe radhi watanzania kwa uharamia wa kuteka mchakato wa katiba na kuufasidi.

KINYUME CHA PALE, BABA ASKOFU NA WENGINE, TOBA YA LOWASA NI MANIPULATIVE NA LENGO LAKE SI KUREKEBISHA MAKOSA BALI ANASAKA KUUNGWA MKONO YEYE NA CHAMA CHAKE KWENYE URAISI.

Nina imani na ufahamu wa viongozi wangu wa dini kwamba ni wasomi na waelewa kuliko kundi lolote wa mambo ya dunia na ya kiroho. Hawatakuwa manipulated so cheaply na hila za fisadi lowasa anayetakakuwatumia kufanikisha uhuni wa ccm hasa kwakuzingatia lowasa anaamni yeye ni mgombea uraisi. anataka katiba ipite ili imlinde katika ufalme wake wa kifisadi.
 
Sitta is beyond redemption. Usaliti wa Sitta kwa watanzania zaidi ya dhambi asili.
 
Yule mwanamke mzinzi aliposamehewa kuuawa kwa kupigwa mawe. Yesu aliwaambia wale washitaki wake "asiye na dhambi kati yenu, awe wa kwanza kumtupia jiwe huyu mwanamke". Wote waliondoka.

Yesu akamwambia "Enenda zako naUSITENDE DHAMBI TENA". Baada ya kusamehewa, kama ni lowasa, ccm, serikali , bmk ama nani sijui aliyekuwa amewakilishwa na lowasa, ,WASIENDELEE NA DHAMBI YA KUSHINIKIZA LI KATIBA FAKE WALILOGHUSHI KWA HILA YA KULINDA WIZI, UFISADI, DHURUMA, MAUAJI YA RAIA, UGANDAMIZAJI WA DEMOCRASIA HUKU WAKIWAUMIZA WATANZANIA TENA.

UDANGANYIFU WOTE WALIOKUWA WAKIUFANYA WAACHE MAANA SASA WAMETUBU NA WASAHAU LI KATIBA LAO LA KIPUMBAVU ILI WAGEUKE NA KUANZA KUFANYA MASUALA KWA HAKI

Zakayo aliposamehewa alirudisha mali alizokwiba mara nne. Kama kweli ni toba sahihi Lowasa na mafisadi wenzie wa ccm, kwa kuwa wamebaini makosa yao, na kama kweli wanamaanisha wanachokisema, warudishe mali walizoiba kwa taifa na wasirudie ujinga huo tena.

Kinyume cha pale huu ni usanii mtupu wenye lengo la kutafutwa kuungwa mkono na kanisa kwenye katiba na utawala wao wa kifashist.
 
Huwezi kuomba toba ukiwa umetengeneza dhambi huku unaendelea kuitenda na bado unaitetea!

Hii ni sawa na mwanume shoga anaye tubu huku akiendelea kufanya ushoga na akipigania watu wengine wayakubali matendo ya ushoga na wajiunge naye.

Maaskofu ni wasomi wazuri wa elimu zote, za dini na za kidunia, watamsamehe kwa matamshi ya dharau dhidi yao lakini hawawezi kukuikubaliana na katiba anayo ipendekeza kwani bado ipo labda aiondoe.
 
BAdo sikubaliani na Toba ya Lowasa.

Kwa nini aende Lowasa na siyo SITA aliyetukana??????

Kitubio gani cha uwakilishi????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom